Matumizi ya Kinaya Kubainishia Maudhui katika Fasihi ya Kiswahili: Mifano kutoka Riwaya ya Chozi la Heri na Tamthilia ya Kigogo

  • Milkah Wanjugu Chuo Kikuu cha Karatina
  • Joseph Nyehita Maitaria, PhD Chuo Kikuu cha Karatina
  • Peter Kinyanjui Mwangi, PhD Chuo Kikuu cha Karatina
Keywords: Riwaya, Kinaya, Mtindo, Nadharia ya mtindo na njia ya kimakusudi
Sambaza Makala:

Ikisiri

Mtunzi wa kazi ya kazi ya fasihi hususan riwaya na tamthilia, hutumia mbinu mahususi kuwasilishia matukio na mawazo yanavyoshuhudiwa katika jamii. Mbinu hizo huteuliwa na mtunzi kwa makusudi ili ujumbe unaokusudiwa kuwasilishwa na kueleweka kwa mwafaka na hadhira. Mbinu hizo ni zile zinazojibainisha katika kitengo cha tamathali za usemi. Katika utafiti huu, mbinu inayozingatiwa ni kinaya ambacho huwasilisha ujumbe kinyume na matarajio. Utafiti huu unatuonyesha matumizi ya kinaya katika riwaya ya Chozi la Heri (2017) ambayo imeandikwa na Matei na tamthilia ya Kigogo (2015) ambayo imeandikwa na Kea. Wanakejeli uhuru katika mataifa yaliyopata uhuru mwanzoni mwa miaka ya 1960 barani Afrika. Mataifa haya ni yale ambayo baada ya kupigania uhuru na kuunyakua kutoka kwa wakoloni, bado raia wanahisi kuwa wanaendelea kuwa katika hali ya kudhulumiwa na hali ya maisha kuwa magumu kutokana na uongozi usioafiki maono ya matarajio yao. Utafiti huu utabainisha jinsi watunzi wa riwaya na tamthilia teule yaani Assumpta Matei na Pauline Kea mtawalia walivyowasilisha kazi zao kwa kuzingatia mbinu ya kinaya katika kubainishia na kuukejeli uongozi katika bara la Afrika. Malengo ya utafiti huu yatakuwa, kufafanua matumizi ya kinaya katika riwaya ya Chozi la Heri na tamthilia ya Kigogo, kujadili jinsi waandishi wa riwaya ya Chozi la Heri na tamthilia ya Kigogo wametumia kinaya katika kuendeleza maudhui na kueleza jinsi mbinu ya kinaya ilivyotumiwa katika usawiri wa wahusika viongozi katika riwaya ya Chozi la Heri na tamthilia ya Kigogo. Utafiti huu utaongozwa na nadharia ya uhakiki wa mtindo na uchanganuzi wa data utaongozwa na mihimili ya nadharia hii kisha matokeo yatawasilishwa kwa njia ya maelezo.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Ali, N. B., & Petersen, K. (2014, September). Evaluating strategies for study selection in systematic literature studies. In Proceedings of the 8th ACM/IEEE international symposium on empirical software engineering and measurement (pp. 1-4).

Augustine, M. (1990). Usawiri wa wahusika makahaba katika Riwaya za Said Ahmed Mohammed. Tasnifu Ya uzamili Chuo kikuu cha Kenyatta (Haijachapishwa).

Chapman, R. (2012). The languge of English Literature London: Edward Arnold Publishers Ltd.

Coombes, J. (953). Literature and criticism. London: Penguin Books Middlesex.

Cuddon, John A. (1999). The Penguin Dictionary of Literary Terms and Literary Theories. Revised by C. Preston. London: Penguin.

Kea, P. (2016). Kigogo. No boundaries Ltd.

Kothari, C. R. (2004). Research methodology: Methods and techniques. New Age International.

Lakoff, G., & Johnson, M. (1980). Metaphors we live by. University of Chicago, Chicago, IL.

Leech, G. N., & Short, M. (2007). Style in fiction: A linguistic introduction to English fictional prose (No. 13). Pearson Education.

Magaju, J. K. (2004).Uhalisia ajabu katika Riwaya ya Said A. Mohammed, Babu Alipofufuka (2001) na Ya Wamitila, Bina-Adamu (2002). Tasnifu ya uzamili Chuo Kikuu cha Kenyatta (Haijachapishwa).

Masinde, E. (2007). Ufundishaji wa ushairi katika shule upili na vyuo. Nairobi. Taaluma Publishers.

Matei, A. K. (2017). Chozi la Heri. One planet publishing & Media services Limited.

Musee, D. (2007). Matumizi ya Majazi kama Mkakati wa Kuepuka Upigaji Marufuku katika Riwaya za Mkangi. Tasnifu ya Uzamili Chuo Kikuu Cha Kenyatta (Haijachapishwa).

Ngara, E. (2011). Stylistic Critism of the African Novel. London: Nairobi: Heineman.

Pandey, P., & Pandey, M. M. (2021). Research methodology tools and techniques. Bridge Center.

Simpson, P. (2004). Stylistics: A Resource Book for students. London : Routldege.

Tuki (2006). Kamusi ya Kiingereza-Kiswahili. Dar es Salaam: TUKI.

Turner, G. W. (1984). Stylistics. Harmond Sworth: Penguine.

Wamitila, K. W. (2008). Kazi ya fasihi : Msingi wa Uchanganuzi wa Fasihi. Nairobi : Vide-Muwa Publishers Ltd.

Tarehe ya Uchapishaji
8 July, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Wanjugu, M., Maitaria, J., & Mwangi, P. (2023). Matumizi ya Kinaya Kubainishia Maudhui katika Fasihi ya Kiswahili: Mifano kutoka Riwaya ya Chozi la Heri na Tamthilia ya Kigogo. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 233-242. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1303