Uhakiki wa Mtindo katika Riwaya ya Kiswahili: Mifano Riwaya za Kidagaa Kimemwozea na Chozi la Heri
Ikisiri
Utafiti huu ulikusudia kuchanganua matumizi ya mtindo katika riwaya za Kidagaa Kimemwozea (2012) ya Ken Walibora na Chozi la Heri (2017) ya Assumpta Matei. Mtafiti aliongozwa na malengo mahususi matatu ambayo ni; kuchunguza baadhi ya mbinu za kimtindo, kujadili athari za mbinu za kimtindo katika usawiri wa wahusika na kujadili mchango wa mbinu teule katika ujenzi wa maudhui kwa mujibu wa riwaya teule. Mtafiti alitembelea maktaba ili kusoma kazi za waandishi zilizojikta kwenye mada zilizo na uhusiano na mbinu za lugha za fasihi. Mtafiti alisoma tasnifu, magazeti, majarida pamoja na vitabu vya waandishi tofauti. Mtafiti pia alisakura kwenye mitandao ili kuboresha data yake kwa kuangazia kazi za wasomi tofauti kuhusiana na mada kusudiwa. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Umitindo iliyoasisiwa na Buffon mnamo mwaka wa 1930. Mihimili minne ya nadharia hii ilitumika kuchunguza matumizi ya mbinu tofauti za mtindo, namna zilivyotumika katika usawiri wa wahusika na kisha mchango wa mbinu angaziwa katika ujenzi wa maudhui. Mbinu ziliochunguzwa ni sadfa, mbinu rejeshi, hadithi ndani ya hadithi, tashbihi na majazi. Data ilichanganuliwa na kuwasilishwa kimaelezo kwa kujikita kwenye mihimili ifaayo. Utafiti huu utarutubisha maarifa kwa wasomaji wanaovutiwa na mbinu tofauti za lugha zilizotumika katika tungo. Pia, utafiti huu utawafaidi walimu na wahadhiri kwa kuwa na uelewa zaidi kuhusu mtindo wa kifasihi wanapofundisha wanafunzi wao. Vivyo hivyo, utafiti huu utafaidi watafiti wa baadaye watakaokuwa na nia ya kuchunguza mitindo katika kazi za fasihi. Hatimaye, utafiti huu utatumika kama marejeleo kwa kazi za baadaye za ubunifu na haswa zile zinazohusiana na mtindo katika fasihi
Upakuaji
Marejeleo
Aboge, A. (2021). Stylistic Devices: Narative Fiction. Nairobi: Phoenix Publishers
Arege, T. (2007). Chamchela. Nairobi. Jomo Kenyatta Foundation.
Babbie, E. (1999). The Basis of Social Research. Belmont: Wadsworth Publishing Company
Buffon, G. (1930). Buffons Discourse on Style. Paris Librairie: Hatier Publishers
Davison, M. (2019). ‘‘Uchambuzi wa Takriri ya Msamiati katika Nyimbo za Tamthilia ya Nguzo Mama’’Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Dar es Salaam. Institute of Kiswahili.
Gora, M. (2007). Analysis of Language used by Matatu Conductors. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa)
Hebert, A. (2016). The Role of Euphemisms in Healthcare Communication. Journal of Healthcare.Volume 1. No .2. 14
Matei, A. (2017). Chozi la Heri. One Planet Publishing & Media Services Limited
Marani, J. (2006). ‘‘Fasihi Simulizi Nguzo ya Fasihi Andishi: Mfano wa Riwaya ya Walenisi’’ Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Kenyatta (Haijachapshwa)
Msokile, M. (1992). Misingi ya Hadithi Fupi.Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press
Mohammed, S. (1980). Dunia Mti Mkavu. Nairobi: Longman
Muhando, P. (2010). Nguzo Mama. Nairobi. Muwa Publication Limited
Ntarangwi, M (2004). Uhakiki wa Kazi ya Fasihi. Augustana College. Rock Island
Obwogi, D. (2022). ‘‘Tamathali za Usemi, Mbinu Rejeshi na Taswira katika Utenzi wa Vita vya Uhud’’ Makala ya Mawasiliano ya Chuo Kikuu cha Nairobi.
Okwena, S. (2013). “Matumizi ya Jazanda katika Tamthilia Tatu za Timothy Arege.” Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa)
Ngara, E. (1992). Stylistic Critisim of the African Novel, London. Nairobi: Heineman.
Senkoro, F. (2011) Fasihi. Dar es Salaam: KAUTU Ltd.
Wafula, R. (1999). Uhakiki wa Tamthilia: Historia na Maendeleo yake. Nairobi: Kenya Literature Bureau
Walibora, K. (2012). Kidagaa Kimemwozea. Nairobi. Target Publication Limited
Wamitila, W. (2002). Uhakiki wa Fasihi: Misingi na Vipengele Vyake. Nairobi: Phoenix Publishers.
Wanyonyi, W. (2009). ‘‘Matumizi ya Tasfida, Ishara na Balagha katika Riwaya ya Nyuso za Mwanamke’’Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Nairobi (Haijachapishwa).
Copyright (c) 2025 Rose Kawira, PhD, Faith Kathure Murugu

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.