Dhima za Tasifida Kimuktadha katika Nyimbo za Singeli: Mifano kutoka kwa Msanii Msaga Sumu na Manfongo

  • Baraka Sikuomba Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  • Lina Godfrey Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Keywords: Tasifida, Singeli na Muktadha
Sambaza Makala:

Ikisiri

Kutokana na ufinyu wa tafiti zilizofanyika kuhusu tasifida katika muktadha wa nyimbo za singeli kumejengeka mtazamo hasi hasa kwenye lugha inayotumika katika muktadha wa nyimbo za singeli miongoni mwa wanajamii. Kutokana na umuhimu wa tasifida katika kuendeleza utamaduni wa jamii kulikuwa na haja ya kuchunguza na kuweka bayana dhima za matumizi ya tasifida katika nyimbo za singeli. Kwa hiyo, makala hii imeangalia dhima za tasifida kimuktadha katika nyimbo za singeli kwa kutumia nyimbo ziitwazo “Siponaye”, “Dada Asha”, “Spesho”, “Mtoto Mdogo” za msanii  Msaga Sumu na  “Chawa”, “Hainogi”, “Kitasa”, “Mashine” “Kipusa”, “Muacheni Adange” za msanii Manfongo. Nadharia ya Semiotiki imetumika kufafanua dhima za tasifida katika nyimbo za wasanii teule. Katika nyimbo hizo tasifida mbalimbali zimetumiwa na wasanii teule kuwasilisha maudhui yao. Nyimbo hizi za singeli, licha ya kuimbwa kwa lugha inayoonekana ni ya mtaani, zimezingatia sana matumizi ya tasifida katika kupunguza ukali wa maneno. Matokeo ya utafiti huu yameonesha wazi kuwa matumizi ya lugha ya tasifida katika nyimbo za singeli, yameonesha wazi kwamba nyimbo za singeli zina dhima kadha wa kadha zinazowasilishwa kwa njia ya matumizi ya tasifida. Kupitia matumizi ya tasifida katika nyimbo za singeli, ni bayana kwamba tasifida zina dhima za msingi katika nyimbo za singeli katika kuendeleza mila, utamaduni na desturi za mawasiliano katika jamii. Dhima hizo ni pamoja na kubainisha kazi zisizo halali katika jamii, kuibua tabia zisizokubarika katika jamii, kukemea mmomonyoko wa maadili katika jamii, kuhimiza umuhimu wa mapenzi ya dhati katika jamii na kuweka bayana uhalisia wa mwanaume. Hivyo basi, watafiti wengine wanaweza kufanya utafiti kama huu kwa kuchunguza kwa kina tofauti ya tasifida na taswira kimuktadha katika nyimbo teule za utafiti huu

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Babbie, E. (1999). The Basics of Social Research. Belmont: Wadsworth Publishing Company.

Barthes, R. (1994). The Semiotic Challenge. Barkeley and Los Angles: University of California Press.

Blonsky, M. (1991). On Signs. Baltimore: The Johns Hopkins University Press.

Bradley, W.G. (1978) Self- Serving Biases in The Attribution process: A Reexamination of The Fact of Fiction Question. Journal of Personality and Social Psychology, 36, 56-7.

Calvo, J.J. (2005) The Language of Sex: Saying and Not Saying. Valencia: De la Universitat de Valencia, Ist Edition.

Chandler, D. (2002). Semiotics for Beginners. Aberystwyth: Aberystwyth University.

Chapman, G. (2008). Deserate Marriages. Moving Toward Hope and Healing in Your Relationship. Chicago: Northfield Publishing.

Charles, Z. (2008). Introduction to Social Work and Social Welfare. U. S. A.:Thomson Brooks/Cole.

De Saussure, F. (1996). A Course of General Linguistics. New York: McGraw-Hill.

Earp, B. D. (2021). The Ordinary Concept of True Love. Oxford: Oxford University Press, in Press.

Fakih, S. J. (2017). Kutathimini Mabadiliko ya Usawiri wa Mwanamke katika Riwaya ya Utengano na Kamwe Si Mbali Tena. [Tasinifu ya Uzamili, haijachapishwa. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania].

Jabir, S. (Mtayarishaji) (2015) “Mkasi, S13E05 with Msagasumu” Inapatikana katika https://youtube.be//21QX9ljuc.

Khatibu, M. S. (1986). Tamathali za Semi za Kiswahili. Mulika, Juz. 18: 1-15.

Lanking (Mtayarishaji) (2019) “Anapoishi Manfong”. Inapatikana katika youtube https://youtube.be/fOUxszd4T1.

Masath, F. B. (2013). Moral Deterioration: The Reflection on Emerging Sreet Youth Gangs in Musoma, Tanzania. Academic Research International, 49(1), 101-111.

Mohammed, K. I. (2018). Kuchunguza Usawiri wa Muhusika Mwanamme katika Riwaya ya Kiswahili: Joka la Mdimu na Watoto wa Mama Nt`iliye. [Tasinifu ya Uzamili, haijachapishwa. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania].

Mwanisenga, R. (2017). Wasiposhtuka Singeli Watajiua Wenyewe. https://mtanzania.co.tz//wasiposhtuka-singeli-watajiua-wenyewe/? fbclid=IwAR2ntPjsvCf44MThdT87RJAoJgs76_hSkfJA_BkGfe1lzrjxscZqHr550ll.

Ndugo, C.M. (2006). Uwiano wa Picha na Matini katika Mango ya Matangazo wa Kisemiotiki. [Tasinifu ya Umahili, haijachapishwa. Chuo Kikuu cha Kenyatta].

Pierce, C. (1977). Semiotics and Signific: The Correspondence between Charles. S. Pierce and Lady Victoria Welby. Indiana: Indiana University Press.

Possi, M. K. (1996). “Effects of Grug Abuse on Cognitive and Social Behaviours: A potential Problem Among Youth in Tanzania”. UTAFITI (New Series), 3(1): 111-128.

Silavwe, M. I. (2016). Mtindo katika Riwaya ya Marimba ya Majaliwa na Edwini Semzaba. [Tasinifu ya Uzamili, haaijachapishwa. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania].

Wasike, W. W. (2020) “Mwanamke wa Kisasa katika Insha za Kifasihi Magazetini: Mtazamo wa Nadharia ya Upalizi”. Mulika, Na. 38, 87-104.

Yangi, E. (2015). Matumizi ya Tamathali za Semi katika Nyimbo za Misiba kwa Jamii ya Wahehe. [Tasinifu ya Uzamili, haijachapishwa. Chuo Kikuu cha Dodoma].

Zahoro, S. (2018). Vionjo vya Fasihi ya Kisasa ya Kiswahili katika Nyimbo za Singeli. [Tasnifu ya Uzamili, haijachapishwa. Chuo Kikuu cha Dodoma].

Tarehe ya Uchapishaji
27 September, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Sikuomba, B., & Godfrey, L. (2023). Dhima za Tasifida Kimuktadha katika Nyimbo za Singeli: Mifano kutoka kwa Msanii Msaga Sumu na Manfongo. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 382-393. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1470