Upambanuzi wa Mikakati ya Kitashtiti katika Vibonzo vya Kisiasa Vya Gado

  • Kerryann Wanjiku Mburu Laikipia University
  • Sheila Wandera-Simwa, PhD Laikipia University
  • Nabea Wendo, PhD Laikipia University
Keywords: Vibonzo vya Kisiasa, Tashtiti, Mikakati ya Kitashtiti, Mtandao
Sambaza Makala:

Ikisiri

Taalumu ya uchoraji na uchapishaji wa vibonzo vya kisiasa umekuwepo tangu karne ya kumi na nane. Saana hii huwavutia watafiti wengi kutokana na uwezo wake wa kusimba jumbe zisizoweza kusemwa wazi wazi. Ifahamike kuwa sifa kuu ya vibonzo vya kisiasa ni kuwa vinapaswa kuwa cheshi na vyenye tashtiti ndiposa viweze kuwasilisha masuala tata kwa njia ya kimzaha. Kutokana na hali hii, utafiti huu ulichunguza tashtiti katika vibonzo vya kisiasa vya Gado vilivyochapishwa katika mwaka wa 2017 kwenye tovuti yake. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kupambanua mikakati iliyotumika katika kuendeleza maudhui ya kitashtiti katika vibonzo vilivyoteuliwa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Semiotiki iliyoasisiwa na Ferdinand De Saussure, na baadaye kuhakikiwa na Chandler na pia Wamitila. Mihimili ya nadharia hii ilitumika kuchambua mikakati iliyotumiwa na Gado katika vibonzo vyake kwa minajili ya kuendeleza maudhui ya kitashtiti. Utafiti huu ni wa kimaelezo na ulifanyika mtandaoni, pale ambapo mtafiti alipekua tovuti ya Gado (www.gadocartoons.com) na kuteua kimaksudi vibonzo vinane kutokana na jumla ya vibonzo ishirini vilivyokuwa vimechapishwa katika mwaka wa 2017. Uteuzi huu ulijikita katika vibonzo vilivyofungamana na madhumuni ya utafiti huu. Kwa jumla, utafiti huu ulidhibitisha kuwa mwanakibonzo Gado alitumia mbinu za lugha kama vile; kinaya, kejeli, metonimia, sitiara, analojia na mwingiliano matini kama mikakati ya kuibua kitashtiti katika vibonzo vyake. Vilevile, utafiti huu ulionyesha kuwa Gado alitumia ishara kama vile; matumizi ya rangi mbalimbali, pamoja na alama kama vile; heshtegi, mviringo na nyota kama mikakati ya kuibua tashtiti katika vibonzo vyake. Mwishowe, utafiti huu ulidhibitisha kuwa vibonzo vilivyochapishwa kwenye mtandao, vilidhihirisha uhuru na ukali mwingi katika usawiri wa masuala mbalimbali, jambo ambalo lilisaidia katika kufanikisha lengo kuu la tashtiti; ambalo ni ushambulizi unaochochea mabadiliko. Mwishowe, matokeo ya utafiti huu yalitarajiwa kuwanufaisha wanamawasiliano, wanasemiotiki na wasomi wa masuala ya kisiasa kwa kuwapa mtazamo mpya kuhusiana na matumizi ya maneno na ishara katika kusimba jumbe tata zinazochapishwa kwenye mtandao ambapo kuna uhuru mwingi wa kuelezea masuala tata bila kudhibitiwa.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Al-Momani, K., Badarneh, M. A., & Migdadi, F. (2017). A semiotic analysis of political cartoons in Jordan in light of the Arab Spring. HUMOR, 30(1). https://doi.org/10.1515/humor-2016-0033

Ayodi, N. K., Beja, S. K., & Ogola, J. O. (2014). Tashtiti na Wanatashtiti: Maana, Umuhimu na Vipengele vyake katika Fasihi. Mulika, 33, 46– 57. https://doi.org/https://journals.udsm.ac.tz/index.php/mj/article/view/1535

Barasa la Kiswahili la Zanzibar. (2010). Kamusi La kiswahili fasaha. Oxford University Press.

Brewer, C. A. (1994). Color use guidelines for mapping. Visualization in modern cartography, 1994(123-148), 7

Chandler, D. (2002) Semiotics for Beginners. Aberystwyth: Aberystwyth University

Condren, C. (2023). Between laughter and satire aspects of the historical study of humour. Springer International Publishing.

Declercq, D. (2018). A definition of satire (and why a definition matters). The Journal of Aesthetics and Art Criticism, 76(3), 319–330. https://doi.org/10.1111/jaac.12563

Dörner, A., & Porzelt, B. (2016). Politisches Gelächter. Rahmen, Rahmungen und Rollen bei Auftritten politischer Akteure in satirischen Interviews desdeutschen Fernsehens. M&K Medien & Kommunikationswissenschaft, 64(3), 339-358.

Eko, L. (2015). The art of satirical deterritorialization: Shifting cartoons from real space to cyberspace in Sub-Saharan africa. International Communication Gazette, 77(3), 248– 266. https://doi.org/10.1177/1748048514568759

Gamen, I. (2022, March 16). Metonimia Ya Kuona ni Nini? Creativos Online. https://www.creativosonline.org/sw/Visual-metonymy.html

Griffin, D. (2015). Satire a critical reintroduction. The University Press of Kentucky.

Kahigi, K. K. (2020). Sitiari katika Kichomi – Uchambuzi wa Mojawapo ya Mbinu za Kifasihi ya Euphrase Kezilahabi. Swahili Forum, 27, 32–56.

Kondowe, W., Fishani Ngwira, F., & Madula, P. (2014). Linguistic Analysis of Malawi Political Newspaper Cartoonson President Joyce Banda: Towards Grice’s Conversational Implicature. International Journal of Humanities and Social Science, 4(7), 40-51.

Knight, C. A. (2004). The literature of Satire. Cambridge University Press.

Lichtenstein, D., & Nitsch, C. (2022). Content analysis in the research field of satire. Standardisierte Inhaltsanalyse in Der Kommunikationswissenschaft – Standardized Content Analysis in Communication Research, 277– 286. https://doi.org/10.1007/978-3-658-36179-2_24

Mbatiah, M. (2001). Kamusi Ya Fasihi. Standard Textbooks Graphics and Pub.

Muchiri, M. (2017, March 9). Shock as Uhuru calls politician ‘Shetani Mshenzi’ in public [video]. Kenyans.co.ke. from http://www.Kenyans.co.ke/news/president-Uhuru-Kenyatta-bitter-exchange-words-turkana-governor-josphat-nanok-17370

Mulanda, O., & Telewa, V. K. (2014). In the Cartoonist’s Mind: Exploring Political Comic Strips in Kenyan Daily Newspapers. The Journal of Pan African Studies, Vol.6, No.9, May 2014, 6(9), 30–40.

Mwetulundila, R., & Kangira, J. (2015). An Analysis of Rhetoric and Humour in Dudley’s Political Cartoons Published in the Namibian Newspaper in 2012. International Journal of Research in Humanities and Social Sciences, 2(6), 63–75. https://doi.org/ ISSN 2394-6296 (Online)

Ng'etich, K. K. (2020). The Power of Satire: an analysis of Gado’s Cartoons in The Standard newspapers (Unpublished master's dissertation). Aga Khan University, East Africa.

Peifer, J., & Lee, T. (2019). Satire and journalism. Oxford Research Encyclopedia of Communication. https://doi.org/10.1093/acrefore/9780190228613.013.871

Salisu Ogbo, U., & Nuhu, M. (2016). Satire as tool of political cartoons in the Nigerian National Dailies: A Critical Discourse Analysis. European Scientific Journal, ESJ, 12(29), 124. https://doi.org/10.19044/esj.2016.v12n29p124

Sani, I. (2014) ‘The use of verbal and visual metaphors in the construction of satire in Nigerian political cartoons’, Online Journal of Communication and Media Technologies, 4(2). doi:10.29333/ojcmt/2471.

Sani, I., Abdullah, M.H., Ali, A.M & Abdullah, F.S. (2012). The role of humour in the construction of Satire in Nigerian political cartoons. Online journal of communication and media technologies,2(3), 148-153.

Stinson, E. (2019). Satire. Oxford Research Encyclopedia of Literature. https://doi.org/10.1093/acrefore/9780190201098.013.1091

Wamitila, K.W. (2002). Uhakiki wa Fasihi: Misingi na Vipengele Vyake. Nairobi: Phoenix Publishers

Tarehe ya Uchapishaji
8 January, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Mburu, K., Wandera-Simwa, S., & Wendo, N. (2024). Upambanuzi wa Mikakati ya Kitashtiti katika Vibonzo vya Kisiasa Vya Gado. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 11-27. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1685