Usawiri Chanya wa Hadhi ya Mwanamke katika Methali za Igikuria

  • Maroa Dunstan Sospeter Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Catherine Ndungo, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Methali, Ufeministi, Utamaduni, Usawiri
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii imechunguza usawiri chanya wa hadhi ya mwanamke katika methali za Igikuria. Swala la usawiri wa mwanamke limeshughulikiwa na watafiti wa awali huku tafiti zao zikiibua usawiri hasi wa mwanamke. Tafiti hizi za awali kama za Matteru (1993) na Ndungo (1998) zilifanywa kuhusu vipera vya fasihi simulizi kama vile; nyimbo na methali zilidhihirisha namna tofauti mwanamke anavyodunishwa katika jamii za Kiafrika. Udunishwaji huu unatokana mifumo tawala inayompendelea mwanamume. Mifumo hii imejificha katika mila na desturi potovu za jamii mbalimbali. Aidha, ingawa jamii huweza kumdunisha mwanajamii yeyote yule kwa kutegemea matendo yake, kuna miktadha mbalimbali ambayo humfanya mtu kupata sifa nzuri kulingana na matendo yake mazuri. Mwanamke anapochangia katika shughuli mbalimbali za jamii hupewa sifa si haba. Kutokana na haya, panaibuka haja ya kuchunguza usawiri chanya wa mwanamke katika methali za Igikuria kwa kudhihirisha anavyotukuzwa katika jamii, miktadha inayompelekea kusifiwa na mchango anaotoa katika kuendeleza asasi mbalimbali za kiuchumi, kisiasa, na kijamii. Makala hii imeongozwa na nadharia ya Ufeministi ambayo iliwekewa misingi na Wollstonecraft (1992), Woolf (1929) na Beauvoir (1994). Mihimili ya Ufeministi iliyotuongoza ni usawazishaji wanadamu kwa upande wa utamaduni na uana, utumiaji wa fasihi kama jukwaa la kueleza kwa uyakinifu hali inayomkumba mwanamke ili iweze kueleweka na watu wengi na kuhamasisha watumiaji wa sanaa wawe na wahusika wa kike ambao ni vielelezo wenye uwezo na wanaoweza kuigwa. Data iliyotumika katika Makala hii ilitolewa maktabani na nyanjani. Maktabani, tasnifu, makala na vitabu vinavyohusiana na mada vilisomwa kwa kina. Nyanjani, data ya methali za kumtukuza mwanamke ilikusanywa kwa njia ya hojaji. Uwasilishaji wa matokeo umefanyika kwa njia ya maelezo na michoro faafu. Matokeo yameonyesha kuwa katika methali za Igikuria, mwanamke amesawiriwa kama mfadhili katika ukoo anaotoka, mshauri wa jamii, kiongozi katika shughuli muhimu za jamii (sherehe), mtetezi wa jamii, mlezi, mjenzi wa familia na msingi thabiti katika jamii. Pia mwanamke amejitokeza kuwa chemchemi katika maisha ya Wakuria. Hidaya na uwezo wa kipekee aliotunukiwa mwanamke na Jalali katika kuendeleza jamii kupitia kwa njia ya uzazi, unamfanya kusifiwa kiasi kuwa mji usio na mwanamke hulinganishwa na chaka lisiloingilika. Aidha, miktadha ya kijamii ambayo inapelekea mwanamke kutukuzwa ni ya sherehe za kitamaduni, shughuli za kilimo na uzalishaji mali, shughuli za uzazi na malezi

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Beauvoir, S. (1994). The Second Sex. London: Jonathan cape.

Bennaars, G. A. (1995). Gender Education and the Pedagogy of Difference: The African predicament. In Basic Education Forum (Vol. 6, Uk. 23-34).

Birke, L. (1986). Women Feminist and Biology. The Feminist Challenge. Wheatsheal: Collins.

Kirumbi, P. S. (1975). Misingi ya Fasihi Simulizi. Nairobi: Shungwaya Publishers L.T.D.

Kolodny, A. (1986). Dancing through the minefield: some observations on the theory, practice and politics of a feminist literary criticism. Feminist studies, 6(1), Uk. 1-25.

Lovenduski., & Randall, V., &, J. (2004). Gender in contemporary British politics. The British Journal of Politics and International Relations, 6(1), 1-2.

Maitaria, J. N. (1991). Methali za Kiswahili kama chombo cha Mawasiliano; Mtazamo Wa Kiismu-Jamii. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu Cha Kenyatta. Kenyatta University Institutional Repository. (Haijachapishwa).

Matteru, M. L. B. (1993). Fasihi Simulizi na Uandishi wa Kiswahili. Dar es Salaam: TUKI.

Mitchell, J. na Oakley, A. (1986). What is Feminism. Oxford: Basil Blackwell.

Msokile, M. (1992). Kunga za Fasihi na Lugha. Kibaha: Education Publishers and distributors ltd.

Mulokozi, M. M. (1996). Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam: KAUTTU.

Ndungo, C (1998). Images of Women in African Oral Literature; Acase of Gikuyu and Swahili Proverbs. Unpublished PHD Thesis, Kenyatta University. Kenyatta University Institutional Repository.

Njogu, K. na Wafula, R. M. (2007). Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Nkwera, F. V. (1979). Sarufi na Fasihi, Sekondari na Vyuo (Vol. 4). Dar es Salaam: Tanzania Publishing House.

Ramazanoglu, C. (1989). Feminism and The Contradictions of Oppression. London: Routledge.

Sengo, T. S. Y. (1985). The Indian Ocean Complex and the Kiswahili Folklore: The Case of the Zanzibarian Tale-Performance. Unpublished PhD Thesis, University of Khartoum. University of Khartoom Institutional Repository.

Senkoro, F. E. M. K. (1987). Fasihi na jamii. Press and Publicity Centre.

Senkoro, F. E. M. K. (2010). Kiswahili Literary Portrayal of Gender and Migration in Africa: An African Perspective? In Unpublished paper presented at Codesria Gender Symposium, Cairo, Egypt, November (Uk. 24-26).

Svensson, A. (1994). Ibiirengio. Nairobi: Phoenix Publishing House.

Wamitila, K. W. (2002). Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Phoenix Publishers L.T.D.

Wamitila, K. W. (2008). Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi. Nairobi: Focus Books.

Wollstonecraft, M. (1992). A Vindication of the Rights of Woman. 1792. The Works of Mary Wollstonecraft, 5, 217.

Woolf, V. (2021). A Room of One’s Own. Virginia: Global Grey.

Woolf, V. (1929). Feminism, Women, literature, education. London: Hogarth Press.

Tarehe ya Uchapishaji
15 July, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Sospeter, M., & Ndungo, C. (2024). Usawiri Chanya wa Hadhi ya Mwanamke katika Methali za Igikuria. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 332-342. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.2048