Mifumo ya Ujinaishaji ya Wameru: Uchunguzi Tarafani Mwimbi katika Jimbo la Tharaka Nithi, Kenya

  • David Micheni Mutegi, PhD Chuo Kikuu cha Egerton
Keywords: Athari, Mbari, Mifumo, Ujinaishaji, Sifabia
Sambaza Makala:

Ikisiri

Lengo la utafiti lilikuwa kubainisha mifumo ya Wameru ya ujinaishaji. Uchunguzi ulifanywa Skatika tarafa ya Mwimbi katika jimbo la Tharaka Nithi nchini Kenya kwa ambavyo hakuna uchunguzi wowote umefanywa kufikia sasa kubainisha namna Wameru wanavyojinaisha watoto. Swali la utafiti katika uchunguzi huu lilikuwa: Wameru huzingatia mifumo gani katika ujinaishaji wa watoto? Majibu kwa swali hili yalibainisha namna Wameru walivyochagua majina waliyowapa watoto. Idadi ya wahojiwa sabini waliteuliwa wakijumlisha vijana hamsini na wazee ishirini kwa kuwa makundi hayo na idadi hiyo ingekuwa kiwakilisho tosha cha wakaazi wa Mwimbi kwa kujibu swali la utafiti na kutosheleza madhumuni yake pia. Mbinu ya mahojiano yenye muundo ilitumiwa ambapo kila mhojiwa aliulizwa swali lile lile lililoulizwa mwingine. Mbinu hii ilifaa utafiti huu kwa vile kila mhojiwa alikuwa na uhuru wa kujieleza kwa hivyo habari nzito na nyepesi ziliweza kupatikana kwa ajili ya kuchuzwa na mtafiti. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Hakiki Usemi na Matini na hasa zaidi ulizingatia Mtazamo Usemi Kihistoria wa Ruth Wodak. Ilibainika kuwa Wameru huwa na mifumo minne mahsusi ya ujinaishaji mathalani: sifabia za mtoto na za ntaguye, kutumia majina ya Ukoo, majina ya Rika na majina ya Nyoni. Mtafiti alipendekeza wazazi wawashirikishe vijana katika uteuzi wa majina ya watoto ili kuepuka mwelekeo hasi kuhusu majina yao wanapokua. Mapitio ya maandishi yalidhihirisha kuwa uchunguzi wa aina hii haujafanywa katika eneo hili kwa hivyo matokeo yalikuwa ni kichocheo kwa watafiti wengine wa kiisimu ambao wangependa kutafiti kuhusu mifumo ya ujinaishaji ya makabila mengine

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abate Fr, Ed. (1994). Proper Names Master Index, A comprehensive index of proper names Detroit.

Abagi, M. (1995). An Anthropology of Names and Naming. Cabridge.Cabridge University press.

Aswani, Mayaka na Riro (2014). Misingi ya Nadharia na Mbinu za Utafiti. Serengeti Publishers. Mwanza.

Barnes R. H, (1980). ‘Hidasta personal names’: An Interpretation Plains Anthropologistics Journal of anthropological Research /25 90311-31281.

Berly, A. (2013).‘African Naming Practices’: Journal of pan Africa studies Vol. 7 no.8/7 South Carolina.

Beidelman, B. (1974). An Alphabetical Guide to the Language of Name Studies Lanham and London, The Scarecrow Press.

Buren, D .V (1977), English personal names, Retrived from https // books. Google.com 15th April, 2017.

Edward, S. (1996), Journal of Languages and Culture. Personal Name and history. Retrived from http://www.journals. Org /.../... on 10th March, 2017.

Garry,T.(2000). Ethinic Naming Customs. Retrieved from http://www.scn.sap.babynames.co on 2nd February, 2017.

Greg, C. (2014), Retrived from https://www. baby centre. Com- names…, Social science space. com, Sage publications on 15th January, 2017.

Greenberg, S. (1980) African Names: Names from the Africa Continent for Children and Adults. Newyork.

Good, C.U. (1963), Introduction to Education Research, New York, Appleton Century Croft

Idowu, E.B. (1991). Introduction to tradition Religion SCM press, London.

Laura, A. ( 2009), The Oxford Hand book of Names and Naming. Oxford University press United Kingdom.

Mugambi, J.N (1989), African Heritage and Contemporary Christianity. Longman, Nairobi, Kenya.

Mbiti, J.S (1992) 2nd Ed. African Religious and Philosophy Heinemmann, London.

Mugenda, O and Mugenda, A. (1999), Research Methods Qualitative and Quantitative

Approaches, Nairobi, African Center for Technology Studies (Acts) Press

Onyango, G.A. (2001), Competencies Needed by Secondary School Head Teachers and

Implications for Pre-Service and In-Service Education, A Case Study of Nairobi and Kakamega District (Kenya), Unpublished PhD. Thesis, Kenyatta University

Orodho, A. J. (2003). Elements of Education and Social Science Research Methods. Nairobi: Mazola Publishers.

Pamela, R. And Linda, R (2004), Cool names for Babies: Retrived from htttp: //www.amazon. com /... Names... on 7th April, 2017.

Webber, M. (1987). ‘Ethics as Personal Names’Greek Personal Names.Their values as Evidence. Oxford University Press.

Wierzbicker, A. (1992). Semantics Culture And Cognition Universal Human Concepts In

Culture Specific Configurations. Oxford university press. New york.

The New Constitution of Kenya (2010), Government printer, Nairobi, Kenya.

Tarehe ya Uchapishaji
12 August, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Mutegi, D. (2024). Mifumo ya Ujinaishaji ya Wameru: Uchunguzi Tarafani Mwimbi katika Jimbo la Tharaka Nithi, Kenya. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 359-370. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.2100