Wakaa katika Hotuba Teule za Wanasiasa wa Kenya

  • Mukonambi Kekonen Stanley Chuo Kikuu Cha Kenyatta
  • Titus Kaui, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Wakaa, Hotuba, Siasa, Naratolojia, Anakroni, Analepsia, Prolepsia
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inachunguza ubainishaji wa wakaa katika hotuba teule za wanasiasa wa Kenya. Baadhi ya wanasiasa hutoa hotuba zinazovuta makini ya wasikilizaji na wafuasi wao kwa mitindo tofauti. Mojawapo wa mbinu hii ya kimtindo ni usimulizi. Wakaa ni mojawapo wa kipengele cha kimtindo katika usimulizi. Tafiti kadha zimefanywa kubainisha wakaa na matumizi yake katika tanzu za fasihi andishi na fasihi simulizi (taz. Kwaka; 2015; Khamis; 2015; Muiya; 2018; Kinga; 2020; Asige, 2021). Licha ya hayo, tafiti hizi za awali hazikushughulikia wakaa kwa kuhusisha moja kwa moja si hotuba tu bali hotuba za kisiasa. Ni katika msingi huu ndipo makala hii imechunguza jinsi wakaa inavyojitokeza katika hotuba teule za wanasiasa wa Kenya. Makala hii imeelekezwa na nadharia ya Naratolojia iliyoasisiwa na mwanafalsafa Plato katika chapisho lake The Republic na baadaye ikaendelezwa na mwanafunzi wake Aristotle (1920) aliyewasilisha mawazo yake katika chapisho la The Poetics na wananaratolojia wa hivi majuzi Gennette (1980), Prince (1982) na Rimmon-Kenan (2002). Uchunguzi huu ulizingatia mawazo yake Rimmon-Kenan. Naratolojia ni stadi ya aina ya utendaji kazi wa usimulizi. Huangalia undani wa vifaa vinavyoongoza maelezo ya simulizi na ufahamu wa utendaji kazi wake. Data iliyotumika katika makala hii imetokana na kusoma machapisho maktabani kama vile tasnifu, majarida na vitabu. Halikadhalika, utazamaji, usikilizaji na uchambuzi wa hotuba teule za wanasiasa Mhes. Kenyatta, Odinga na Ruto katika mtandao wa YouTube ulihusishwa. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kuwepo kwa vipengele vya wakaa vya mpangilio, muda na idadi au umara katika hotuba za wanasiasa. Isitoshe, imebainika kuwa kipengele hiki cha usimulizi kimetumiwa kuendeleza maudhui, fani za lugha na kuchimuza wahusika

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Arege, T. (2012). Narration in Swahili Narrative Poetry: An analysis of Utenzi wa RASI ‘L GHULI. Tasnifu ya Uzamifu. Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa).

Aristotle (1920). The Poetics. Oxford: Clarenton press.

Asige, N. (2021) Uchanganuzi wa Usimulizi kama Mtindo katika Nyimbo za Bahati Bukuku. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa).

Aswani, B., Mayaka, G. na Matinde, R. (2013). Misingi ya Nadharia na Mbinu za Utafiti. Mwanza: Serengeti Educational Publishers, Tanzania.

BAKIZA (2010). Kamusi ya Kiswahili Fasaha. Nairobi: Oxford University Press.

Bal, M. (2009) Naratolojia: Introduction to the Theory of Narrative. Toronto: University of Toronto Press.

Barry, P. (1995). Beginning Theory. New York: Manchester University Press.

Barthes, R. (1970) An Introduction to the Structural Analysis of Narration Discourse. Blackwell: Oxford University Press.

Chatman, S. (1978). Story and Discourse: Narrative Structure in Fiction and Film. Ithaca, New York: Comell University Press.

Genette, G. (1980). Narrative Discourse: New York: Cornel University Press.

Griffith, K. (2010). Writing Essays About Literature. Cengage. Wadsworth Publishers.

Habwe, H.J. (1999). Discourse Analysis of Swahili Political Speeches. PHD Thesis, University of Nairobi.

Keen, S. (2003). Narrative Form. London: Macmillan.

King’ei, K. na Kisovi, C. (2005). Msingi wa Fasihi Simulizi. Nairobi: Kenya Literature Bureau.

Kothari, R. (2004). Research Methodology: Methods and Techniques, (second edition). New Delhi: New Age International Publishers.

Kwaka, A. (2018) Uhakiki wa wakati na uwasilishaji usemi katika Utenzi wa Nabii Isa. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa).

Lwaitama, F. (1988) Hotuba za Kisiasa katika Kiswahili: Mtindo wa Maongezi ya Wanasiasa wa Tanzania (Nyerere na Mwinyi) Dar es Salaam; University of Dar es Salaam.

Lwaitama, A.F. (1995). A Critical Language Study of Tanzania Kiswahili Presidential Political Oratory. PhD Thesis. Birmingham Department of Modern Languages. Birmingham: Aston University.

Mdee, N.W. (2014). Kamusi ya Karne ya 21. Longhorn Publishers.

Msanjila, P. (1989) Sociolinguistic Rules of Formal Address in Kiswahili in D.P.B Massamba et al (ed) Jarida la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili vol. 56; Dar es Salaam; TUKI.

Muiya, P. (2022) Muundo wa Usimulizi wa Riwaya ya Kiswahili: Uchanganuzi wa Vuta N’Kuvute. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa).

Mulokozi, M.M. (1996). Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania.

Njogu, K. na Chimera, R. (1999). Ufundishaji wa Fasihi, Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Plato. (1930). The Republic, Books 1 to 5 trans. P. Shorey. Cambrigde: Havard University Press.

Ponera, A. S (2014). Utangulizi wa Nadharia ya Fasihi Linganishi. Dar esalam: Karljamer Print Technology.

Propp, V. (1968). The Morphology of the Folk Tale. The American Folk Society and Indiana University Press. Texas.

Raglan, L. (1956). The Hero: A Study in Tradition Myth and Drama. New York: Vintage Books.

Rimmon-Kenan, S. (1983). Narrative Fiction. London: Methuen& Co. Ltd.

Rimmon-Kenan, S. (2002). Narrative Fiction: Contemporary Poetics. London: Routledge.

Stanzel, F. (1984). A Theory of Narrative. London: Cambridge University Press.

TUKI, (2019). Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Nairobi: Oxford University Press.

Wamitila, K. (2002). Uhakiki wa Fasihi: Misingi na vipengele vyake. Nairobi, Focus Publishers Ltd.

Wamitila, K.W. (2003). Kamusi ya Fasihi Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Books Publishers

Wamitila, K.W. (2008). Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi. Nairobi: Vide-Muwa Publishers.

www.elections.nation.africa

www.iebc.co.ke/election/?election-results

www.youtube.com/watch/v=rTU3akPgErU

www.youtube.com/watch?app=desktop&v=284Ch224rxQ

www.youtube.com/watch?v=4UfEtaBiaA4

www.youtube.com/watch?v=dR440W_n4XQ

www.youtube.com/watch?v=InGgRa2ZrEo

www.youtube.com/watch?v=KvXdWzOZq0M

www.youtube.com/watch?v=ONd8ye-wfb4&t=479s

www.youtube.com/watch?v=QR6TvEiGmWg

Tarehe ya Uchapishaji
13 August, 2025
Jinsi ya Kunukuu
Stanley, M., & Kaui, T. (2025). Wakaa katika Hotuba Teule za Wanasiasa wa Kenya. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 8(2), 173-187. https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3485