Maana za Majina ya Asili ya Watoto katika Jamii ya Waasu

  • Janeth Jafet Shule ya Sekondari Kitefu
  • Perida Mgecha, PhD Chuo Kikuu Tumaini Makumira
Keywords: Maana, Majina, Kichasu, Jamii ya Waasu
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inachunguza maana za majina ya asili ya watoto katika jamii ya Waasu. Malengo mahususi yakiwa kwanza kubaini majina ya asili ya watoto, na pili kueleza maana zilizobebwa na majina hayo. Utafiti huu ni wa kitaamuli hivyo umetumia usanifu wa kifenomenolojia. Watoataarifa waliohusika katika kutoa data ni 18 ambao wamepatikana kwa mbinu ya usampulishaji tabakishi na usampulishaji tajwa. Data za makala hii zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya usaili na majadiliano ya vikundi lengwa; kisha zikachanganuliwa kwa mbinu ya kusimba maudhui. Nadharia ya Uumbaji iliyoasisiwa na Sapir (1958) ndiyo iliyotumika katika makala hii. Matokeo yamebainisha majina ya asili ya watoto 145. Maana za majina haya zimegawanyika katika makundi yafuatayo: majina yenye maana zitokanazo na imani kwa Mwenyezi Mungu, mahali mtoto alipozaliwa, wanyama, misimu ya miaka na siku, majanga, vyakula na matukio ya furaha. Utafiti huu una mchango mkubwa katika kuhifadhi historia, na utamaduni uliojificha katika lugha ya Kichasu. Hata hivyo, tafiti zaidi kuhusu majina zifanyike katika jamii nyingine kwani jamii zinatofautiana katika asili, historia, shughuli za kijamii na utamaduni

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Agyekum, K. (2006). The Socialinguistics of Akan Personal Names. International Journal of Humanities and Social Science, 15(2), 206–23.

Azael, R. (2013). Maana ya Majina ya Asili katika Jamii ya Kiuru.Tasnifu ya Umahiri katika Kiswahili (haijachapishwa), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Baitan, B. (2010). A Mopho Semantic Analysis of Ruhaya Person Names. M.A. Dessertation (unpublished), University of Dar es Salaam.

Creswell, J. W. & Creswell, J. D. (2022). Reseach Design: Qualitative, Quantitative and Mixed Method Approaches. Califonia: Sage Publications. Inc.

Elihaki, Y. (2012). Majina ya Mahali katika Jamiilugha ya Chasu.Tasnifu ya Umahiri katika Kiswahili (haijachapishwa), Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Kalekwa, L. B. (2018). Uchambuzi wa Kiisimujamii wa Majina ya Koo za Kisukuma, Wilaya ya Misungwi. Tasnifu ya shahada ya Umahiri ya Kiswahili, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Kihore, Y. M. (2009). Isimu jamii Sekondari na Vyuo. Chuo Kikuu Dar es Salam: TUKI.

Leech, G. N. (1974). Semantics: The Study of Meaning. Auxland: Penguin Books.

Lenjima, L. (2019). Kuchunguza Maana ya Majina Asilia ya Watu katika Jamii ya Wajita Mkoani Mara Nchini Tanzania. Tasnifu ya shahada ya Umahiri katika Kiswahili (haijachapishwa), Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Masanja, N. T. (2019). Uchunguzi wa Kisemantiki wa Majina ya Asili katika Koo za Ginantuzu. Tasnifu ya shahada ya Uzamivu ya Kiswahili (haijachapishwa), Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Massamba, D. P. B. (2009). Kamusi ya Isimu na Falsafa. Dar es Salaam: TUKI.

Mbiti, S. (1990). African Religion and Philosophy. USA: Heinemann Educational Books Inc.

Mulokozi, M. M. (1996). Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Muzale, H. R. T. (1998). The Linguistic and Social Culture Aspects in Intercustrine Bantu Names. Kiswahili, 2 (61), 28-29.

Nyanganywa, M. (2013). Uchunguzi wa Kisemantiki na Taratibu za Utoaji wa Mjina ya Kijita. Tasnifu ya M.A Kiswahili (haijachapishwa), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Nyiti, J. (2021). Maana ya Majina ya Koo katika Jamii ya Wameru: Tasnifu ya shahada ya Umahiri katika Kiswahili (haijachapishwa), Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira.

Ponera, S. A. (2019). Misingi ya Utafiti wa Kitaamuli na Uandishi wa Tasnifu. Dodoma: Central Tanganyika Press.

Rashidi, M. O. (2017). Michakato na Mbinu Zilizotumika katika Uundaji wa Majina ya Mitaa katika Wilaya ya Mjini Unguja. Tasnifu ya Shahada ya Umahiri katika Isimu ya Kiswahili (haijachapishwa), Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Resani, M. (2016). Maana katika Majina ya Wabena Nchini Tanzania. Mulika, Na. 35.

Resani, M. (2017). Semantiki na Pragmantiki ya Kiswahili. Dar es Salam: Karljamer Print Technology.

Sapir, E. (1958). Language. New York: Harcourt, Brace and Co.

Tarehe ya Uchapishaji
15 March, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Jafet, J., & Mgecha, P. (2024). Maana za Majina ya Asili ya Watoto katika Jamii ya Waasu. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 170-181. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1826