Aina ya Nyenzo Katika Ufundishaji wa Fasihi Simulizi ya Kiswahili Katika Shule za Sekondari Nchini Kenya

  • Bakari Osundwa Kassim Masinde Muliro University of Science and Technology
  • John Kirimi M'raiji, PhD Masinde Muliro University of Science and Technology
  • Luganda Manasseh Masinde Muliro University of Science and Technology
Keywords: Nyenzo, Fasihi Simulizi, Ufundishaji, Kufundishia, Shule za Sekondari

Abstract

Madhumuni ya makala haya yalikuwa kubaini aina ya nyenzo katika ufundishaji wa Fasihi Simulizi ya Kiswahili katika Shule za Sekondari katika Kaunti ya Kakamega nchini Kenya kwa kuangazia madarasa ya mwanzo. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Maendeleo ya Kiutambuzi ya Jean Piaget (1896-1980) iliyoasisiwa mwaka 1954 inayosisitiza umuhimu wa kutangamana na matini husika kwa lengo la kuelewa katika hatua za mwanzo za funzo. Utafiti huu ulitumia muundo wa usoroveya elezi. Idadi lengwa ya utafiti huu ni walimu wa somo la Kiswahili pamoja na wanafunzi wa madarasa ya mwanzo katika shule za sekondari katika Kaunti ndogo ya kati ya Kakamega. Mtafiti alitumia mbinu za usampulishaji za kinasibu na kimakusudi kuteua sampuli ya kutumiwa ambayo ilikuwa theluthi moja ya idadi lengwa. Walimu ishirini na tano (25) ambao ni theluthi moja ya walimu wote wanaofundisha Kiswahili katika madarasa ya mwanzo katika shule za sekondari Kaunti ndogo ya kati ya Kakamega na wanafunzi mia mbili hamsini (250) walishirikishwa na data kukusanywa kwa kutumia miongozo ya uchunzaji, hojaji, mahojiano na uchanganuzi wa nyaraka. Data ziliwasilishwa kwa kutumia maelezo, majedwali, vielelezo na viwango vya kiasilimia. Matokeo ya utafiti huu yalikuwa kwamba, walimu wanatumia aina tatu za nyenzo katika ufundishaji wa Fasihi Simulizi ya Kiswahili lakini hawatilii mkazo nyenzo zinazotokana na hali na mazingira mbalimbali ya mfumo wa kijamii katika kufundisha Fasihi Simulizi ya Kiswahili licha ya kuwepo. Utafiti huu utakuwa muhimu kwa sababu mbali na kuwapa walimu uelewa mpana wa aina ya nyenzo katika ufundishaji wa Fasihi Simulizi ya Kiswahili, utasaidia katika kutambua hali na mazingira inayopatikana kama nyenzo katika ufundishaji na hivyo kuimarisha juhudi za wadau katika sekta ya elimu katika kuboresha matumizi yake. Utafiti ulipendekeza serikali kutenga sehemu maalumu katika Kaunti ili kuwapa walimu nafasi ya kutangamana na aina tofauti ya nyenzo zinazotokana na mifumo ya kijamii kwa kufundisha Fasihi Simulizi ya Kiswahili kwa kuimarisha na kuhifadhi mazingira ya kijamii kwa lengo la kutumika kama nyenzo.

Downloads

Download data is not yet available.

References

Aras G. (2012). Teaching writing through non library formats in Departments of English and literature. Fronters of language & Teaching, 132-138

Bennaars, G. A, Otiende, J. E. & Boisvert, R. (1994). Theory and Practice of Education. Nairobi: East African.

Chesaina, C. (2007). The Role and significance of Oral Literature in Social and Psychological Development of Children. Nairobi: Nairobi University Press.

Clark, L. H., & Starr, S. L. (1986). Secondary and Middle School Teaching Methods. New York: Macmillan.

Creswell, J. W. (2006). Research Design: Qualitative, Quantitative and Mixed Research Approaches. Thousand Oaks, CA: Sage.

Cross, G. P. (1974). The Psychology of Learning. Paris: Pergamon Press.

Donhardt, G. L. (1984). Microcomputers in education: Elements of a computer-based curriculum. Educational Technology, 24(4), 30-32.

Dorr, A. (1984). Television and Children. Newbury Park: Calif Educational Publishers.

Farrant, J. S. (1980). Principals and Practice of Education. Essex England: Longman.

Gagne (2006). The Condition of Learning. New York: Holt Rinehart and Winston.

Gathumbi, A. W., & Ssebbunga, C. M. (2005). Principles and Techniques in language Teaching; A Text for Teacher Educators. Teachers and pre-service Teachers, Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Henson, K. (1987). Teaching Secondary and Middle Schools. New York: Longman

KIE (2002). Secondary School Syllabus, Vol. 1. Nairobi: K.I.E.

KIE (2006). Secondary School Syllabus, Vol. I. Nairobi: K.I.E.

Kothari, C. (2012). Quantitative Techniques. (Toleo 3). New Delhi. Vicas publishing House Limited.

Kothari, C. R. (2003). Research methodology: Methods and techniques. New Delhi: Vishwa

Luvisia, J. C. (2003). A study of availability and use of instructional resources in teaching Kiswahili grammar in selected secondary schools of Bungoma District, Kenya. Tasnifu ya Uzamili ya Chuo Kikuu cha Moi.

Macharia, S. N., & Wario, L. H. (1989). Teaching Practices in Primary Schools. London: Macmillan.

Mugenda, O. M. & Mugenda, A. G. (2003). Research Methods Quantitative and Qualitative Approaches. Nairobi: Acts Press.

Mugenda, O. M., & Mugenda, A. G. (2006). Qualitative and Quantitative Approaches. Nairobi: Acts press.

Musau, P., & Chacha, L, (2001). Mbinu za Kufundisha Kiswahili. Nairobi: Kenya Literature Bureau.

Mwakyembe, G. R. (1982). Misingi ya Ualimu. Dar es Salaam: General Publishers Ltd.

Ogulla, P. A. (2002). Research Methods. Nairobi: Catholic University of Eastern Africa.

Okwalo, P. O. (2012). Matumizi ya Nyenzo katika ufundishaji wa Fasihi Simulizi ya Kiswahili katika shule za sekondari Wilayani Mumias na Matungu. Tasnifu ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Masinde Muliro.

Omstein, C. A. (1990). Strategies for Teaching. New York: Harper Collins.

Pappert, S. (1987). Computer Criticism Vs Technocentric Thinking.

Peil, M. (2002). Social Science Research Methods. A Handbook for Africa. Nairobi: East African Educational Publishers.

Postman, N. (1979). Teaching as A Counselling Activity. New York: Delacorte. Prakashan.

Quist, D. (2000). Primary Teaching methods. Oxford UK: Macmillan.

Robinson, A. (1980), Principals and Practices of Teaching. London: George Allenand Unwin.

Shitohi, E. (1992)."An Investigation into The Use of the Radio Component in Training Inservice Primary Teachers": A project Report Submitted in Partial Fulfilment of the Requirements for the Degree of M.Ed Kenyatta University (unpublished).

Sifuna, D. N. (1996). Short Essays on Education in Kenya. Nairobi: Kenya Literature Bureau.

Singleton, R. A. (1993). Approaches to Social Research. New York: O. U. P.

Published
24 October, 2020
How to Cite
Kassim, B., M’raiji, J., & Manasseh, L. (2020). Aina ya Nyenzo Katika Ufundishaji wa Fasihi Simulizi ya Kiswahili Katika Shule za Sekondari Nchini Kenya. East African Journal of Swahili Studies, 2(2), 143-152. https://doi.org/10.37284/eajss.2.2.227