Nafasi Ya Fasihi Andishi Ya Watoto Kama Chombo Cha Malezi Kwa Watoto Wa Kisasa

  • Naomi Nzilani Musembi, PhD Chuo Kikuu cha Jaramogi Oginga Odinga cha Sayansi na Teknolojia
  • Peter Karanja, PhD Chuo Kikuu cha Gretsa
Keywords: Mtoto, Fasihi ya Watoto, Chombo cha Malezi, Malezi
Sambaza Makala:

Ikisiri

Fasihi andishi ya watoto ina nafasi kubwa ya kuwasaidia watoto kuelewa mazingira yao pamoja na kujenga mwonoulimwengu wao kulingana na wanachosoma. Hii ni kutokana na sababu kwamba watoto hubwia wasomacho kuwa kiwakilishi cha uhalisia katika jamii. Fasihi ya watoto huchokoza fikra zao na kuwachochea kufikiria, kuimarisha msamiati wao, na pia huwasaidia kujifahamu kando na kuwafahamu watu wengine. Fasihi hii hivyo basi inajitokeza kama kioo ambacho watoto wanajiona kwacho na pia dirisha la kuwawezesha kuutalii ulimwengu unaowazunguka. Fasihi andishi ya watoto vilevile ina uwezo wa kuonyesha kuwa, watu tofauti wanaweza kufanya kazi pamoja bila ubaguzi wa aina yoyote. Waandishi wa fasihi ya watoto hivyo basi hubuni ulimwengu ambao watoto wanaweza kuutambua kwa urahisi na kujinasibisha nao. Kwa msomaji mtoto, hali hii hurahisisha uvushaji wa maarifa na kuifanya fasihi andishi yao kuwa nyenzo muhimu ya kuimarisha mtagusano wa kijamii pamoja na uvushaji wa maarifa ya kiakademia. Lengo la makala hii ni kubainisha kuwa, kupitia fasihi andishi ya watoto ya Kiswahili, msomaji mtoto anaweza kufafanukiwa na hali halisi ya maisha yake na wakati huo huo kupata suluhu ya kutatua matatizo yanayomkumba na ya jamii yake. Kazi hii itafanya hivyo kwa kuhakiki vitabu vya fasihi andishi ya watoto vifuatavyo:  Momanyi, C (2006) Tumaini, Momanyi, C.  (2005), Siku ya Wajinga, Musembi, N. (2009) Nipe Sababu, Musembi, N. (2019) Dhiki Yangu Ngugi, P. (2003) Usicheze na Moto Mdari, A. (2001) Alitoroka kwao. Ndoto ya Mwanafunzi, Manji, M (2013), na Safari ya Sungura Omusikoyo T, ( 2021).  Makala hii inatoa mwito kwa waandishi wa fasihi ya watoto watunge vitabu vitakavyo wasaidia watoto kukabiliana na hali zote za maisha yao wanapoendelea kukua katika dunia hii inayobadilika kila uchao

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Hunt, P. (1991) Criticsm, Theory and Childrens’s Literature. Oxford: Blackwell.

Manji, A. (2013) Ndoto ya Mwanafunzi: Nairobi. The Jomo Kenyatta Foundation.

Matundura, B. (2007). Taswira Dumifu za Uana katika Fasihi ya Kiswahili ya Watoto. Tasnifu ya Uzamili ya Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa).

Mbuthia, E. M (2018). The Role of Children’s Literature in Fomulating their World View in International Journal of Education and Research. Vol 6. No. 2 Feb. 2018.

Mdari, A. (2001) Alitoroka Kwao. Nairobi: Focus Books.

Momanyi, C. (2006) Tumaini. Vide-Muwa: Nairobi

Momanyi, C. (2005) Siku ya Wajinga. Nairobi: Phoenix Publishers.

Musembi, N. (2022). Ukataji Tamaa miongoni mwa Watoto katika jamii ya Kisasa. Tathmini kutoka Riwaya ya Kiswahili. Katika Jarida la CHAKAMA Juzuu 1 uk 141-147.

Musembi, N. N. (2018). “Nafasi ya Fasihi Simulizi katika Jamii Inayobadilika Karne ya 21”. Makala yaliyowasilishwa katika Kongamano la Kimataifa la Chaukidu, SUZA.

Musembi, N.N (2009). Nipe Sababu. Nairobi: Oxford University Press.

Musembi, N.N. (2019). Dhiki Yangu. Naorobi. East African Educational Publishers.

Mwanzi, H. (2006) “Children’s Literature: The Concept of Socializing the Young” In the Nairobi Journal of Literature No 4. pp 49.

Ndungo, C. (1985) “Matumizi ya Tamathali za Usemi katila Lugha ya Kisasa”. Katika Njogu, K. na wengineo (Wah.). Fasihi simulizi ya Kiswahili. Nairobi: Twaweza Communications.

Ngugi, P.M. (2003). Usicheze na Moto. Nairobi: Oxford University Press.

Ngugi, P.M. Nabea, W. (2011). Children’s Literature in Kiswahili: A Stylistic Approach katika East African Literature: Essays on Written and Oral traditions, Logos Verlag Berlin. Kur. 223-244.

Omolo, O. (1971) Uhalifu Haufai: Longhorn Publishers Ltd.

Omusikoyo, T. (2021). Safari ya Sungura: Nairobi: Story Moja Publishers.

Ngugi, P.M (2016). Usawiri wa Masuala Ibuka katika Fasihi ya Watoto: Mifano kutoka Kenya katika: Mulika, No 35. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kur. 76-86.

Wamitila, K.W. (2008). Kanzi ya Fasihi. Nairobi: Vide-Muwa Publishers Limited.

Tarehe ya Uchapishaji
13 May, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Musembi, N., & Karanja, P. (2024). Nafasi Ya Fasihi Andishi Ya Watoto Kama Chombo Cha Malezi Kwa Watoto Wa Kisasa. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 224-232. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1924