Mikabala Tofauti ya Waandishi wa Vitabu vya Kiada kuhusu Kipengele cha Mtindo wa Uandishi Insha za Kiswahili Nchini Kenya

  • Nester Ateya Chuo Kikuu cha Kibabii
  • Eric Walela Wamalwa Chuo Kikuu cha Kibabii
  • Stanley Adika Kevogo Chuo Kikuu cha Jaramogi Oginga Odinga cha Sayansi na Teknolojia
Keywords: Mikabala, Mtindo, Vitabu Vya Kiada, Ufundishaji, Ujifundishaji
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya yanabainisha mikabala ya waandishi wa vitabu vya kiada katika ufundishaji na ujifundishaji wa mtindo wa insha za Kiswahili kwa shule za upili nchini Kenya. Mikabala tofauti ya waandishi aghalabu huwa chanzo cha utata miongoni mwa walimu na wanafunzi na hivyo kuathiri matokeo ya mtihani wa kitaifa. Uchunguzi huu umekitwa kwa mihimili ya Nadharia ya Mtindo iliyoasisiwa na Louis Tonko Milic. Nadharia hii inashikilia kuwa mtindo hutegemea mtu binafsi. Utafiti huu ulitumia muundo wa kimaelezo, mkabala wa kithamano. Idadi lengwa ya utafiti ni walimu wa somo la Kiswahili 73, wanafunzi 2,000 na vitabu vya kiada 7 vya shule za upili. Kwa hivyo, usampulishaji wa kimakusudi ulitumiwa kuteua walimu 22, wanafunzi 320 na vitabu vya kiada 6. Mbinu za ukusanyaji wa data zilizotumika ni uchanganuzi wa yaliyomo, mahojiano na hojaji. Data ilichanganuliwa kwa kutumia asilimia, majedwali na kuwasilishwa kiufafanuzi. Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kwamba, matumizi ya vitabu vya kiada tofauti tofauti yanazua mikabala tofauti katika ufundishaji na ujifundishaji wa mtindo wa insha. Hali hii inatokana na waandishi wa vitabu kiada kuwa na mikabala tofauti kuhusu mtindo wa insha za Kiswahili. Matokeo ya uchunguzi huu ni muhimu kwa walimu na wanafunzi wa Kiswahili katika shule za upili, viwango vingine vya elimu na wakuza mitaala pamoja na waandishi wa vitabu vya kiada. Wizara ya Elimu pamoja na vyuo vya walimu kupitia warsha na maarifa zaidi ya yale ya vitabu vya kiada, watafaidi mikakati ya kuimarisha ufundishaji na ujifundishaji wa somo la insha

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Butler, P. (2008). Out of Style: Reanimating Stylistic Study in Composition and Rhetoric. All USU Press Publications. 162. https://digitalcommons.usu.edu/usupress_pubs/162

Corbett, E. (1998). Approaches to the study of style. Teaching Composition 12(1): 83-130.

KIE. (2002). Kiswahili kwa Sekondari Mwongozo wa Walimu. Nairobi: KIE.

KNEC. (2020). Mwongozo wa kusahihishia insha. Naiobi: Kenya National Examination Council.

KNEC. (2020). The year 2019 Examination Report. Nairobi: Kenya National Examination Council.

Milic, L. (1965). Theories of style and their implications for the teaching of composition and other Essays. Ilinois: College composition and communication.

Montin, R.A. (2011). From theory to praxis: Style, dualism, and the composition classroom. Tasnifu ya Uzamili (MA) isiyochapishwa. Stillwater, OK: Oklahoma State University.

Mumbo, C. & Ngamia, F. (2013). Johari ya Kiswahili kidato cha pili Nairobi: East Africa Educational Publishers.

Ngure, A. (2011). Hazina ya Kiswahili, kidato cha tatu, Nairobi: Longman Kenya.

Nyariki, E. (2021). Tofauti kati ya muundo na mtindo wa insha. Taifa Leo, Februari 22, 2021. Nairobi: Nation Media Group.

Richards, J.C. (2001). Curriculum Development in Language Teaching. Cambridge: Cambridge University Press.

Vonyoli A. J, Watuha, A. I, Mutekwa. F.O. ... Waweru, M.K. (2015). Kiswahili Kitukuzwe: kwa kidato cha tatu, kitabu cha mwanafunzi (Toleo la tano). Nairobi: Kenya Literature Bureau.

Vonyoli, A. Watuha, A., Mutekwa, F.O. ... Waweru, M.K. (2014). Kiswahili Kitukuzwe: kwa kidato cha kwanza, kitabu cha mwanafunzi (Toleo la tano). Nairobi: Kenya Literature Bureau.

Vonyoli, A.J, Watuha, A.I, Mutekwa, F.O. ... Waweru, M.K. (2014). Kiswahili Kitukuzwe: kwa kidato cha Nne, kitabu cha mwanafunzi (Toleo la tano). Nairobi: Kenya Literature Bureau.

Walibora, K. & Wangendo, F. (2004). Uhondo wa Kiswahili kwa shule za upili kitabu cha mwanafunzi kidato 1. Nairobi: Moran (E.A) Publishers.

Wamitila, K.W. & Waihiga, G. (2010). Chemichemi za Kiswahili kidato cha pili. Nairobi: Longhorn Publishers.

Wamitila, K.W. (2015). Chemichemi za Kiswahili kidato cha nne. Nairobi: Longhorn Publishers.

Tarehe ya Uchapishaji
6 March, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Ateya, N., Wamalwa, E., & Kevogo, S. (2024). Mikabala Tofauti ya Waandishi wa Vitabu vya Kiada kuhusu Kipengele cha Mtindo wa Uandishi Insha za Kiswahili Nchini Kenya. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 114-123. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1803