Uchanganuzi wa Sauti ya Usimuliaji na Mahusiano ya Wakati wa Usimulizi katika Nyimbo Teule za Bahati Bukuku

  • Asige Nelson Aboge Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Sauti ya Usimuliaji, Mahusiano, Usimulizi, Nyimbo Teule
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inalenga kubainisha jinsi sauti ya usimuliaji, kama kipengele muhimu cha kuhakiki simulizi, imejitokeza katika nyimbo teule zenye sifa za kisimulizi zilizowasilishwa na msanii Bahati Bukuku. Makala vilevile imechanganua mahusiano ya wakati wa usimulizi kwa kuhakiki vipengele vyake muhimu kama usimulizi baadaye, usimulizi kabla, usimulizi sawia na usimulizi zongomezi. Makala hii iliongozwa na lengo kuu la kudhihirisha jinsi vipengele vya sauti ya usimuliaji na mahusiano ya wakati wa usimulizi vinavyobainika katika nyimbo teule za Bahati Bukuku. Nyimbo zilizochanganuliwa ni: Lazima usamehe, Dunia haina huruma, Waraka, Tupatupa, Maamuzi, Ahabu, Unatisha. Vigezo vikuu vya uteuzi wa nyimbo hizi ni vipengele vya kihadithi ndani mwao. Nadharia iliyotumika ni ya Naratolojia inayojumuisha usimulizi katika tanzu za fasihi kama vile nyimbo, mashairi, maghani na kadhalika. Sauti ya usimulizi hujenga uhusiano na anayesimuliwa. Mtazamo wa masimulizi, mfuatano wa matukio pamoja na dhamira kuu huwasilishwa na msimulizi. Matukio katika simulizi hutendeka kiwakati. Simulizi hutambulishwa katika wakati fulani kuhusiana na kitendo cha usimuliaji: kabla ya kutendeka, wakati yanapotendeka, baada ya kutendeka na iwapo kuna uchangamano wa matukio kusimuliwa yakitendeka. Kwa mujibu wa matokeo, makala imebainisha kuwa mihimili ya sauti ya usimuliaji pamoja na mahusiano ya wakati wa usimuliaji ilijitokeza kwa namna mbalimbali katika nyimbo za msanii Bahati Bukuku kwa kutegemea miktadha mbalimbali. Makala ilihitimisha kuwa kigezo cha wakati ni nguzo muhimu katika uwasilishaji wa hadithi, na uelewa wa hadithi hutokana na matumizi sawa ya kigezo hiki, kwani matukio yanayosimuliwa hutendeka kiwakati.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Arege, T. (2012). Narration in Swahili Narrative Poetry: An analysis of Utenzi wa RASI ‘L GHULI. Tasnifu ya Uzamifu. Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa)

Barthes, R. (1975). Structural Analysis of Narrative. Criticism: The Major Statements.

Chatman, S. (1990). Coming to Terms: The Rhetoric of Narrative in Fiction and Film. Ithaca Cornel University Press.

Fludernik, M. (1993). Second person fiction: Narrative ‘you’ as adressee and/or protagonist. London: Routledge.

Genette, G. (1980). Narrative Discourse. New York: Cornell University Press.

Kieti, M. (1990). The Wisdom of Kamba Oral Literature. Nairobi: Phoenix Publishers.

Kimani, P. W. (2012). Arki Za Simulizi Bunilizi Katlka Utendi Wa Mikidadi Na Mayasa (Doctoral dissertation, University of Nairobi).

Lanser, S. (1981). The Narrative Act. Point of view in Prose Fiction. Princeton. UP

Mohammed, S.A. (1995). Kunga za Nathari ya Kiswahili. East African Educational Publishers, Nairobi.

Njogu, K. na Chimera, R. (1999). Ufundishaji wa Fasihi, Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Rimmon-Kenan, S. (2002) Narrative Fiction: Contemporary poetics. London: Routledge.

Propp, V. (1968). The Morphology of the Folk Tale. The American Folk Society and Indiana University Press. Texas.

Prince, G. (1973). A Grammar of Stories: An Introduction. The Hague-Paris. Walter de Gruyter.

Manfred, J. (2005). Narratology: A Guide to the Theory of Narrative. Cologne: English Department, University of Cologne.

Stanzel, F. (1984). A theory of Narrative. London: Cambridge University Press.

Wamitila, K.W. (2002). Uhakiki wa fasihi: Misingi na vipengele vyake. Nairobi Focus Publishers (K) LTD.

Wafula, R. M., & Wanjala, C. L. (2017). Narrative Techniques in Chinua Achebe’s Things Fall Apart. Journal of Social Sciences, 50(1-3), 62-69.

WICHLACZ, S. (2007). Issues of Narration: Voice-Over in Film. [Online] 27th May 2006.

Tarehe ya Uchapishaji
17 September, 2025
Jinsi ya Kunukuu
Aboge, A. (2025). Uchanganuzi wa Sauti ya Usimuliaji na Mahusiano ya Wakati wa Usimulizi katika Nyimbo Teule za Bahati Bukuku. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 8(2), 338-353. https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3656