Falsafa ya Umoja na Mshikamano katika Misemo ya Vyombo vya Usafiri katika Ziwa Tanganyika

  • Anna Ussiry Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
  • Mohamed Maguo Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
  • Salma Hamad Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Keywords: Falsafa, Umoja, Mshikamano, Vyombo vya Usafiri, Ziwa Tanganyika, Sosholojia
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya yanaangazia falsafa ya umoja na mshikamano katika misemo ya vyombo vya usafiri katika ziwa Tanganyika ikiwa ni moja kati ya vipengele vya falsafa ya Kiafrika. Lengo la makala haya ilikuwa ni kutaka kuona namna falsafa ya Kiafrika kupitia kipengele cha umoja na mshikamano inavyojitokeza na kuwasilishwa katika misemo hiyo. Uandishi wa makala uliongozwa na nadharia ya Sosholojia ya Fasihi ambapo suala la falsafa ni sehemu ya jamii na hivyo nadharia hii ni faafu. Data ya makala hii ilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na kuchambuliwa kwa kutumia mbinu ya kimaelezo. Makala imebainisha kwamba falsafa ya umoja na mshikamano inajitokeza katika misemo ya vyombo vya usafiri wa majini katika ziwa Tanganyika kupitia misemo ambapo ni umoja na mshikamano ni kupendana, umoja na mshikamano ni kuepuka chuki, umoja na mshikamano ni kuwajali wageni, umoja na mshikamano ni kusaidiana, umoja na mshikamano ni kubarikiwa, umoja na mshikamano ni kuelimishana na umoja na mshikamano katika kuonyana. Makala yanatoa mapendekezo kwamba utafiti kama huu ufanyike kwa kutazama falsafa ya misemo ya kwenye vyombo vya usafiri wa majini katika maziwa na mito mingine ya jamii mbalimbali ili kuweza kupata picha kamili ya falsafa ya umoja na mshikamano katika jamii

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Babbie, E. (1999). The Basics of Social Research. Belmont: Wadsworth Publishing Company.

Burke, K. (1941). The Philosophy of Literary Form: Studies in Symbolic Action. Baton Rouge, Louisiana: Louisiana State University Press.

Faustine, S. (2017). Falsafa ya Waafrika na ujenzi wa mtindo wa uhalisia ajabu katika riwaya ya Kiswahili (Tasnifu ya uzamivu, Chuo cha Dodoma (Tanzania).

Faustine, S. (2019). Ufrikanishaji katika riwaya ya Kiswahili. Mulika, 38, 55-73.

Fuluge, A., & Ngatungwa, F. J. (2021). Mdhihiriko wa falsafa ya Kiafrika katika vitendawili vya Kiswahili. Jarida la Chama cha Lugha na Fasihi ya Kiswahili Tanzania (CHALUFAKITA), 3(1), 40-68.

Kaponda, G. J. (2018). Ontolojia ya Kiafrika katika Mbolezi za Wanyasa (Tasnifu ya Umahiri katika fasihi ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dodoma (Tanzania)).

Kombo, D. K., & Tromp, D. L. (2006). Introduction to proposal and thesis writing. Nairobi: Paulines Publications.

Kothari, C. R. (2008). Research methodology: Methods and Techniques 2nd Edition. New Delhi: Wiley.

Mungah, C. I. (1999). Dhana ya Maisha katika novela mbili za Kezilahabi: Nagona na Mzingile (Tasnifu ya Umahiri katika Fasihi, Chuo Kikuu cha Nairobi (Kenya)).

Narizvi, S. (1982). The sociology of literature of politics. Australia: Edamund Burke.

Nassoro, H. (2016). Semi katika vyombo vya safari vya bahari kisiwani Pemba (Tasnifu ya shahada ya umahiri ya Kiswahili, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania).

Ngatungwa, F. J. (2020). Usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika semi: Mifano kutoka vitendawili vya Kiswahili (Tasnifu ya umahiri, Chuo Kikuu cha Dodoma (Tanzania)).

Nyerere, J. K. (1971). Elimu haina mwisho: Risala za Rais kwa Taifa alizozitoa katika mkesha wa mwaka 1970 na 1971. Dar es Salaam: Government printers.

Taine, H. (1873). The philosophy of art. New York: Holt & Williams.

Temples, P. (1959). Bantu philosophy. Paris: Presence of Africaine.

Yonazi, E. (2023). Mchango wa ujumi mweusi katika unusura wa nyimbo za Muziki wa dansi wa Tanzania: 1970-2000. East African Journal of Swahili Studies, 6(1).

Tarehe ya Uchapishaji
27 August, 2025
Jinsi ya Kunukuu
Ussiry, A., Maguo, M., & Hamad, S. (2025). Falsafa ya Umoja na Mshikamano katika Misemo ya Vyombo vya Usafiri katika Ziwa Tanganyika. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 8(2), 256-264. https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3559