Simulizi za Unyanyapaa Unaohusiana na Virusi vya UKIMWI/UKIMWI Nchini Kenya Kibaadausasa

  • Alexander K. Rotich, PhD University of Kabianga
Sambaza Makala:

Ikisiri

Tangu kuibuka kwa janga la Virusi Vya Ukimwi/Ukimwi maarufu kama VVU/UKIMWI zaidi ya miongo mitatu iliyopita, juhudi nyingi zilizowekwa na serikali za mataifa mbalimbali, masharika yasiyokuwa ya kiserikali na watu binafsi hazijafaulu kutokomeza kabisa janga hili. Hii ni kwa sababu, kama magonjwa mengine hatari, ugonjwa huu unahusishwa na unyanyapaa unaoelekezwa kwa walioambukizwa Virusi Vya Ukimwi. Isitoshe, hata matumizi ya dawa za kupunguza makali ya virusi husika, almaarufu ARVs yamekuwa chanzo kikubwa cha unyanyapaa badala ya kuleta afueni kwa waathiriwa. Unyanyapaa unaoelekezwa kwa wanaoonyesha dalili za kuambukizwa Virusi Vya  Ukimwi pamoja na wale wanaotumia dawa za kupunguza makali unaelekea kuufanya ugonjwa huu kuwa changamano zaidi. Kwa kujikita katika nyimbo tatu za Kiswahili zilizoimbwa katika nyakati hizi za kibaadausasa, makala hii imepania kubainisha na kufafanua simulizi kuu na simulizi ndogo ndogo zinazokuza na zinazopinga unyanyapaa unaohusishwa na VVU/UKIMWI. Kwa kuongozwa na nadharia ya Baadausasa, watafiti walibainisha na kuchanganua vipande vya simulizi zinazohusiana na unyanyapaa husika. Aidha, wamedhihirisha kuwa, nyimbo, hasa za kibaadausasa ni chombo mhususi kinachoweza kutumiwa  na wanajamii kupiga vita unyanyapaa unaohusishwa na VVU/UKIMWI hasa ikizingatiwa kwamba, mbali na kutatiza ufanisi uliofikiwa katika vita dhidi ya VVU/UKIMWI, unyanyapaa ndio chanzo cha vifo vingi vinavyohusishwa na VVU/UKIMWI.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.
Tarehe ya Uchapishaji
21 February, 2019
Jinsi ya Kunukuu
Rotich, A. (2019). Simulizi za Unyanyapaa Unaohusiana na Virusi vya UKIMWI/UKIMWI Nchini Kenya Kibaadausasa. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 1(1), 1-6. Retrieved from https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/1