TEHAMA na Athari zake katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa Kiswahili katika Shule Teule za Sekondari Nchini Rwanda

  • Stanislas Munyengabire Chuo Kikuu cha Rwanda-Koleji
Keywords: TEHAMA, Lugha ya Pili, Ufundishaji na Ujifunzaji, Zana za Kiteknolojia
Sambaza Makala:

Ikisiri

Katika enzi hizi, TEHAMA inatazamwa kama kifaa cha kurahisisha maisha. Inarahisisha maisha kwa kuathiri kila uwanja wa maisha ya mwanadamu (Mikre, 2011). Athari hizi zinajitokeza katika shughuli zote za mtu wa kisasa. Katika uga wa elimu, ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya pili nao uliathiriwa sana kutokana na TEHAMA. Hali hii ilisababisha kuibuka kwa makala haya kutokana na malengo mahsusi matatu. Lengo la kwanza lilikuwa kubainisha mchango wa TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kwa wanafunzi wa kidato cha nne katika shule teule za sekondari nchini Rwanda. Lengo la pili lilikuwa kuchambua hasara za matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wa kidato cha nne katika shule teule za sekondari nchini Rwanda. Lengo la tatu nalo lilikuwa kubainisha namna ya kutumia TEHAMA katika ufundishaji wa Kiswahili nchini Rwanda. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya ushuhudiaji, usaili, na upitiaji wa maandiko. Sampuli ilikuwa walimu na wanafunzi wa Kiswahili katika kidato cha nne katika shule teule za sekondari nchini Rwanda pamoja na wazazi wa wanafunzi hao. Sampuli ilipatikana kwa mbinu ya sampuli lengwa. Utafiti ulioibua makala haya uliongozwa na Nadharia ya Uunganisho. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba TEHAMA ni nyenzo mwafaka katika ufundishaji wa Kiswahili. Hii ni kwa sababu hutumiwa kufundisha msamiati, sarufi na stadi nne za lugha hasa kwa kutumia nyeno kadhaa za kiteknolojia. Aidha, utafiti huu umebaini kwamba TEHAMA inapotumiwa vibaya inaweza kusababisha madhara makubwa kwa wanafunzi. Baadhi ya madhara hayo ni pamoja na kuamini lugha ya mtandaoni zaidi, maandishi ya mkononi (kalamu) mabaya, kuathiriwa na tabia na damaduni za nje, na kutokubaliana kati ya mwalimu na wanafunzi juu ya masomo. Mwishoni, makala imejadili namna ya kuitumia TEHAMA katika ufundishaji wa lugha ya pili hususan nchini Rwanda

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Ahmadi, A., Abzari, M., Nasr Isfahani, A., & Safari, A. (2018). High-Performance, Knowledge Sharing and ICT Skills. Human Systems Management, 37(3), 271-280.

Amin, E. (2020). A Review of Research into Google Apps in the Process of English Language Learning and Teaching. Arab World English Journal (AWEJ), 11(1), 399-418.

Arnell, A. (2012). The use of ICT in the Teaching of English Grammar. Sweden: Linnaeus University, Course Code: 2EN10E. Web, 7, 1-29.

Carr, N. (2011). The Shallows: What the Internet is Doing to Our Brains. New York: W. W. Norton & Company.

Chepkemoi, N., & Wanyonyi, D. (2017). The use of ICT in teaching kiswahili play in secondary schools in Uasingishu County, Kenya. European Scientific Journal, 13 (25) 1857 –7881.

Chikamma. M. A & Nwaudu. U. C. (2018). Language Teaching and Technology. Journal of Languages and Literatures (JOLL). 3 (2) 190-198.

Downes, S. (2007). Places to Go: Google's Search Results for Net Generation". Innovate Journal of Online Education, 3 (4), 1-4.

Mikre, F. (2011). The Roles of Information Communication Technologies in Education: Review Article with Emphasis to the Computer and Internet. Ethiopian Journal of Education and Sciences, 6(2), 109-126.

Hennessy, S., Onguko, B., Harrison, D., Ang’ondi, E. K., Namalefe, S., Naseem, A., & Wamakote, L. (2010). Developing the use of information and communication technology to enhance teaching and learning in East African schools: Review of the literature. Centre for Commonwealth Education & Aga Khan University Institute for Educational Development–Eastern Africa Research Report, 1, 1-3.

Kavitharaj, K. (2017). ICT to enhance speaking skills. International Journal of English Language, Literature in Humanities (IJELLH), 5(9), 843-847.

Miller, M. (2011). Using Google Apps. US: Pearson Education, Inc. Publishing Limited.

Mobi, M. I., U Onyenanu, I., & C Ikwueto, O. (2015). A study of the negative influences of ICT on secondary school students in Nigeria. American Academic & Scholarly Research Journal, 7(5).

Mugiraneza, J. P (2021). Digitalization in Teaching and Education in Rwanda: Digitalization, The Future of Work and the Teaching Profession Project, International Labour Office, Geneva, Switzerland.

Mukama, E. (2009). Information and Communication Technology in Teacher Education: Thinking and learning in computer‐supported social practice. Linköping University, Faculty of Educational Sciences.

Naciri, H. (2019). The Use if ICT to Enhance Students’ Speaking Skills. University Sultan Moulay Slimane, Beni Mellal, Morocco.

REB, (2015). Competence-based Curriculum: Summary of Curriculum Framework Pre-Primary to Upper Secondary 2015. WordCore Communications Limited.

Idayani, A., & Sailun, B. (2017). Roles of Integrating Information Communication Technology (ICT) in Teaching Speaking at the First Semester of English Students oF FKIP UIR. J-SHMIC: Journal of English for Academic, 4(2), 12-23.

Spitzer, M. (2014). Information Technology in Education: Risks and Side Effects. Trends in Neuroscience and Education, 3(3-4), 81-85.

Uwizeyimana, V. (2015). An Investigation into the Contribution of Mobile-assisted Language Learning to the Acquisition of English as a Second Language in Rwanda. Stellenbosch: Stellenbosch University.

Yunus, M. M., Nordin, N., Salehi, H., Sun, C. H., & Embi, M. A. (2013). Pros and Cons of Using nICT in Teaching ESL Reading and Writing. International Education Studies, 6(7), 119-130.

Ugwu, I. (2015). Language Teaching Methods: A Conceptual Approach. Obudu Journal of Educational Studies. 9 (1) 20-34.

Mofareh, A. (2019). The Use of Technology in English Language Teaching. Frontiers in Education Technology 2 (3). www.scholink.org/ojs/index.php/fet.

Mechlova, E & Malcik. M (2012). ICT in Changes of Learning Theories. Emerging eLearning Technologies & Applications (ICETA), 2012 IEEE 10th International Conference. 10.1109/ICETA.2012.6418326.

Shang, H. F. (2007). An Exploratory Study of E-mail Application on FL Writing Performance. Computer Assisted Language Learning, 20(1), 79-96.

Padurean, A., & Margan, M. (2009). Foreign language teaching Via ICT. Revista de Informatica Sociala 7(12), 97-101.

Hussain, Z. (2018). The Effects of ICT-Based Learning on Students’Vocabulary Mastery in Junior High Schools in Bandung. International Journal of Education, 10(2), 149-156.

Korlotyan, D. (2015). New Technologies in Learning English. Hupatikana kwenye: https://prezi.com/d4ehdwyeqla5/new-technologies-in-learning-english.

Tarehe ya Uchapishaji
15 March, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Munyengabire, S. (2024). TEHAMA na Athari zake katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa Kiswahili katika Shule Teule za Sekondari Nchini Rwanda. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 155-169. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1795