Fasihi ya Kigereza: Uhakiki wa Riwaya ya Haini (Shafi, 2003) kwa Mtazamo wa Ki-Foucault

  • John Musyoka Mutua Chuo Kikuu cha Machakos
  • Justus Kyalo Muusya Chuo Kikuu cha Kirinyaga
  • Gerald Okioma Mogere Chuo Kikuu cha Machakos
Keywords: Gereza, Ki- Foucault, Fasihi, Riwaya Na Uhakiki
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inakusudiwa kutalii jinsi gereza ilivyotumiwa kama msingi wa kuendeleza maudhui katika riwaya ya Haini ya Shafi Adam Shafi. Aidha, inapania kudhihirisha jinsi maudhui ya jamii ya kigereza yanavyobainika kuambatana na sifa zinazotambuliwa na Michael Foucault ambaye ni mwasisi wa nadharia ya Ki-Foucault inayoongoza uhakiki huu. Aghalabu msanii wa fasihi huchota malighafi yake kutokana na jamii anamokulia pamoja na tajriba yake inayoongozwa na ubunifu wake. Pia, matukio na asasi mbalimbali za jamii hutoa mchango mkubwa katika kuendeleza maudhui katika fasihi ya Kiswahili. Gereza ni mojawapo ya asasi zinazokuwa chemichemi ya maudhui yanayoendeleza fasihi katika jamii. Maudhui ni kipengele muhimu katika kazi ya fasihi, yanapofafanuliwa na kueleweka na msomaji, hapo ndipo lengo la mwandishi hukamilika. Katika msingi huu tumechunguza jukumu la mfumo wa kigereza na athari zake katika jamii kwa kurejerea riwaya ya Haini. Huu ni uchunguzi wa kimaktabani. Data ya makala hii imetokana na usomaji na uhakiki wa riwaya teule pamoja na machapisho mengine kuhusu mada na nadharia iliyoongoza uchunguzi. Kwa vile data ni ya kimaelezo, ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia iyo hiyo ya kimaelezo. Matokeo ya uchunguzi huu yanatumiwa kutoa changamoto kwa viongozi wanaoyatumia mamlaka yao vibaya kwa kuwawatia wapinzani wao gerezani na vivyo hivyo kuwafunga wananchi wanaowaongoza gerezani nje ya gereza bila kuwajali.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Buntman, F. (2003). Robben Island: Prisoner Resitstance to Apartheid. Cambridge: CUP.

Encyclopedia Americana (Vol. 22) (1979) New York: Americana Corporation

Encyclopedia New Universal Library (Vol. II) (1967). London: International Learning Systems Corporation Limited.

Freire, P. (1972). Pedagogy of the Oppressed: London: Penguin Books.

Fromm, E. (1980). The Heart of Man. New York: Harpercollions Publishers.

Foucault, M. (1977). Discipline and Punish: The Birth of the Prison. London: Allen Lane.

Jackson, G. (1971). The Prison Letters of George Jackson.London: Ebenezer Bayles and Son Ltd.

Kihoro, W. (1998). Never Say Die: the Chronicle of a Political Prisoner: Nairobi: East African Educational

Kinyatti, M. (1996). Kenya: A Prison Notebook. London: Vita Books.

Shafi, A. (2003). Haini. Nairobi: Longhorn Publishers.

Sithole, N. (1976). Letters from Salibury Prison. Nairobi: Trans-Africa Publishers.

Wamitila, K. (2002). Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Phoenix Publishers Ltd.

Tarehe ya Uchapishaji
18 May, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Mutua, J., Muusya, J., & Mogere, G. (2023). Fasihi ya Kigereza: Uhakiki wa Riwaya ya Haini (Shafi, 2003) kwa Mtazamo wa Ki-Foucault. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 154-164. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1215