Athari za Mtagusano Kati ya Jamii na Ekolojia Katika Ushairi wa Mberia: Bara Jingine na Rangi ya Anga

  • John Mugwe Mwaniki Ntunene Girls High School
  • Rayya Timammy, PhD University of Nairobi
  • Mary Ndung'u University of Nairobi
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya yameangazia athari za mtagusano kati ya jamii na ekolojia katika diwani ya Bara Jingine na Rangi ya Anga. Ili kufaulisha hili, tumeongozwa na nadharia ya Ekolojia ambayo inaangazia mahusiano na mwingiliano kati ya jamii na mazingira inamoishi. Nadharia hii ya Ekolojia inahusishwa na Cheryll Glotfelty na Harold Fromm mwaka wa 1996. Malengo ya uchunguzi wetu ni kubainisha athari za mtagusano kati ya jamii na mazingira ya kiasili katika diwani ya Bara Jingine na Rangi ya Anga. Baada ya uchunguzi wetu tumebainisha kuwa wanajamii wanapotagusana na mazingira wanachangia katika uharibifu wa misitu, hewa, mito, mabwawa na udongo. Hali hii inaathiri mataifa husika kiuchumi kwani binadamu huishi katika mazingira haya. Isitoshe, mazingira haya huwa ndio makazi ya wanyama na viumbe vingine ambavyo huwa na wajibu mkubwa katika mchakato mzima wa ekolojia. Ili kubainisha haya tumechanganua data yetu kwa njia ya maelezo huku tukitoa ufafanuzi na thibitisho kutoka katika diwani ya Bara jingine na Rangi ya Anga.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.
Tarehe ya Uchapishaji
31 July, 2019
Jinsi ya Kunukuu
Mwaniki, J., Timammy, R., & Ndung’u, M. (2019). Athari za Mtagusano Kati ya Jamii na Ekolojia Katika Ushairi wa Mberia: Bara Jingine na Rangi ya Anga. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 1(1), 23-34. Retrieved from https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/17