Mbinu Za Lugha Katika Nyimbo Teule Za Mapenzi Kwenye Kipindi Cha Mambo Mseto Cha Redio Citizen
Ikisiri
Utafiti huu ulichunguza mbinu za lugha katika nyimbo za mapenzi kwenye kipindi cha Mambo mseto cha Redio Citizen. Nadharia iliyotumika ni Nadharia ya mtindo iliyoasisiwa na Buffon (1930) na kuendelezwa na watafiti wengine. Muundo uliotumika ni mkabala mseto kuegemea muundo wa QUAL-quan. Sampuli za maksudi zilitumika kukiteua kipindi cha Mambo mseto na wanafunzi wa chuo kikuu cha kikatoliki cha Afrika Mashariki. Wanafunzi 83 kutoka chuo kikuu cha Kikatoliki cha Afrika mashariki walifanyiwa utafiti. Nyimbo saba kuashiria asilimia 30 kutoka jumla ya nyimbo ishirini na nne za mapenzi zilizochezwa ziliteuliwa. Uteuzi wa nyimbo hizo saba uliongozwa na maoni ya Fink (2003) anayesema kuwa, kwa watafitiwa chini ya 1000, jumla ya asilimia 30 ya usampulishaji hutumika. Hivyo katika utafiti huu, mtafiti alichukua ailimia 30 ya nyimbo 24 alizosikiza akapata nyimbo saba. Matokeo ya utafiti yalibaini kuwa mbinu za lugha zinazodhihirika katika nyimbo za mapenzi zilizochunguzwa ni kuchanganya ndimi, takrikiri, Chuku, tasfida, sitiari na tashbihi. Utafiti huu ulipendekeza watunzi wa nyimbo za mapenzi watumie pia mbinu nyingine za lugha kama vile methali ambayo haikujitokeza sana. Watafiti wengine pia wafanye utafiti kuhusu mbinu za lugha kwenye aina nyingine za nyimbo. Utafiti huu utakuwa wa manufaa kwa vyombo vya habari haswa stesheni za redio ili wafahamu mchango wao kwa ujenzi wa lugha ya Kiswahili kwani wao ndio husambaza na kucheza nyimbo hizi za mapenzi. Vilevile utafiti huu utakuwa na mchango katika kuleta ushirikiano mzuri wa kiakademia katika jumuiya ya Afrika mashariki kwa vile ilitafiti nyimbo kutoka Kenya, Uganda na Tanzania
Upakuaji
Marejeleo
Aga Khan, (2023). Report on survey on millennials & digital natives’ consumption habits and the implications for legacy media in east Africa Radio Brands Consumed by the Millennials and Gen Zs. Radio Brands Consumed and Relied on for News Offline
Barry, P. (2002) Beginning Theory: An introduction to literary and cultural Theory. Manchester university press.
Bhatia, T. K. (2001). Language mixing in global advertising. The Three Circles of English, 4, 195–215.
Buffon, G. (1930). Buffon’s Discourse on style. Paris Librairie : Hatier publishers.
Coombes, H. (1953). Literature and criticism. Harmondsworth: Penguin.
Fink, A. (2003). How to sample in Surtveys (Vol. 7. Sage)
Kangogo, E. (2013). Nafasi ya mwanamke: Jinsi inavyotetewa katika nyimbo za taarab. Utafiti wa chuo kikuu cha Nairobi
Katutu, R.M. (2013). Mtindo katika diwani ya mfuko mtupu na hadithi nyingine. Tasnifu ya chuo kikuu cha Nairobi.
Matara, V. (2020). Top 10 Most popular Radio shows in Kenya; Victoriamatara.com.
Leech, G. (1969). A Linguistic Guide to Modern English Poetry.Essex: Longman Group Ltd.
Mburu, J. M. (2014). Fani Katika Nyimbo Teule za Anastacia Mukabwa (Doctoral dissertation, University of Nairobi).
Mkonda, J. J. (2015) Taswira katika fungate ya uhuru na wasakatonge. Tasnifu ya Chuo kikuu cha Dodoma
Mrikaria, S. (2007). Fasihi simulizi na Teknolojia mpya. Swahili forum
Msokile, M. (1992) Misingi ya Hadithi Fupi. Dare es Salaam University Press.
Ndumbu, J. M. (2013). Matumizi ya takriri na sitiari katika utenzi wa rasi’lghuli (Doctoral dissertation, University of Nairobi,).
Njogu, K, & Chimerah, R. (1999). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na mbinu. Nairobi http://www.coursehero.com
Nyandiwa, H. (2015). Uchanganuzi wa kimtindo wa Zinguo na Mbaya wetu. Tasnifu ya Chuo kikuu cha Nairobi
Ransom, Patricia Fox (2015). Message in the Music: Do Lyrics Influence Well-Being? Master of Applied Positive Psychology (MAPP) Capstone Projects. 94. https://repository.upenn.edu/mapp_capstone/94
Redio free Afrika (2009) Ni kwa nini muziki ama nyimbo zenye ala na ujumbe wa kimapenzi unapendwa Zaidi kuliko nyimbo nyingine? . https://www.radiofreeafrica.co.tz
Shonko. D. (2012). Mbinu za lugha ya Kiswahili. Blogu ya Kiswahili. Swahili Hub
Simpson. P. (2004). Stylistics. A resource book for students, London Routledge.
TutorKE.com (2023). Online learning in Kenya.
Wamitila, K. W. (2003). Kichocheo cha Fasihi: Simulizi na Andishi.Toleo la pili. Phoenix publishers: Nairobi
Copyright (c) 2023 Lydia Chelagat, Rebecca Wanjiku-Omollo, PhD, Margan Adero

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.