Tathmini Linganishi kati ya Mtalaa wa 8.4.4 na wa Umilisi wa 2.6.6.3 katika Ufundishaji wa Fonimu za Kiswahili katika Kiwango cha Chekechea

  • Nabangi Joan Wataka Masinde Muliro University of Science and Technology
  • Susan C Choge, PhD Masinde Muliro University of Science and Technology
  • Luganda Musavi Manasseh Masinde Muliro University of Science and Technology
Keywords: Mtalaa, Mtalaa wa Umilisi, Nadharia ya Utambuzi, Fonimu za Kiswahili, Chekechea

Abstract

Mtalaa ni mpangilio ambao huweka malengo katika ufunzaji wa wanafunzi. Unatumika kama mwongozo kwa walimu ambao huweka viwango vya matokeo ya mwanafunzi sawia na uwajibikaji wa mwalimu. Nchi ya Kenya imeshuhudia mabadiliko ya mitalaa mbalimbali tangu ilipojinyakulia uhuru. Nafasi ya mtalaa wa uhuru wa 7.4.2.3 ilichukuliwa na 8.4.4 mwaka wa 1985 ambao nafasi yake kwa sasa inachukuliwa na mtalaa mpya wa umilisi wa 2.6.6.3 ambao ulianzishwa mwaka wa 2017. Mitalaa hii imefafanua vipengele mbalimbali kwa kutumia mbinu mbalimbali za ufundishaji na ufunzaji. Kwa hivyo, lengo la nakala hii ni kutathmini kiulinganishi ufundishaji wa fonimu za Kiswahili katika kiwango cha chekechea katika mtalaa wa 8.4.4 unaoondolewa, na katika mtalaa mpya wa umilisi wa 2.6.6.3. Mtalaa wa 7.4.2.3 na wa 8.4.4 iliegemea sana uwezo wa mwalimu, yeye ndiye aliyechukua jukumu kubwa katika mchakato wa ufundishaji kuliko wanafunzi. Tofauti na mitalaa hiyo miwili, mtalaa wa 2.6.6.3 unampa mwanafunzi jukumu kubwa katika mchakato wa ujifunzaji kuliko mwalimu. Makala haya pia yamechunguza kiulinganishi ubora na udhaifu wa mbinu mbalimbali za ufundishaji wa fonimu za Kiswahili katika kiwango cha chekechea katika mitalaa ya 8.4.4 na mpya wa 2.6.6.3. Nadharia ya Piaget ya Utambuzi imeongoza makala haya. Makala haya yanaripoti baadhi ya matokeo ya utafiti uliofanywa kwa minajili ya shahada ya uzamili katika Elimu ya Kiswahili.

Downloads

Download data is not yet available.

References

Bruner, J. S. (1974). The Relevance of Education. New York: Norton.

Chiduo, F. K. na wengine. (2016). Kamusi Elezi ya Kiswahili. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Choge, S. (2009). Understanding Kiswahili Vowels. Journal of Pan African Studies, 2(8), 62-77.

Facun-Granadozo, R. (2014). Developing Mastery in Phonemic Awareness, Phonics, and Morphemic Awareness: A Multiple Case Study of Preservice Early Childhood Educators. PhD Thesis. East Tennessee State University.

Flinders, D. & Thornton, J. S. (2004). The Curriculum Studies Reader. Milton Park, Abingdon, Oxon (UK): Routledge Falmer.

KICD. (2017). Curriculum Design for PP1, PP2 & Grades One to Three. Nairobi: Kenya Institute of Curriculum Development.

KICD. (2019). Curriculum Design for Grade Four. Nairobi: Kenya Institute of Curriculum Development.

Kridel, C. (Ed.) (2010). Encyclopaedia of Curriculum Studies. A Thousand Oaks (CA): Sage Publishers.

Massamba, D. P. B., Kihore, Y. M, & Msanjila, Y. P. (2004).Fonolojia ya Kiswahili Sanifu. Dar es salaam: TUKI.

Mdee, J. S. na wengine (2019). Kamusi ya Karne ya 21. Nairobi: Longhorn Publishers PLC.

Mgullu, S. R. (2016). Mtalaa wa Isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Nairobi: Longhorn Publishers PLC.

Mwongozo wa KIE .(2002). Primary School Syllabus. Nairobi: Kenya Institute of Education

Okal, O. B. (2017). Uhakiki wa Fonimu na Miundo ya Silabi za Kiswahili: Kioo cha Lugha Juz 13.

Piaget, J. (1972). “Development and Learning.” In Lavatellic S. & Stendler F. (wah) (1972) Reading in Child Behaviour and Development. New York, Hacourt Brace.

Powers, E. J. (2008). ‘The Effectiveness of Phonemic Awareness Instruction on Struggling Readers’. Masters Thesis, State University of New York College at Brockport.

Wandera, S. (2018). Mitalaa ya Shahada ya Uzamili ya Kiswahili: Mtazamo wa Urie Bronfenbrenner. Coretrain Journal of Languages, Humanities, Social Sciences and Education, 1(1), 236-248.

Published
8 January, 2021
How to Cite
Wataka, N., Choge, S., & Manasseh, L. (2021). Tathmini Linganishi kati ya Mtalaa wa 8.4.4 na wa Umilisi wa 2.6.6.3 katika Ufundishaji wa Fonimu za Kiswahili katika Kiwango cha Chekechea. East African Journal of Swahili Studies, 3(1), 1-9. https://doi.org/10.37284/eajss.3.1.267