Mitazamo ya Kiskaz Kuhusu Covid-19 Inavyojitokeza katika Lugha ya Wananchi Nchini Kenya

  • Alexander Rotich, PhD Chuo Kikuu cha Kabianga
Keywords: Skaz, COVID-19, Mtazamo, Kizuizui, Kericho
Sambaza Makala:

Ikisiri

Madhumni ya makala haya yalikuwa ni kubainisha na kuchanganua mitazamo ya WaKenya kuhusu Tangaavu la Korona (COVID-19) kama inavyodhihirika kupitia mazungumzo ya kikawaida, Skaz. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, tafiti za awali kuhusu mada hii hazikukitwa katika misingi ya Skaz. Kwa hivyo, taarifa nyingi kuhusu Tangaavu la Korona zilizowasilishwa na Shirika la Afya Ulimwenguni pamoja na Wizara ya Afya nchini Kenya zilikuwa za kitaalamu (kiakademia). Utafiti huu ulikuwa wa nyanjani na ulifanyika Kericho, Kenya. Mtafiti aliteua sampuli kimakusudi na kukusanya data kwa kutumia mbinu ya utazamaji nyanjani. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ya Usemezano ikijumuisha sifa za Skaz kama ilivyoelezwa na Bakhtin ikitiliwa nguvu na Mbinu ya Urazini wa Kiwatu kama ilivyoendelezwa na Sacks na wenzake. Uchanganuzi wa data ulionesha kuwa, mwanzomwanzo, kutokana na kukosa ufahamu wa kitaaluma kuhusu ugonjwa “mpya” Tangaavu la COVID-19 kwa jumla, bila kukusudia kupotosha WaKenya waliibuka na mitazamo mbalimbali kuhusu ugonjwa huu. Mitazamo hii pia ilitokana na jitihada za hekaheka kutafuta njia za kuzuia usambazaji na hata tiba miongoni mwa wanajamii. Utafiti huu umeweka wazi mitazamo “hasi” kuhusu ugonjwa wa COVID-19 jinsi ili(na)vyodhihirika katika mazungumzo ya kikawaida na hivyo kuwafaidi watafiti wa utabibu na wapangaji sera za kiserikali kutilia maanani mitazamo katika lugha ya kikawaida haswa kwenye majanga ya kiulimwengu

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

AFP. (2020) Covid Pandemic and Lockdown: How 2020 Changed the World. Ilisomwa https://www.standardmedia.co.ke/article/2001398421/covid-pandemic-and-lockdown-how-2020-changed-the-world

Bakhtin, M.M (1981). Dialogic Imagination: Four essays. Michael H. (mh). Texas University Press.

BBC (8 June, 2020) Coronavirus: John Magufuli declares Tanzania free of Covid-19. Ilisomwa: https://www.bbc.com/news/world-africa-52966016

CGTN. (24 August, 2020). Misconceptions on COVID-19 persists in Kenya's rural areas. Ilisomwa: https://newsaf.cgtn.com/news/2020-08-24/Misconceptions-on-COVID-19-persists-in-Kenya-s-rural-areas-Te1cCee03m/index.html

Kilonzo, S.M na Omwalo, B.O. (2020). The politics of pulpit reliogiosity in the era of COVID-19 in Kenya. Ilisomwa: https://www.frontiersin.org/articles/10.3389/fcomm.2021.616288/full

Mghenyi, C. (7 May, 2020). Is Joho a hero or a villain in the fight against Covid-19? Ilisomwa: https://www.the- star.co.ke/news/big-read/2020-05-07-is-joho-a-hero-or-a-villain-in-the-fight-against-covid-19/

Mghenyi, C. (24 May, 2020). Mombasa slums flirt with Covid-19 explosion. Ilisomwa: https://www.the- star.co.ke/news/big- read/2020-05-24-mombasa-slums-flirt-with-covid-19-explosion/

Ministry of Health (2020). Frequently asked questions about Coronavirus (COVID-2019). Republic of Kenya.

Ozili, P.K na Arun, T. (2020) Spillover of COVID-19: Impact on the Global Economy. https://papers.ssrn.com/sol3/papers.cfm?abstract_id=3562570

Reliefweb (2020). Kenya Situation Report, 14 May 2020. Ilisomwa: https://reliefweb.int/report/kenya/kenya-situation-report-14-may-2020

Sacks, H., Schegloff, E.A., and Jefferson, G. (1974). A simplest systematics for the organization of turn-taking in conversation. Katika Language 50, 696-735.

Schmid, Wolf: "Skaz". In: Hühn, Peter et al. (eds.). The living handbook of narratology. Hamburg University. URL = http://www.lhn.unihamburg.de/article/skaz [Ilisomwa:12 Feb 2021]

Vidija, P. (2021). Facts or myths?: Demystifying Covid- 19. Ilisomwa https://www.standardmedia.co.ke/fact- check/article/2001416708/facts-or-myths-demystifying-covid-19

World Health Organization (2020). Advice for public myth usters. https://www.who.int/emergencies/diseases/novel- coronavirus- 2019/advice- for- public/myth- busters?gclid=EAIaIQobChMI_Z6t_8n2_AIVwuDtCh02WQ1HEAAYASACEgKq9fD_BwE

Tarehe ya Uchapishaji
13 February, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Rotich, A. (2024). Mitazamo ya Kiskaz Kuhusu Covid-19 Inavyojitokeza katika Lugha ya Wananchi Nchini Kenya. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 79-86. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1754