Sababu za Kutokea kwa Ndoa za Mitala katika Riwaya Teule- Barua Ndefu Kama Hii (1980), Takadini (2004) na Paradiso (2014) katika Mpito wa Wakati

  • Agnes Kwamboka Omete Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Jesse Joseph Murithi, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Mitala, Talmudi, Mfumo huu
Sambaza Makala:

Ikisiri

Ndoa za mitala zimekuwepo katika jamii zetu kwa kipindi kirefu sana. Walio katika ndoa hizi huchochewa na sababu tofauti tofauti. Kwa kuwa suala hili limekita mizizi sawasawa katika jamii zetu, waandishi mbalimbali wa kazi za fasihi wameweza kuliangazia katika kazi zao kwa kipindi kirefu. Ni kutokana na hali hii, makala hii inaangazia kwa kina sababu za kutokea kwa ndoa hizi kwa mujibu wa riwaya tatu teule - Riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii iliyoandikwa na Mariama Bâ (1980), Takadini ya Ben Hanson (2004) na Paradiso ya John Habwe (2014). Riwaya hizi ziliteuliwa kimakusudi kwa kuwa japo zimeandikwa katika vipindi tofauti, zote zimeangazia vyema suala hili la ndoa za mitala. Hii inabainisha kuwa ndoa hizi zingali na umaarufu katika jamii zetu. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Uhalisia ya Villanueva (1997). Utafiti ulifanywa maktabani na mtandaoni. Data ya msingi ilipatikana kwa kuvitalii vitabu vilivyoteuliwa kisha kuipanga katika makundi na kuichanganua kwa kuzingatia malengo ya utafiti. Aidha, utafiti ulinufaishwa kwa kuzisoma na kuzihakiki kazi zinazohusiana na suala hili kwenye majarida, makala ya magazeti, tasnifu, vitabu na machapisho mengine. Matokeo yaliwasilishwa kupitia maelezo. Ingawa kuna mabadiliko makubwa katika mpito wa wakati, utafiti huu ulibaini kuwa sababu za kutokea kwa ndoa hizi hazijabadilika sana. Baadhi ya sababu hizi ni; utamaduni katika jamii, shinikizo la kulipiza kisasi, ubabedume, mafundisho ya kidini, ari ya kupata utajiri, viongozi kuwavutia wanawake, utasa au kukosa mtoto wa kiume, mabadiliko ya kimajukumu katika ndoa, wanandoa kutengana kutokana na ajira na hali ya wanandoa kutotosheka kimapenzi. Waandishi, watafiti na wadau wengine wa kazi za fasihi watafaidika na makala hii kwa kuwa yameviangazia kwa kina visababishi vya suala hili la mitala. Aidha, matokeo ya kazi hii yataweza kuwafaa wanaojihusisha na masuala ya kijamii kupata mwanga zaidi kuhusu mabadiliko katika suala la mitala miongoni mwa wanajamii kote ulimwenguni.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Al-Krenawi, A. (2001). Women from polygamous and monogamous marriages in an out-patient psychiatric clinic. Transcultural Psychiatry, 38(2), 187-199.

Al-Krenawi, A., & Graham, J. R. (1999). The story of Bedouin-Arab women in a polygamous marriage. Women’s Studies International Forum, 22(5), 497-509.

Bâ, M. (1980). Barua Ndefu Kama Hii. Mkuki wa Nyota Publishers. Dar es Salaam. Tanzania.

Elbedour, S., Onwuegbuzie, A. J., Caridine, C., & Abu- Saad, H. (2002). The effect of polygamous marital structure on behavioral, emotional, and academic adjustment in children: A comprehensive review of the literature. Clinical Child and Family Psychology Review, 5(4), 255-257.

Greer, G. (1970). The Female Eunuch. London: Grafton Books.

Hanson, B.J. (2004). Takadini. East African Educational Publishers. Nairobi, Kenya.

Kezilahabi, E. (1971), Rosa Mistika. Arusha. ELB

Lukacs, G. (1979). The Meaning of Contemporary Realism. London. Merlin.

Mageche, K.S. (2017). Nadharia ya Ufeminist katika Jamii. Tasnifu ya Uzamili, Dar es Salaam: St. Augustine University of Tanzania.

Sanja, W. L. (2012). Maudhui ya Ndoa na Dini Katika Riwaya za Kala Tufaha na Paradiso. Tasnifu ya Uzamili, Nairobi: Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Senkoro, F. E. M. K. (1987). Fashi na Jamii. Dar es Salaam: Press and Publishing Centre.

Strobel, M. (1979). Muslim women in Mombasa, 1890-1975. Yale University Press.

Wanjiku, K. na Akinyi, N. (1993). Celebrating Women’s Resistance. A case study of Women Groups Movement in Kenya. Nairobi: Africa Women Perspective.

Yule, G. (1996). The Study of Language. Cambridge University Press, Cambridge.

King James Bible (2008). Oxford University Press (Original work published 1769)

The Qu’ran. Translated by M.A.S. Abdel Haleem, Oxford UP, 200

Habwe, J. (2014). Pardiso. Nairobi. Jomo Kenyatta Foundation.

Tarehe ya Uchapishaji
9 October, 2025
Jinsi ya Kunukuu
Omete, A., & Murithi, J. (2025). Sababu za Kutokea kwa Ndoa za Mitala katika Riwaya Teule- Barua Ndefu Kama Hii (1980), Takadini (2004) na Paradiso (2014) katika Mpito wa Wakati. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 8(2), 384-396. https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3783