Sifa za Kimuundo Katika Diwani Huru ya Rangi ya Anga

  • Eunice Wavinya Nzioki Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Geoffrey Kitula King'ei, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Sifa za Kimuundo, Kimofolojia, Kisintaksia, Wizani, Ushairi Huru
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inalenga kuchambua na kutathmini sifa za kimuundo katika diwani huru ya Rangi ya Anga. Sifa za kimuundo ni muhimu katika kuudhibiti usomaji wa mashairi teule na kumwelekeza msomaji katika kuuelewa ushairi. Ijapokuwa tafiti nyingi zimefanywa kuhusu muundo katika mashairi, pana haja ya kuchambua sifa za kimuundo katika ushairi huru hasa diwani huru ya Rangi ya Anga. Utafiti huu ulitumia nadharia changamano: nadharia ya uhakiki ya umuundo na nadharia ya uhakiki wa kimtindo. Nadharia ya uhakiki ya umuundo iliasisiwa na Ferdinand De Saussure karne ya ishirini. Mawazo yake yaliendelezwa na Culler (1975) aliyeangazia umuundo katika ushairi. Alisisitiza kwamba ushairi ni ishara zinazojisimamia bila kudhibitiwa na mtunzi na ufasiri wa maana unatokana na namna vipengee vya kimuundo huchagizana kimaana. Kutokana na nadharia hii kutokuwa na urejelezi wa nje, nadharia ya uhakiki wa kimtindo ilitumika kufidia udhaifu huu. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhakiki wa kimtindo iliyoasisiwa na Coombes (1953) na kuendelezwa na Leech (1969). Mihimili mitatu ilitumika kuuongoza utafiti. Mathalan, viwango vya kimofolojia na kisintaksia ni msingi mkuu wa lugha unaodhibiti matumizi ya lugha, matumizi ya maumbo ya picha huonyesha umilisi wa mtunzi katika kuelezea hisia zake na vipashio mbalimbali vya muundo huingiliana na kujengana. Utafiti huu ulitumia sampuli ya kimaksudi kuteua diwani huru ya Rangi ya Anga (2014) kutokana na matumizi ya miundo tengemano na wepesi wa mawazo ya mtunzi. Uhakiki wa sifa za kimuundo ulizingatia sampuli ya kimaksudi ya mashairi teule, tasnifu, majarida na tahakiki. Data ya pili ilijumuisha mahojiano na mtunzi Kithaka wa Mberia. Matokeo ya data yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo. Yalionyesha kuwa sifa za kimuundo ni za kimsingi katika utunzi wa mashairi teule, ujenzi wa wizani na kudhibiti usomaji. Utafiti huu unapendekeza wasomaji wa ushairi huru wazingatie sifa za kimuundo ili kuufasiri ujumbe ipasavyo.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abedi, A. (1954). Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri. Nairobi: Kenya Literature Bureau.

Coombes, H. (1953). Literature and Criticism. Newyork: Chatto and Windows.

Crystal, D. & Davy, D. (1969). Investigating English Style. London: Longman Group Limited.

Culler, J. (1975). Structuralist Poetics. Structuralism, Linguistics & the Study of Literature. London: Routledge.

Hoopes, J. (1991). Peine on Signs: Writings on Semiotic by Charles Sanders Peine. Chapel Hill London: The University of North Carolina Press.

Indede, F. (2008). Mabadiliko katika Umbo la Ushairi na Athari zake katika Ushairi wa Kiswahili: SWAHILI FORUM 15:73-94.

Kezilahabi, E. (2008). Dhifa. Nairobi: Vide-Muwa Publishers Limited.

King’ei, K. & Kisovi, C. (2005). Msingi wa Fasihi Simulizi. Nairobi: Kenya Literature Bureau.

Leech, G. & Short, M. (1981). Style in Fiction: A Linguistic Introduction to English Fictional Prose 2nd Edition. Harlow: Longman Group Ltd. ; Essays and Reviews on 19th & 20th Century Literature. London: Routledge & Kegan Paul.

Leech, G. (1969). A Linguistic Guide to English Poetry. London & New York: Longman.

Lutomia, D. (2017). Mwanga wa Ushairi kwa Shule za Upili. Kakamega: Double Shasa Limited.

Mazrui, A. (1988). Chembe Cha Moyo. Nairobi: Heinemann Kenya Ltd.

Mberia, K. (2007). Msimu wa Tisa. Nairobi: Marimba Publications Ltd.

Mberia, K. (2014). Rangi ya Anga. Nairobi: Marimba Publications Ltd.

Mulokozi, M. (1989). Mgawanyo wa Tanzu na Vipera vya Fasihi Simulizi. Dar es Salaam: TUKI

Mwai, W. (1988). New Trends in Ushairi, Tasnifu ya M.A., Chuo Kikuu cha Nairobi.

Ntarangwi, M. (2003). Gender, Performance & Identity. NewYork: Africa World Press.

Onyancha, W. (2016). Changamoto za Mikondo Mipya ya Utunzi wa Mashairi ya Kiswahili, Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Pierce, C. & Welby, V. (1977). Semiotic and Significs. Canada: Indiana University Press.

Saussure, F. (1966). Course in General Linguistics. Newyork: Mc Graw-Hill.

Simpson, P. (2004). Stylistics. London & NewYork: Routledge.

Wamitila, K. W. (2008). Kanzi ya Fasihi. Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi. Nairobi: Vide-Muwa Publishers Limited.

Wordsworth, W. (1797). Lyrical Ballads. London: Methuen & Company Ltd

Tarehe ya Uchapishaji
15 November, 2020
Jinsi ya Kunukuu
Nzioki, E., & King’ei, G. (2020). Sifa za Kimuundo Katika Diwani Huru ya Rangi ya Anga. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 2(2), 153-167. https://doi.org/10.37284/eajss.2.2.237