Kuchambua Mbinu za Kiaristotle na Zisizo za Kiaristotle katika Tamthiliya ya Sadaka ya John Okello
Ikisiri
Uandishi wa tamthiliya kwa mwega wa Kiaristotle umekuwa na athari kubwa sana kwa waandishi wa Kiafrika. Katika fasihi ya Kiswahili, baadhi ya waandishi wa mwanzo walioathiriwa na mkabala huo ni Ebrahim Hussein na Penina Mlama (Wafula na wenzake, 2020). Makala haya yanachambua mbinu za Kiaristotle na zisizo za Kiaristotle katika tamthiliya ya Sadaka ya John Okello (Mbogo, 2015). Mbinu ya usomaji makini ndiyo imetumiwa kukusanya data. Data zimewasilishwa kwa Mkabala wa Kimaelezo. Ukusanyaji, uchambuzi na mjadala katika makala haya umeongozwa na Nadharia ya Kiaristotle. Kimsingi, Emmanuel Mbogo, mtunzi teule ametumia mbinu za Kiaristotle na zisizo za Kiaristotle katika tamthiliya ya Sadaka ya John Okello (2015). Mbinu za Kiaristotle zimejidhihirisha kupitia vipengele vya msuko, wahusika, lugha za kishairi, uteuzi wa misamiati, na dhamira. Mbinu zisizo za Kiaristotle zimejidhihirisha kupitia mbinu za monolojia, kuchanganya nathari na ushairi, pamoja na dayalojia. Makala haya yanaeleza kuwa tamthiliya ya Sadaka ya John Okello ni drama tanzia. Drama hii imebeba sifa nyingi za Kiaristotle na sifa chache zisizo za Kiaristotle. Mhusika mkuu John Okello amepitia mambo mazito na magumu ambayo mtu yeyote akikutana na kazi hii lazima ahisi huzuni moyoni mwake na amwonee mhusika huyu huruma kwa mateso na malipo mabaya aliyoyapata. Kutokana na mikondo mbalimbali ambayo drama tanzia inapitia si lazima tena shujaa au mhusika mkuu atoke familia ya tabaka la juu au tabaka tawala. Mhusika mkuu sasa anaweza kutoka tabaka lolote katika jamii yoyote.
Upakuaji
Marejeleo
Aristotle, N. (1965). Introduction to Aristotle (1965-02-01). Mc Graw - Hill Education.
Awhida, H. H. H. (2021). Matumizi ya Lugha katika Tamthiliya ya Sadaka ya John Okello. Journal of Human Sciences 20 (1).
BAKITA (2022). Kamusi Kuu ya Kiswahili (Toleo la 3). Dar es Salaam: Longhorn Publishers Plc. Tanzania
Bikorimana, D. (2020). Uhakiki wa Fasihi. https://www.academia.edu/41870699/UHAKIKI_WA_FASIHI_1_.
Bosibori, B. T. (2016). Mwingilianomatini katika Mkaguzi Mkuu wa Serikali na Mstahiki Meya. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Nairobi.
Njogu, K., & Chimerah, R. (1999). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu. Nairobi: Autolitho Ltd.
Clemence, S. M. (2015). Kuchunguza Mbinu za Tanzia za Kiaristotle katika Tamthiliya za Fumo Liyongo na Sundiata. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Hunt, F. (2021). Michango 10 ya Aristotle kwa Sayansi na Utamaduni (https://sw.warbletoncouncil.org/aportaciones-aristoteles-15015) .
Hussein, E. (1983). Hatua Mbalimbali za Kubuni na Kutunga Testo Teatrale Kufuatana na Misingi ya Kiaristotle (Uk. 197 – 205). Makala za Semina za Kimataifa III. Dar es Salaam. Taasisi ya Ukuzaji Kiswahili (TUKI).
Mashele, (2020). Tamthiliya ya Kiswahili https://www.masshele.co.tz/2020/01/tamthiliya-tamthiliya-ya-kiswahili.html.
Mbogo, E. (2015), Sadaka ya John Okello. Dar es Salaam: Karljamer Print technology.
Mbogo, E. (2016). Tamthiliya ya Kiswahili (OSW 602). Dar es Salaam. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Mbogo, E. (2022). Wasifu wa Maisha yangu. Usaili Uwandani. Dar es Salaam.
Omar, M. (2019). Sanaa za Maonyesho katika Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Omar, M. (2020). Tamthiliya ya Kiswahili. Dar es Salaam. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Mhando, P. & Balisidya, N. (1976). Fasihi na Sanaa za Maonyesho. Dar es Salaam. Tanzania Publishing House.
Mhando, R. E. (2015). Kuchunguza Dhamira za Kijamii katika Tamthiliya ya Hatia ya Penina Mlama. Tasnifu ya Uzamili (Haijachapishwa). Dar es Salaam. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Mulokozi, M. M. (1996) Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Mulokozi, M. M. (2017). Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili: Kozi za Vyuoni na Vyuo Vyuo Vikuu (Toleo II). Dar es Salaam. Kauttu Publishers.
Mningo, R. A. (2015). Tathmini ya Mwingilianomatini katika Utunzi wa Emmanuel Mbogo: Utafiti Linganishi wa Tamthiliya ya Ngoma ya Ng’wanamalundi na Fumo Liyongo. Tasnifu ya Uzamili (Haijachapishwa). Dar es Salaam. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Msangi, E. O. (2018). Kuchunguza Ubiblia katika Tamthiliya za Emmanuel Mbogo. Tasnifu ya Uzamili (Haijachapishwa). Dar es Salaam. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Njogu, K. & Chimerah, R. (2011). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu (Chapa 3). Nairobi. Jomo Kenyatta Foundation.
Ochieng, D. (2020). Michakato ya Utafiti wa Isimu ya Kiswahili. Dar es Salaam. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Ponera, A. (2019). Misingi ya Utafiti wa Kitaamuli na Uandishi wa Tasnifu. Dodoma. Central Tanganyika Press.
Sanga, A. (2018). Mkengeuko wa Ujumi wa Kiafrika katika Hadithi Fupi Andishi za Kiswahili: Mifano kutoka Magazeti ya Habari Leo, Nipashe na Mwananchi. Tasnifu ya Uzamivu. Chuo Kikuu cha Dodoma.
Semzaba, E. (1996). Tamthiliya ya Kiswahili. Dar es Salaam. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Seni, D. J. (2020). Fasihi Andishi (Mhadhara Darasani). Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Wafula na wenzake (2020). Uchanganuzi wa Miundo ya Aristotle katika Tamthiliya ya Kinjeketile. Mulika V-39 (79 – 95). Dar es Salaam. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Wamitila, K. W. (2003). Kichocheo cha Fasihi: Simulizi na Andishi. Nairobi. Focus Publications
Wamitila, K. W (2008) Kanzi ya Fasihi: Misingi ya Uchanganuzi na Fasihi. Nairobi. Vide ¬ Muwa Publisherw Limited.
Zelda, E. (2022). Mbinu za Utafiti katika Lugha ya Kiswahili. Dar es Salaam. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Copyright (c) 2023 Emmanuel Oscar Msangi

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.