Upembezwaji wa Mwanamke kama Kihunzi cha Ufanisi wa Ujenzi wa Ujitambuzinafsia Katika Baadhi ya Bunilizi za Clara Momanyi

  • Kawira Kamwara, PhD Chuo Kikuu cha Nairobi
Keywords: Ujitambuzinafsia, Upembezwaji, Ubaada Wa Ufeministi Wa Kiafrika, Bunilizi
Sambaza Makala:

Ikisiri

Jamii nyingi za Kiafrika ni za kuumeni na humpembeza mwanamke kwa kumweka katika ngazi za chini akilinganishwa na mwanamume. Upembezwaji wa mwanamke katika tungo za kifasihi na katika maendeleo ya jamii ni matokeo ya mwingiliano wa fahamu tambuzi na fahamu bwete za mtunzi hasa kwa mujibu wa utamaduni wa jamii lengwa. Mwingiliano huu wa ufahamu tambuzi na ufahamu bwete unaekezwa kwa makusudi katika utunzi wa tungo mahususi kama ilivyo kwenye tungo za Momanyi ‘Ngome ya Nafsi’ katika Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine (2004), Tumaini (2006) na Nakuruto (2010). Nadharia tuliyotumia ni ya  Ubaada wa Ufeministi wa Kiafrika iliyoasisiwa na Steady (1981). Mwanaufeministi huyu alisema kuwa Ubaada wa Ufeministi wa Kiafrika huweka masuala pamoja ya kijinsia, ubaguzi, mielekeo ya kiutamaduni na tabaka ili kumwangalia mwanamke kama kiumbe mtegamewa bali sio mtegemezi. Data ya usomi huu ilitokana na usomaji wa bunilizi hizi maktabani. Tuliweza vilevile kutumia mitandao kurutubisha utafiti wetu. Hivyo, ni kwa jinsi gani ambavyo utamaduni unatinga ufanisi wa mwanamke kisanii katika jamii? Ni mikakati ipi ambayo jamii imeweka kupigania ufanisi wa mwanamke? Mwanamke anachangia vipi upembezwaji wa kijinsia? Maswali haya ndiyo tulipania kuyajibu katika Makala haya.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Ameir, S. (2010). ‘Shein aieleza Afrika: Msidharau Maarifa ya Asilia katika kukabiliana Na changamoto za Mazingira zinazolikabili Bara la Afrika’ katika Jarida la Umaskini na Mazingira.Toleo la 8:3-4 Penplus Ltd: Tanzania.

Chesaina, C. (1987). Women in African Drama: Representation and Role (Doctoral dissertation, University of Leeds).

Eagleton, M. (1991). Feminist Literary Criticism - Woman in Literature. London: Longhorn Publisher.

Lugano, R. S. (1989). Mwanamke katika Riwaya za Kezilahabi. Gainesville: Florida University Press.

Kamwara, K. (2016). ‘Mtazamo Mpya katika Sauti ya Kike katika Riwaya ya Kiswahili’. Tasnifu ya Uzamili Chuo Kikuu cha Mount Kenya. (Haijachapishwa).

Mavisi, R. (2007). ‘Usawiri wa wahusika wa kike katika kazi za Z. Burhani’. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa).

Mikell, G., (1997). African Feminism: The Politics of Survival in Sub-Sahara Africa. University of Pennsylvania Press Mohamed, S.A. (1980), Utengano. Nairobi: Longhorn Publishers.

Mogere, O. (2003). ‘Uhakiki wa riwaya za Said Ahmed Mohamed katika misingi ya Kiufeministi’. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa)Momanyi, C.

(1998). ‘Usawiri wa Mwanamke Mwislimu katika jamii ya Waswahili kama inavyobainika katika Ushairi wa Kiswahili’. Tasnifu ya Uzamifu. Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa)

Mohamed, S.A. (1980), Utengano. Nairobi: Longhorn Publishers

Momanyi, C. (2006). Tumaini. Nairobi: Vide – Muwa publishers.

Momanyi, C. (2009). Nakuruto. Nairobi: Longhorn publishers.

Muindi, A. (1990). Usawiri wa Wahusika Makahaba Katika Riwaya za S.A Mohamed. Tasnifu ya Uzamifu Chuo Kikuu cha Kenyatta. Haijachapishwa.

Musyoka F.M. (2011). ‘An Analysis of the Women in Gender Role-Play Dyanamics in Kenyan Kiswahili Drama.’ (Doctoral dissertation, University of Nairobi, Kenya).

Mwanahamisi, H. (2018, 24 Julai) Mwanamke Bomba. Msururu wa Vipindi vya Televisheni ya Citizen Kenya. https://youtu.be/WvlnJgnPyVo

Ndungo, C. (1998). Images of Women as Exemplified in Gikuyu and Swahili Proverbs. Tasnifu ya Uzamifu Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa).

Nkealah, N. (2006) ‘Conceptualizing Feminism in Africa. The challenges facing African Women writers and Critics. English Academy Review, 23:1, 133-144 DOI:10.1080/10131750608540431’

Pinkie, M., (2006). Theorizing African Feminism(s): The Colonial Question. QUEST: An African journal of Philosophy, 20(1-2), 11-22.

Steady, F. C. (1981). Reflecting on the Politics of Sisterhood. New York: African Wordpress.

Swaleh, A. (2011). A critique of the mapping and construction of gender identity and authority in selected Kiswahili novels (Doctoral dissertation, University of Nairobi, Kenya).

Wamitila, K.W. (2002). Uhakiki wa Fasihi. Nadharia na Mbinu. Nairobi: Focus Publishers.

Tarehe ya Uchapishaji
10 June, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Kamwara, K. (2024). Upembezwaji wa Mwanamke kama Kihunzi cha Ufanisi wa Ujenzi wa Ujitambuzinafsia Katika Baadhi ya Bunilizi za Clara Momanyi. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 283-296. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1978