Mwathiriano Kati ya Watunzi wa Riwaya ya Kiswahili: Mwangwi wa Maudhui ya Mafuta (2008) katika Cheche za Moto (2008)

  • Felix Musyoka Kalingwa Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Titus Musyoka Kaui, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Athari, Mwingiliano, Matini, Watunzi, Riwaya
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inashughulikia athari za Katama Mkangi kwa John Habwe kwa kujikita katika riwaya teule za Kiswahili za Mafuta (1984) na Cheche za Moto (2008). Utanzu wa riwaya ya Kiswahili umeendelea kupanuka kimaudhui na kifani kutokana na juhudi za watunzi mbalimbali kama vile Katama Mkangi na John Habwe. Japo tafiti za awali zimetafitia suala la mwingiliano matini, tafiti nyingi zimejikita katika kazi za mtunzi mmoja. Utafiti wa kina ulihitajika kuchunguza namna utunzi wa Mafuta (1984) ulivyoathiri John Habwe alipoitunga riwaya yake ya Cheche za Moto (2008). Katama Mkangi aliandika riwaya ya Mafuta katika wakati wa chama kimoja cha kisiasa ambapo uhuru wa kujieleza ulikuwa umebanwa sana. Habwe ameandika kazi yake katika mazingira yaleyale lakini katika kipindi ambapo uhuru wa kujieleza umepanuliwa. Kwa hivyo, amekwepa mtindo wa kimajazi alioutumia Mkangi na kuyaangazia masuala anayoyaibua kwa njia wazi. Makala hii ililenga kuonyesha kuwa maudhui katika riwaya ya Cheche za Moto ni mwangwi unaotokana na riwaya ya Mafuta (1984). Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya mwingiliano matini iliyoasisiwa na Julia Kristeva (1969). Mihimili mikuu ya nadharia hii iliyoongoza utafiti huu ni pamoja na: hakuna matini ya fasihi yenye sifa za pekee, matini hubainisha sifa mbalimbali za matini tangulizi, na mwisho, matini ya baadaye huweza kufafanua dhana fulani kutoka matini tangulizi kwa njia inayoeleweka.  Nadharia hii ya mwingiliano matini ilisaidia pakubwa kuonyesha namna kazi ya awali, Mafuta (1984) ilivyomwathiri John Habwe katika utunzi wa Cheche za Moto (2008) kimaudhui. Riwaya teule ziliteuliwa kimakusudi ili kupata sampuli faafu yenye data ya kujaza pengo la utafiti. Data ilikusanywa kupitia kwa usomaji wa maktabani na vilevile kusakura mitandaoni kuhusu vipengele vya mwingiliano matini katika riwaya ya Kiswahili. Data hii imewasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Utafiti wa makala hii unatarajiwa kutoa mchango katika uhakiki wa utanzu wa riwaya ya Kiswahili, hususan kuhusu kipengele cha kuathiriana baina ya watunzi wa riwaya za Kiswahili

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

BAKITA (2015). Kamusi kuu ya Kiswahili. Dar es Salaam.Longhorn Publishers.

Clayton, J. & Rotherstein, E. (1991). Figures in the Corpus:Theories of Influence and Intertexuality. Madison, Wisconsin:University of Winconsin Press Uk 3-35

Chacha, N. C. (1980) Ushairi wa Abdilatif Abdalla. Nairobi. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Nairobi (Haijachapishwa)

Fakih, S. J. (2017). Kutathmini Mabadiliko ya Usawiri wa Mwanamke katika Riwaya ya Utengano na Kamwe si Mbali Tena. Tasnifu ya M.A (isiyochapishwa). Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Habwe, J. (2008). Cheche za Moto. Nairobi.Jomo Kenyatta Foundation.

Kaui T. M (2008). Usawiri wa Vijana katika Tamthilia Teule za Kiswahili. Chuo Kikuu cha Kenyatta

Kilonzo (2012) . Ujitambuzi na Utambulisho wa Kijinsia katika Riwaya ya Maisha Kitendawili. Chuo Kikuu cha Nairobi

Kimwea (2019). Taswira ya Jamii katika Riwaya ya Yasinya na Mwanaisha. Chuo Kikuu cha Nairobi.

Kristeva, J. (1969). Desire in Language: Asemiotic Approach to Literature and Art.New York.Colombia University Press.

Maitaria, J. N (2014). Dhima ya Ushairi wa Kiswahili katika Kuelimisha Jamii kuhusu Demokrasia. Kiswahili Juzuu 77.

Mishra, R.K (2012). ‘A Study of Intertextuality: The Way of Reading and Writing.’ Katika Prime Journals. http://primejournal.org/PRE/pdf/11/10/2023

Mkangi, K. (1984). Mafuta. Nairobi.Heinamann Educational Books

Mwongela (2021) . Usimulizi katika Riwaya ya Trilojia ya Kiswahili: Mfano wa Siri Sirini.

Nabangi, J.K (2013). Athari za Utenzi katika Uandishi wa Riwaya Teule ya Kiswahili: Tasnifu ya uzamili(isiyochapishwa). Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Njogu, K(1997). Uhakiki wa Riwaya za Visiwani Zanzibar. Nairobi: Nairobi University Press.

Oketch, S., Ambuyo, B., & Makokha, R. (2020). Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili. East African Journal of Swahili Studies, 2(1), 8-18. https://doi.org/10.37284/eajss.2.1.135.

Omoga, R. G (2018). Mwananchi kama mdhulumu wa Maslahi yake katika Tamthilia za Kilio cha Haki, Amezidi na Mstahiki Meya. Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa)

Shemwata (2021). Itikadi katika Tamthilia ya Emmanuel Mbogo: Utafiti (isiyochapishwa) Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Wafula & Mue (2021). Uchanganuzi wa Riwaya ya Kiza katika Nuru ya Said Ahmed Mohammed kwa Misingi ya Umarxi mpya wa Kifreire. Swahili Forum 28: 34-45

Wafula P.K (2015). Mwingilianomatini katika Cheche za Moto na Kidagaa Kimemwozea. Chuo Kikuu cha Kenyatta

Wamitila, K. (2003). Kamusi ya Fasihi, Istilahi na Nadharia. Nairobi.Focus Publishers

Wamitila, K. (2006). Uhakiki wa Fasihi: Misingi ya vipengele vyake.Nairobi.Phoenix Publishers Limited

Wamitila, K. (2008). Misingi ya Uchambuzi wa Fasihi. Nairobi.Vide-Muwa Publishers

Tarehe ya Uchapishaji
18 October, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Kalingwa, F., & Kaui, T. (2023). Mwathiriano Kati ya Watunzi wa Riwaya ya Kiswahili: Mwangwi wa Maudhui ya Mafuta (2008) katika Cheche za Moto (2008). Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 394-402. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1524