Changamoto Zinazowakabili Wanafunzi Wakimbizi wa Sudan Kusini katika Ushairi wa Kiswahili
Ikisiri
Utafiti huu unaeleza changamoto zinazowakumba wanafunzi wakimbizi kutoka Sudan Kusini katika ushairi wa Kiswahili. Utafiti huu ulilenga kuchunguza changamoto zinazokumba wanafunzi wakimbizi kutoka Sudan Kusini katika ushairi wa Kiswahili katika shule ya upili. Nadharia ya Uchanganuzi Makosa ilielekeza utafiti huu. Utafiti huu ulifanywa katika shule ya upili ya Fanaka (jina la msimbo) katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, Kaskazini Magharibi mwa Kenya. Data ilikusanywa kupitia mahojiano, uchunzaji na uchanganuzi wa matini. Matokeo ya utafiti huu yalibaini kuwa wanafunzi wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanakabiliwa na changamoto ya ugumu wa kujibu maswali ya ushairi. Changamoto ya ugumu wa ushairi kwa wanafunzi wakimbizi kutoka Sudan Kusini imetokana na mtazamo hasi kuwa ushairi ni mgumu, ukosefu wa miongozo ya ushairi, ukosefu wa vitabu teule vya ushairi, na walimu kutotumia mbinu na nyenzo mwafaka za kufundisha ushairi. Utafiti umetoa mapendekezo ya jinsi ya kuboresha ufundishaji wa ushairi katika shule za upili nchini Kenya. Aidha, utafiti huu unatoa mchango kwa ufundishaji na ujifunzaji wa ushairi wa Kiswahili kwa wanafunzi wa kigeni wanaojifunza Kiswahili
Upakuaji
Marejeleo
Ayot, H.O (1986). Instructional Materials for Educational Communication and Technology. First Edition. Kenyatta University, Kenya.
Corder, S. P. (1967). The Significance of Learners’ Errors. International Review of Applied Linguistics in Language Teaching, 5, 161-170.
Corder, S.P. (1974). Error Analysis, In Allen, J.L.P. and Corder, S.P. (1974). Techniques in Applied Linguistics. Oxford: Oxford University Press
Iyaya , R., Kobia, J., & Luganda, M. (2016). Uchanganuzi wa Mambo Yanayoathiri Ufundishaji wa Ushairi Katika Shule za Upili Nchini Kenya, Mara Research Journal of Kiswahili 1(1), 18-36.
Mohamed, S. A. ( 1990). Mfumo wa 8:4:4 Mbinu na Mazoezi ya Ushairi. Nairobi. Evans Brothers (Kenya) Ltd.
Mukoya, H. (2019). Ufundishaji wa Ushairi kwa Kutumia Tamthilia Katika Shule Za Upili Kenya: Uchunguzi Kifani kaunti ndogo ya Teso Kaskazini. Tasnifu ya uzamili, Chuo Kikuu cha Kibabi (haijachapishwa)
Mwangi, J. (2005). Ufundishaji na Ujifunzaji wa Ushairi katika Shule za Upili.Tasnifu ya uzamili: Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Njogu, K., & Chimerah, R. (2000) Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na mbinu. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.
Norrish, J. (1983). Language learners and their Errors. London: Macmillan Press.
Odaga, A. (1985). Literature for children and Young People in Nairobi. Nairobi University Press.
Oyinda, P., & Lokidor, E. (2021) Mwongozo wa Ushairi kwa Shule za Upili. Nairobi: Dilev Publication Limited.
KNEC (2019). Ripoti ya utahini ya Karatasi ya 3, Fasihi .
Shitemi, N. (2010). Ushairi wa Kiswahili; kabla ya karne ya ishirini. Eldoret :Moi University Press.
Swaleh, A., & Timammy, R. (2019). Literature as medium for Moral Instruction: A Swahili/Islamic Analysis of Ahmad Nassir's Utenzi wa Mtu ni Utu. Moi University Press.
Taasisi ya Elimu ya Kenya (2006). Kiswahili sekondari: Mwongozo wa Mwalimu. Nairobi: K.I.E
Walla, W. (1988). Malenga wa Ziwa Kuu, Maswali na Istilahi za Kifasihi, Nairobi: East African Education Publishers.
Copyright (c) 2023 Edward Ekadeli Lokidor

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.