Tamthilia ya Kiswahili katika Ukuaji na Ustawi Endelevu wa Ujasiriamali Nchini Tanzania: Uchunguzi wa Tamthilia ya Safari ya Chinga (2009) ya Shani Omari

  • Furaha Jumapili Masatu Chuo Kikuu cha Dodoma
Keywords: Ujasiriamali, Mjasiriamali, Safari ya Chinga, Dola, Tamthilia ya Kiada
Sambaza Makala:

Ikisiri

Ujasiriamali ni wimbo unaozidi kurindima masikioni mwa wanajamii. Wimbo huu unatokana na changamoto ya fursa funge za ajira miongoni mwa vijana. Tatizo linaonekana kuwa kubwa kwa sababu vijana wengi hawaonekani kuwa na msukumo wa ndani na wa kimazingira wa kujiajiri. Vijana wengi bado wanaamini katika kuajiriwa badala ya kujiajiri ilhali fursa za ajira rasmi wazitakazo ni chache kuliko idadi yao. Serikali na wadau wa maendeleo, wanazidi kukuna vichwa kutafuta ufumbuzi wa changamoto hii ya ajira miongoni mwa vijana. Mojawapo ya mapendekezo ya kutatua changamoto hii, ni kwa serikali na wadau kuwawezesha vijana kujikomboa kifikra kupitia elimu na mazingira rafiki kwa ujasiriamali. Baadhi ya wadau, wanaamini elimu rasmi ya ujasiriamali katika shule ya msingi na sekondari ndiyo suluhu kwa vijana kufikiria kujiajiri. Hata hivyo, kuna hoja kuwa wadau wa elimu wamechelewa sana kuiteua tamthilia ya Safari ya Chinga (2009) ya Shani Omari kuwa tamthilia ya kiada miongoni mwa tamthilia rasmi zinazopaswa kufundishia na kujifunza uhakiki wa fasihi na ujasiriamali katika ngazi ya sekondari na vyuo. Hivyo, makala haya yanawasilisha sehemu ya matokeo ya uchunguzi tulioufanya kuhusiana na maudhui ya tamthilia ya Safari ya Chinga ili kuonesha nafasi adhimu ya Tamthilia ya Kiswahili katika ukuaji na ustawi endelevu wa ujasiriamali nchini Tanzania.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Bible Society of Tanzania. (1997). Maandiko matakatifu ya Mungu yaitwayo BIBLIA. Nairobi: Africa Area Typesetting Unit.

Drucker, P. F. (2002). Innovation and entrepreneurship: Practice and discipline (Adobe Acrobat E-Book Reader edition v 1). Toronto, Canada; London, UK: HarperCollins Publishers Ltd.

Hilrisch, R. D., & Peters, M. P. (1992). Entrepreneurship: Starting, developing and managing a new enterprise (2nd Edition). Boston: Irwin Homewood.

Independent Commission of the South on Development Issues. (1992). The challenge to the south: The report of the South Commission. Oxford University Press.

International Labour Organisation. (2022). World employment and social outlook: Trends 2022. Geneva: International Labour Office.

International Organization for Migration. (2023). World migration report 2022. https://publications.iom.int/system/files/pdf/wmr_2023.pdf.

Ismail, B. (Jumatano, Oktoba 12, 2022). Makinda awataka vijana kujitafutia ajira wenyewe. Katika Mwananchi.

Kuratko, D. F. & Hodgetts, R. M. (2005). Entrepreneurship: Theory, process, practice (6th Edition). Thomson South – West.

Masatu, F. J. (2011). Ufundishaji wa Nadharia za Uhakiki wa Fasihi ya Kiswahili katika Tanzania. Tasnifu ya Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dodoma. Haijachapishwa.

Matakala, P. & Kwesinga, F. (2001). Community needs and demands and their actual involvement in forest management. Katika Stisen Müller, B., S. na wenzake (Wah.), Proceedings from the Danida DANCED workshop on sustainable forest management in Southern Africa, Windhoek, Namibia.

Mbhele, T. P. (2012). The study of venture capital finance and investment behaviour in small and medium-sized enterprises. SAJEMS NS 15 (1). 94 – 111.

Ministry of Finance and Planning. (2021). National five-year development plan 2021/22-2025/26: Realising competitiveness and industrialisation for human development. ___

MoSHE. (2019). Entrepreneurship. Addis Ababa: _____

Nyerere, J. K. (1973). Uhuru na maendeleo. Oxford: Oxford University Press.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu. (2020). 2019 Tanzania kitarakimu. https://www.nbs.go.tz/nbs/takwimu/refrences/Tanzania_in_Figures_2019.pdf.

Omari, S. (2009). Safari ya Chinga. Dar es salaam: TUKI.

Satpayeva, Z., Kangalakova, D., Ibraimova, S., & Utemissova, G. (2022). The Science Impact on Country’s Socio-Economic Development. Eurasian Journal of Economic and Business Studies, 3(65), 27-46. https://doi.org/10.47703/ejebs.v3i65.142.

Steil, B., Victor, D. G., & Nelson, R. R. (2002). Technological innovation and economic perfomance. Oxford: Princeton University Press.

Stokes, D. (1998). Small business management (3rd Edition). London: Continuum.

Tanzania Urbanisation Laboratory. (2019). Harnessing urbanisation for development: roadmap for tanzania’s urban development policy. paper for the coalition for urban transitions. London and Washington DC. http://newclimateeconomy.net/content/cities-working-papers.

United Nations Department of Economic and Social Affairs, Population Division. (2022). World population prospects 2022: Summary of results. UN DESA/POP/2022/TR/NO. 3.

Tarehe ya Uchapishaji
18 August, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Masatu, F. (2023). Tamthilia ya Kiswahili katika Ukuaji na Ustawi Endelevu wa Ujasiriamali Nchini Tanzania: Uchunguzi wa Tamthilia ya Safari ya Chinga (2009) ya Shani Omari. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 274-288. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1377