Tathmini ya Aina za Ujumbe Unaoibuliwa Kutokana na Matumizi ya Lugha katika Kuwasilisha Habari za Mazingira katika Gazeti la Taifa Leo, Kenya

  • Nelly Nzula Kitonga, PhD Chuo Kikuu cha Garissa
Keywords: Aina ya ujumbe, Habari za Mazingira, Gazeti la Taifa Leo, Kiswahili
Sambaza Makala:

Ikisiri

Utafiti huu unahusu aina za ujumbe unaoibuliwa kutokana na matumizi ya lugha katika kuwasilisha habari za mazingira kwenye gazeti la Taifa Leo nchini Kenya. Gazeti la Taifa Leo huwasilisha habari kwa wasomaji kwa lugha ya Kiswahili. Lugha ya Kiswahili inatambuliwa na Katiba ya Kenya kama lugha ya Taifa na pia lugha rasmi sambamba na lugha ya Kiingereza. Mazingira ni suala mtambuko na nyeti kitaifa na kimataifa. Mazingira yanaathiri maisha ya kila kiumbe kila siku kwa njia moja au nyingine. Jamii hupata takriban kila kitu kinachohusiana na mazingira yake kupitia vyombo vya habari. Moja kati ya njia zinazotumiwa na vyombo vya habari kupitisha ujumbe kuhusu mazingira kwa watu ni lugha. Inatarajiwa kwamba, kwa vile vyombo vya habari, Gazeti la Taifa Leo likiwemo, vimetwikwa jukumu la kuwapasha wanajamii yale yanayoendelea duniani kuhusiana na mazingira, vitafanya hivyo kwa namna ambayo itawawezesha watu kufahamu umuhimu wa mazingira na hivyo kuingiliana nayo kwa njia chanya. Hoja hii inatokana na imani kwamba mtu huelewa ujumbe kulingana na jinsi mwasilishi wa ujumbe husika anavyoteua lugha ili kuwasilisha anachokusudia. Madhumuni ya mwandishi wa matini ndiyo yanamwongoza katika uteuzi wa kipengele cha lugha atakachozingatia katika kuandika anachokusudia kuandika. Aidha, lengo la mwandishi wa matini ndilo huamua jinsi atakavyokiwasilisha kile anachokiandika kwa wasomaji. Kwa hivyo, matumizi ya lugha kwa namna tofauti humwezesha mwandishi wa matini kuibua aina tofauti za ujumbe ili kutimiza madhumuni yake. Uchunguzi huu ulidhamiria kubainisha aina za ujumbe uliowasilishwa na waandishi wa habari katika gazeti la Taifa Leo. Utafiti huu ulifanyika maktabani ambapo taarifa kuhusu habari za mazingira zilizochapishwa katika gazeti la Taifa Leo zilichanganuliwa. Data ilikusanywa kwa kudondoa matumizi ya lugha katika uwasilishaji wa taarifa za mazingira kutoka magazeti ya Taifa Leo teule pamoja na aina za ujumbe uliojitokeza katika habari hizo.Utafiti huu ulibainisha kwamba kuna aina tofauti za ujumbe katika taarifa za mazingira zilizochunguzwa: maana dhamirifu, maana akisifu, maana athirifu, maana kimtindo, maana halisi na maana ashirifu

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Cruse, D.A. (2010). Meaning in Language: An Introduction to Semantics and Pragmatics. Oxford: Oxford University Press.

Griffiths, P. (2006). English semantics and pragmatics. Edinburgh: Edinburgh University Press.

Kearns, K. (2000). Semantics: modern linguistics series. London: Palgrave Macmillan (UK)

Saeed, J. (2009). Semantics. Malden: Wiley-Blackwell Publishers.

Oduor, J.A.(2016). An analysis of Kenya`s mainstream print media`s usage of objectification and anchoring to represent the kenyan international crimnal court cases in the Daily Nation and the Standard news articles. MA Thesis, Maseno University, Unpublished.

Tarehe ya Uchapishaji
21 May, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Kitonga, N. (2024). Tathmini ya Aina za Ujumbe Unaoibuliwa Kutokana na Matumizi ya Lugha katika Kuwasilisha Habari za Mazingira katika Gazeti la Taifa Leo, Kenya. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 244-252. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1936