Ruwaza za Toni katika Vitenzi Visoukomo Changamani vya Kirombo

  • Peter T Mramba Chuo Kikuu cha Mt Augustino
Keywords: Sifa za Kimuundo, Kimofolojia, Kisintaksia, Wizani, Ushairi Huru
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya yanahusu uchanganuzi wa ruwaza za Toni katika Vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo. Lengo kuu la makala haya ni kuchunguza ruwaza ya ujitokezaji wa toni katika vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo na kanuni zinazotawala utokeaji huo. Aidha, malengo mahususi: kubainisha silabi inayohusishwa na Tonijuu Msingi (kuanzia sasa TJM) na mbili, kujadili ruwaza ya utokeaji wa toni katika vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo na kanuni zinazotawala hutokeaji huo. Data ya Makala haya imetokana na utafiti mpana uliofanywa juu ya toni katika wilaya ya Rombo (2019) ambao   uliongozwa na Nadharia ya Fonolojia Vipandesauti Huru kwa kutumia Mkabala wa Tonijuu Msingi kama ulivyoasisiwa na Goldsmith (1976) na kuboreshwa na wanazuoni mbalimbali katika taaluma ya fonolojia. Aidha, mbinu za ukusanyaji data zilizotumika ni pamoja na mahojiano na ushuhudiaji. Katika mahojiano vitenzi visoukomo changamani viliandaliwa kwa Kiswahili na watoataarifa walihitajika kuvitamka kwa Kirombo huku mtafiti akirekodi na kualamisha toni katika vitenzi hivyo. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kuna ruwaza mbalimbali za kitoni zinazoleteleza utokeaji wa kanuni za kitoni ambazo hutofautiana kutegemeana na idadi ya silabi na uwapo au kutowapo kwa yambwa. Aidha, vitenzi visoukomo changamani vya silabi moja hutawaliwa na kanuni ya uhusishaji wa toni chini na vitamkwa na sharti la ukubalifu, wakati vitenzi visoukomo changamani vya silabi mbili hadi ama tano au sita za shina hutawaliwa na kanuni ya udondoshaji wa TJM pamoja na kanuni nyingine kitoni kama vile: kanuni ya msambao wa tonijuu kuelekea kulia mwa shina, uhamaji wa TJM kutoka silabi ya kwanza kwenda katika silabi ya pili ya shina, unakiliji wa TJM katika silabi ya mwisho kasoro moja. Aidha, TJM hupachikwa katika mofimu ya yambwa kwa vitenzi visoukomo changamani vya silabi moja ya shina. Pia, matokeo yanaonesha kwamba kuna TJM mbili, yaani, ya kwanza ni ya yambwa na ya pili ikiwa ya shina, ambapo katika mchakato wa ukokotozi wa uibuzi wa toni, TJM ya shina hudondoshwa kwa kuwa yambwa ina nguvu zaidi.  Makala haya yamesaidia kujua namna toni zinavyojitokeza katika vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo kwa ujumla.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Batibo, H. M. (2012), Can tone shift be regarded as tone depression in Shisukuma? Katika M. Brenzinger and A.-M. Fehn (Wah.), Proceedings of the 6th World Congress of African Linguistics. kur. 201-206. Cologne: Ruediger Koeppe Verlag.

Goldsmith, J. (1976), “Autosegmental Phonology”. Tasnifu ya Uzamivu, MIT. (Imechapishwa).

Heine, B & Nurse, D. (2003), (Wah.). African Languages: An Introduction. Cambridge: Cambridge University Press.

Hyman, L. M. (2003), Basaá (A43). Katika. Nurse & Philippson, 257-282.

Hyman, L. M. (2008), Directional asymmetries in the morphology and phonology of words, with special reference to Bantu. Linguistics 46. 309-350.

Hyman, L. M. (2017), Katika. search of prosodic domains in Lusoga. Paper presented at the Workshop on the Effects of Constituency in on Sentence Phonology, University of Massachusetts, Amherst, Julai 30, 2016. Ms. University of California, Berkeley (submitted).

Marlo, M. R. & Odden, D. (2014), Bakweri tone melodies. Africana Linguistica 20.295-312.

Martinet, A. (2005), Economie des changements linguistiques. Paris: Maisonneuve et Larousse.

Massamba, D. P. B. (2011), Maendeleo katika Nadharia ya Fonolojia. Dar es Salaam: TATAKI.

Massamba, D. P. B. (2012), Misingi ya Fonolojia: Dar es Salaam. TATAKI.

Massamba, D. P. B. (2016), Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam: TATAKI.

McHugh, B. D. (2006), The phrasal cycle in Kivunjo Chaga tonology. Katika. Inkelas & Zec, kur. 217-242.

Meeussen, A. E. (1980), Bantu lexical reconstructions. Tervuren: Musée Royal de l’Afrique.

MLUTA. (2009), http/www.google.com/lugha/. LOT (10/4/2018).

Möller, K. (2014). Vom naturwissenschaftlichen Sachunterricht zum Fachunterricht–Der Übergang von der Grundschule in die weiterführende Schule. Zeitschrift für Didaktik der Naturwissenschaften, 20(1), 33-43.

Mramba, P. T. (2015), ‘Athari za Kirombo katika ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Pili: vipengele vya Kifonolojia na Kimofolojia’. Tasnifu ya Umahiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (Haijachapishwa).

Nash, J. A. (1992), Underlying low tones in Ruwund. Studies in African Linguistics 23.223-278.

Nelson, C. (2013), ‘Toni katika Vitenzi vya Kimochi’. Tasnifu ya Umahiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (Haijachapishwa).

Nurse, D & Phillipson, G. (1977), ‘‘Tones in Old Moshi (Chaga)’’, katika Studies in African Linguistics 8, kur. 49-80.

Nurse, D. & Philippson, G. (Wah.) (2003), The Bantu languages. London: Routledge.

Odden, D. (2005), Introducing Phonology. Cambridge: Cambridge University Press.

Polomé, S. A. (1971), ‘Phonological Survey of the Chaga Dialect of Tanzania’. Tasnifu ya Umahiri, Austin Texas. (Imechapishwa).

Raum, J. (1964), Versuch einer Grammatik der Dschaggasprache (Moschi-Dialekt). U.S.A: The Gregg Press Incorporated.

Snider, K. (1999), On establishing underlying tonal contrast. Language Documentation and Conservation 8, kur. 669–699.

Stevick, E. W. (1969), Tone in Bantu. International Journal of American Linguistics 35.330-341.

Van Spaandock, M. (1971), L’Analyse Morphotonologique dans les Langues Bantoues. Paris: SELAF.

Tarehe ya Uchapishaji
30 November, 2020
Jinsi ya Kunukuu
Mramba, P. (2020). Ruwaza za Toni katika Vitenzi Visoukomo Changamani vya Kirombo. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 2(2), 168-196. https://doi.org/10.37284/eajss.2.2.242