Athari za Kimofosintaksia za Ngeli za Luganda katika Matumizi ya Kiswahili Sanifu Miongoni mwa Wanafunzi Shuleni, Uganda

  • Mulei Martin Chuo Kikuu cha Kabale School
  • Debora Nanyama, PhD Chuo Kikuu cha Maseno
  • Beverlyne Ambuyo, PhD Chuo Kikuu cha Maseno
Keywords: Mofosintaksia, Kanuni, Athari, Upatanishi wa Kisarufi, Lugha ya Kwanza, Umilikifu Na Unganifu, Uhamishaji, Uchopekaji, Ujumlishaji, Ubadilishanaji
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inaonesha athari za kimofosintaksia za ngeli za Luganda katika matumizi ya Kiswahili sanifu. Makala hii inatokana na kuwa, Luganda na Kiswahili huainisha ngeli kutumia mfumo mmoja na matumizi yake kuzingatia sheria za kuonyesha upatanishi wa kisarufi wa nomino na maneno mengine katika tungo kimofosintaksia. Uwiano na tofauti za kanuni za matumizi ya vipashio vya kimofosintaksia baina ya lugha asili na Kiswahili sanifu umeripotiwa kuingiliana na kuathiri matumizi ya Kiswahili sanifu. Utafiti huu ulifanywa baada ya kubaini kuwa maandishi na mazungumzo ya wanafunzi ambao lugha yao ya kwanza ni Luganda na ambao wanajifunza Kiswahili kama lugha ya pili ulikiuka utaratibu wa kisarufi wa matumizi ya Kiswahili sanifu. Data ilitokana na uchanganuzi wa maandishi na mazungumzo ya wanafunzi 117, usaili na mijadala ya walimu 30 kutoka shule za upili 15 teule, wilayani Kampala, Uganda. Utafiti huu uliongozwa na mihimili ya sarufi bia na upatanifu wa nadharia ya Umilikifu na unganifu (Chomsky, 1981) ambayo huonesha ubia wa lugha na hali ya vipashio fulani vya kisarufi kutawala vipashio vingine katika tungo. Matokeo ya tathmini ya kanuni za matumizi ya kipashio cha kimofosintaksia cha ngeli za Luganda katika matumizi ya Kiswahili sanifu yalidhihirisha athari za; uhamishaji wa maumbo, mofofonolojia, ubebaji wa viambishi vya ngeli tofauti, uchopekaji wa viambishi, ubadilishanaji wa viambishi ngeli, uchanganyaji wa maumbo na ujumlishaji wa viambishi vya msingi vya ngeli ya Luganda katika matumizi ya Kiswahili sanifu. Makala hii inatarajiwa kuwasaidia walimu na wanafunzi kutambua athari za lugha ya kwanza katika matumizi ya Kiswahili sanifu, kuweka mikakati ya kuondokana na athari hizi kujenga matumizi bora ya Kiswahili sanifu.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Adolph, E. (2014). Utohozi wa nomino za kiswahili na athari yake katika ngeli za kihaya.

Tasnifu ya uzamili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Ame, P. M. (2017). Athari za Kiisimu za Lahaja ya Kitumbatu katika Kiswahili Sanifu

Kinachotumika katika Shule za Tumbatu Zanzibar. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Barno, H. C. (2013). Muundo wa Kimofo-Sintaksia wa Kitenzi (Kt) cha Kinandi kwa Mtazamo wa Kiunzi cha Kanuni Finyu (Kkf). NordicJournalof African Studies, 22(4), 23-23.

Carolyne, O., Simala, I. K., & John, K. M. (2017). Athari za uhamishaji wa sarufi ya Kiluo kwenye upatanisho wa sarufi ya Kiswahili. Kiswahili, 76(1).

Chomsky, N. (1981). Lectures on government and binding: The Pisa Lictures. Dordrecht: Foris.

Habwe, J. & Karanja, P. (2004). Misingi ya sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Jarada Phoenix Publishers Ltd.

Kapinga, M. C. (1983). Sarufi Maumbo ya Kiswahili sanifu. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Dar es Salaam, TZ: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kihore, Y, M., Massamba, D. P. B. & Msanjila, Y. P. (2004). Sarufi maumbo ya Kiswahili Sanifu (Samakisa) Sekondari na Vyuo. Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kithuku, M. (2012). Mofosintaksia ya ngeli ya 9/10 (N/N). Nairobi, KE: Tasnifu ya Uzamili ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Massamba, D. P. B. (2004). Kamusi ya isimu na falsafa ya lugha. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mathooko, P.M. (2004). Towards integrative perspective of linguistic accommodation: A case study of Kikamba and Kitharaka. (Unpublished PhD thesis). NAironi, KE: Kenyatta University.

Mgullu, R. S. (1999). Mtalaa wa isimu: fonetiki, fonolojia na mofolojia ya Kiswahili. Nairobi, KE: Longhorn Publishers.

Mramba, P. T. (2015). Uchunguzi wa athari za Kirombo katika jifunzaji wa kiswahili Vipengele vya kifonolojia na kimofolojia. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mukuria, D. M. (1987). Mpangilio wa Ngeli: Ulinganishi wa Ngeli za Kiswahili sanifu na Kikikuyu cha Kiambu. Tasnifu ya Uzamili ya Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya.

Niyomugabo, C. (2016). Ufundishaji wa Kiswahili katika Shule za Rwanda: Historia, Tathmini ya Makosa, Matatizo na Mahitaji. Kiswahili, 79(1).

Ntawiyanga, S. (2015). Changamoto za kimofosintaksia miongoni mwa wanafunzi wa Kiswahili wa shule za upili wilayani Muhanga, Nchini Rwanda. Tasnifu ya uzamili ya Chuo Kikuu cha Kenyatta, Kenya.

Nyanda, J. (2015). Athari za Lugha ya Kinyamwezi Katika Kujifunza Lugha ya Kiswahili. Tasnifu ya uzamili ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Okumu, N. B. (2006) Tathmini ya mpango wa kisintaksia wa ngeli za nomino za Kiswahili: ufunzaji shule za Nairobi. Tasnifu ya uzamili ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Otiende, M. A. (2013). Athari za Kimofofonolojia za Kiolusuba katika Matumizi ya Kiswahili sanifu kama Lugha ya Pili. Chuo Kikuu Cha Nairobi.

Shabani, A. N. & R. (2015). Nadharia ya Utawala na Ufunganisho Inavyojihusisha na Aina za Vikundi Nomino katika Kiswahili, (2004), 1–8.

Tarehe ya Uchapishaji
20 May, 2021
Jinsi ya Kunukuu
Martin, M., Nanyama, D., & Ambuyo, B. (2021). Athari za Kimofosintaksia za Ngeli za Luganda katika Matumizi ya Kiswahili Sanifu Miongoni mwa Wanafunzi Shuleni, Uganda. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 3(1), 10-23. https://doi.org/10.37284/jammk.3.1.331