Msatakabala na Changamoto za Kiswahili Nchini Uganda

  • Florence Abuyeka Miima, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Vincent Ferrel Kawoya Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Msatakabala, Changamoto, Lugha, Kiswahili, Uganda
Sambaza Makala:

Ikisiri

Kiswahili ni lugha ya kimataifa na ni mojawapo ya lugha rasmi za Muungano wa Nchi za Afrika. Vilevile, katika nchi za Afrika Mashariki, Kiswahili kina hadhi ya aina ya kipekee kikilinganishwa na lugha zingine zenye asili ya Kiafrika. Nchini Kenya na Tanzania ni lugha ya taifa na rasmi. Kwa upande mwingine, nchini Uganda, Kiswahili kinatambulika kikatiba kama lugha ya pili rasmi. Hali kadhalika katika kanda ya maziwa makuu kinategemewa sana kama chombo muhimu cha kufanikisha harakati za kibiashara. Kutokana na ukweli huu kuhusu hadhi na umuhimu wa lugha ya Kiswahili, ingetarajiwa kuwa Kiswahili kingetumiwa kwa mawasiliano rasmi na katika ngazi mbalimbali za kimataifa. Hata hivyo, ni wazi kwamba kinakabiliwa na changamoto chungu nzima hasa zaidi nchini Uganda kiasi kwamba hatima yake haijulikani. Makala hii itaangazia hali ya lugha ya Kiswahili, changamoto zinazoikabili na hatima yake nchini Uganda. Itatoa mapendekezo kuhusu mikakati inayoweza kutumiwa ili kutamanisha wananchi wa Uganda kukienzi Kiswahili, kuinua hadhi yake na kukistawisha ipasavyo

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abdallah, K. (1977). The Liberation of Swahili from European Appropriation. Nairobi. East African Literature Bureau.

Chimera, R. (1998). Kiswahili: Past, Present and Future Horizons. Nairobi: N.U.P

Kihore, Y. M. (1983). ‘Nafasi ya Kiswahili Barani Afrika,’ katika MULIKA Nambari 15, uk. 32-39

Mazrui, A. A., & Mazrui, A. M. (1995). Swahili State and Society: The Political Economy of an African Language. Nairobi: E.AE.P.

Mbaabu, I. (1978). New Horizons in Kiswahili. Nairobi: KLB.

Mbaabu, I. (1995). “Linguistic and Cultural Dependency in Africa,” katika BARAGUMU, Jizuu la 2 Namb. 1-2 uk. 72-86.

Ministry of Education and Sports (2012). Primary Seven Curriculum. Kampala. National Curriculum Centre.

Msanjila, Y.P. (1997). “Towards A Policy on the Use of Kiswahili in Africa,” katika Kiswahili. Juzuu la 60. Uk. 61-67.

Msanjila, Y. P. (2003). “Kushuka kwa Hadhi ya Lugha za Jamii Nchini Tanzania,” in Nordic Journal of African Studies12 (3). 296–309

Msanjila, Y.P. (2009). “Haja ya Kuwa na Sera Tosherevu ya Lugha Tanzania: Uzoefu na Changamoto”, Katika Mulika.28

Whitely, W.H. (1969). Swahili: The Rise of the Swahili Language. Methuen & Co. Ltd., London.

Whitely, W. H. (1971). “Some Factors Influencing Language Policies in Estern Africa” in Rubin Joan (1971) Can Language be Planned? The University Press of Hawii.

Tarehe ya Uchapishaji
27 July, 2021
Jinsi ya Kunukuu
Miima, F., & Kawoya, V. (2021). Msatakabala na Changamoto za Kiswahili Nchini Uganda. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 3(1), 70-77. https://doi.org/10.37284/jammk.3.1.367