Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Ikisiri
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika kuwasilisha maudhui ya kidini, sera za matumizi ya lugha, na athari ya matumizi ya lugha ya Kiswahili katika kuwasilisha ujumbe wa kidini. Nadharia ya umilisi mawasiliano yake Dell Hymes (1966) iliongoza utafiti. Data ilikusanywa kwa kutumia hojaji, mahojiano na uchunzaji. Wanafunzi thelathini wa kidato cha nne, viongozi kumi wa kidini wa wanafunzi na kasisi mmoja wa shule walihusishwa katika ukusanyaji wa data. Matokeo yalibaini kuwa sera ya lugha katika shule ya wasichana ya Itigo ilipendelea matumizi ya Kingereza kama lugha ya mawasiliano. Wanafunzi walisema kuwa lugha ya Kiswahili inapotumika katika mahubiri, ujumbe hueleweka zaidi. Vilevile, ilidhihirika kuwa viongozi wa kidini wa wanafunzi hutumia lugha ya Kiswahili kuwasiliana katika mikutano yao lakini wao huandika kumbukumbu kwa lugha ya Kiingereza. Isitoshe, ilibainika kuwa lugha anayoitumia zaidi kasisi wa shule katika mahubiri yake ni Kiingereza. Licha ya uwezo wa Kiswahili katika kufanikisha mawasiliano kuhusu maswala ya kidini shuleni, Kiingereza ndicho hutumika zaidi. Kunahitajika mabadiliko katika sera ya lugha shuleni ili kuipa lugha ya Kiswahili nafasi zaidi katika mawasiliano ya kidini
Upakuaji
Marejeleo
Davis, S.C (1976). Basic Principals of Functional Grammar in Syntax and Semantics, Volume 13. New York: Academic Press
Hymes, D. (1972). Models for the interaction of language and social life. In J. J. Gumperz & D.H. Hymes (Eds.), Directions in sociolinguistics: The ethnography of communication (pp. 35–71). New York: Holt, Rinehart and Winston.
Kipchirchir, M. (2019). Matumizi ya Vifaa vya Kisasa katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa Sarufi katika shule za Upili zilizoko kaunti ndogo ya Moiben, Uasin Gishu. Tasnifu ya Uzamili. Chuo kikuu cha Kibabii.
Kothari, C (1993). Research Methodology, Methods, and Techniques. New Delhi: Wiley Eastern Limited.
Massamba na Wenzake (2001). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam: TUKI.
Misiko, D (2008). Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano Rasmi Nchini Kenya: Uchunguzi kifani wa Wilaya ya Uasin Gishu. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Moi.
Mugenda, O., & Mugenda, A. (2003). Research Methods, Qualitative & Quantitive Approaches. Nairobi: ACTS Press.
Musau, M (2001). The Spread of Kiswahili in Kenya in the New Millenium: Prospects and Challenges. Dar es Salaam: TUKI.
Mbaabu, I (1978). Kiswahili Lugha ya Taifa. Nairobi: Kenya Literature Bureau.
Oduori, R (2002). Dhima ya Kiswahili katika Maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Eldoret: Moi University Press.
Osore, K (2002). The Role of Language in Scientific and Technological Development: The case of Kiswahili Language in East Africa. Hammanskraal University: Pretoria.
Onen, D. (2005). A General Guide to Research Proposal and Report. Oxford: Oxford University Press.
Sharman, D. (1983). Research Methods in Social Science. New Delhi: Sterling Publishers.
Copyright (c) 2023 Joachim Kipchirchir Melly, Ernest Sangai Mohochi, PhD

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.