Uamili wa Ufokasi katika Kudhihirisha Itikadi

  • Dinah Sungu Osango Chuo Kikuu cha Nairobi
  • Mwenda Mbatiah, PhD Chuo Kikuu cha Nairobi
  • Timammy Rayya, PhD Chuo Kikuu cha Nairobi
Keywords: Ufokasi, Ngazi Ya Itikadi, Mkabala, Naratolojia, Itikadi Ya Kibepari, Imani
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya yanachunguza ngazi ya itikadi na uamilifu wake katika riwaya teule za Kiswahili kupitia kwa ufokasi.  Riwaya teule ni Haini (Adam Shafi, 2003), Makuadi wa Soko Huria (C. Chachage, 2005), Harufu ya Mapera (K. Wamitila, 2012), Hujafa Hujaumbika (F. Kagwa, 2018), Ndoto ya Almasi (Ken Walibora, 2006) na Nyuso za Mwanamke (S. Mohamed, 2010). Ngazi ya itikadi ni mojawapo ya ngazi mbalimbali za ufokasi zilizopendekezwa na wananaratolojia. Kimsingi, ufokasi ni mkabala ambao huchukuliwa katika kuwasilisha simulizi na kuikuza hadithi kwa ujumla. Data ya kuudhibiti na kuthibitisha madai ya mjadala wetu imetolewa katika  riwaya teule.  Uteuzi wa riwaya hizi unahalalishwa kwa misingi kwamba, hizi ni riwaya zilizo na matini pana zinazowezesha udondoaji wa mifano faafu inayodhihirisha ngazi ya itikadi na wakati huo huo kudhihirisha uamili wa ngazi hiyo katika simulizi. Mjadala wa kimsingi katika makala haya umekitwa na kuongozwa na teneti za kimsingi za nadharia ya naratolojia ambayo inatambua ufokasi kama kipengele muhimu katika uwasilishaji wa simulizi. Uchunguzi wetu umeonyesha kuwa, kupitia kwa ufokasi nje na ndani, waandishi wa riwaya teule wamedhihirisha ngazi ya itikadi. Imebainika kuwa wahusika mbalimbali huwa na tabia, mitazamo, misimamo na hisia fulani kuhusu masuala mbalimbali kutokana na athari za itikadi zinazotawala mazingira au matamanio yao

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Althusser, L. (1981). “Ideology and Ideological State Apparatuses”. Katika Lenin and Other Essays. (B. Brewster, Mtaf.). London: New Left Books.

Bal, M. (1985). Narratology. Introduction to the Theory of Narrative. Toleo la 3 (2009). Toronto: University of Toronto Press.

Barthes, R. (1966). Introduction to the Structural Analysis of Narratives. Cambridge: University Press.

Chachage, S. C. (2005). Makuadi wa Soko Huria. Dar es Salaam: E&D Limited.

Chatman, S. (1978). Story and Discource: Narrative Structure in Fiction and Film. Ithaca: Cornell University Press.

Eagleton, T. (1976). M a r x i s m and Literary Cr it ic is m. London: Methuen.

Genette, G. (1972). Narratology. Imesomwa (Jumamosi 1/07/2017). http://www.signosemio.com/genette/narratology.asp

Gholami, V. (2013). “Conrad and Narrative Theory: A Narratological Reading of Selected Novels of Joseph Conrad. Tasnifu ya Uzamivu. Chuo Kikuu cha London. Haijachapishwa.

Gramsci, A. (1985). Selections from Cultural Writings. London: Lawrence and Wishart.

Greimas, A. J. (1973). On Meaning. Minnesota: University of Minnesota Press.

Hancock, B. (2002). An Introduction to Qualitative Research. Nottingham: Trent Focus Group.

Kagwa, F. M. (2018). Hujafa Hujaumbika. Nairobi: Longhorn.

Kennedy, E. (1978). A Philosophe in the Age of Revolution: Destutt de Tracy and the Origins of ‘Ideology’. Philadelphia: American Philosophical Society.

Marx, K. (1979). Pre-Capitalist Social Economic Formations. Moscow: Progress Publishers.

Marx, K na F. Engels. (1977). The German Ideology. London: Lawrence and Wishart.

Mohamed, S. A. (1995). Kunga za Nathari ya Kiswahili: Tamthilia, Riwaya na Hadithi Fupi. Nairobi: East African Education Publishers.

Mohamed, S. A. (2010). Nyuso za Mwanamke. Nairobi: Longhorn Publishers.

Rimmon-Kenan, S. (1983), (2003). Narrative Fiction: Contemporary Poetics. London: Routledge.

Shafi, A. S. (2003). Haini. Nairobi: Longhorn Publishers.

Shivji, I. (2002). Makuadi wa Soko Huria (Chachage, S. Chachage): Hotuba ya Uzinduzi wa Kitabu, katika Mulika Na. 26 (2000-2002): 93-97.

Todorov. T. (1990). Genres in Discourse. New York: Cambridge Press.

Walibora, K. (2006). Ndoto ya Almasi. Nairobi: Moran Publishers.

Wamitila, K. W. (2012). Harufu ya Mapera. Nairobi: Vide-Muwa Publishers.

Tarehe ya Uchapishaji
28 May, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Osango, D., Mbatiah, M., & Rayya, T. (2024). Uamili wa Ufokasi katika Kudhihirisha Itikadi. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 272-282. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1959