Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili https://journals.eanso.org/index.php/eajss <p>Maendeleo ya Kiswahili kama lugha ni muhimu katika kukuza na kuhifadhi utamaduni wa kiasili, maarifa na dini katika mikoa inayozungumza Kiswahili barani Afrika. Jarida hili linalokaguliwa na wanarika kwa hivyo linachapisha nakala za Kiswahili tu. Nakala zinazoweza kuchapishwa chini ya jarida hili ni nakala kutoka kwa aina zote za maarifa isipokuwa zimeandikwa kwa lugha ya Kiswahili. Waandishi wanaowasilisha kwa jarida hili wanaweza kuamua kutafsiri nakala zao kwa Kiingereza na kuchapisha tafsiri katika majarida mengine yoyote tulio nayo.</p> East African Nature & Science Organization (EANSO) sw-KE Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili 2707-3467 Usawiri wa Vijana wa Kisasa katika Riwaya ya Dunia yao ya Kiswahili https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/1669 <p>Makala hii itachunguza usawiri wa vijana katika dunia ya sasa inayobadilika kila uchao. Itafanya hivi kupitia uchanganuzi wa riwaya mpya ya Dunia Yao (2006) ya S.A Mohamed.&nbsp; Utafiti unaonyesha kwamba vijana kote duniani sasa wana utamaduni wao ambao watafiti wanaueleza kama ‘ulimwengu huru’ wa vijana ulio na mitindo na njia za maisha ambazo, vijana hufuata ili kujitofautisha na utamaduni wa wazazi wao. Utamaduni wa vijana kwa kiasi kikubwa ni zao la maendeleo katika jamii za ulimwengu. Kadri jamii inavyosonga mbele kimaendeleo, ndivyo ambavyo utamaduni wa vijana unakuzwa, unaimarishwa na kusambazwa miongoni mwa vijana kote duniani. Vijana wamebuni utamaduni wao kama njia moja ya kuasi dhidi ya utamaduni uliotawaliwa na wazee. Wanataka kujihusisha na tabia kama matumizi ya dawa za kulevya, ushoga, uasi wa maadili ya kijamii, Mitindo mipya ya mavazi, muziki miongoni mwa tabia nyingine ambazo wanajua huwatenga wazee. Hii ni tabia ibuka ya vijana kupania kuonyesha nguvu na uwezo wao katika jamii. Ujumbe wanaopitisha ni kuwa hawako tayari kushiriki utamaduni unaowadhibiti na kuwanyima nafasi yao katika jamii. Malengo mahususi yatakayoongoza makala haya ni pamoja na kuangazia sifa za vijana wa kisasa na wakati huo huo kufafanua njia mabazo wanajamii wanaweza kutumia ili kujaribu kuziba mwanya mpana uliopo kati ya kizazi cha jana na cha leo. Makala hii itaongozwa na nadharia ya uhalisia. Mhimili mkuu wa nadharia ya uhalisia ambao utaongoza makala ni kwamba, fasihi ni kioo cha jamii na inapaswa kumulika maisha kama yalivyo. Muundo wa kimaelezo utatumika kuchanganua data. Data itakusanywa kutokana na kusoma riwaya teule na kudondoa sehemu zinazolingana na malengo ya utafiti. Data itadondolewa, itanukuliwa, itapangwa kisha kuchanganuliwa kulingana na mada husika</p> Naomi Nzilani Musembi, PhD Fred Wanjala Simiyu, PhD ##submission.copyrightStatement## http://creativecommons.org/licenses/by/4.0 2024-01-02 2024-01-02 7 1 1 10 10.37284/jammk.7.1.1669 Upambanuzi wa Mikakati ya Kitashtiti katika Vibonzo vya Kisiasa Vya Gado https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/1685 <p>Taalumu ya uchoraji na uchapishaji wa vibonzo vya kisiasa umekuwepo tangu karne ya kumi na nane. Saana hii huwavutia watafiti wengi kutokana na uwezo wake wa kusimba jumbe zisizoweza kusemwa wazi wazi. Ifahamike kuwa sifa kuu ya vibonzo vya kisiasa ni kuwa vinapaswa kuwa cheshi na vyenye tashtiti ndiposa viweze kuwasilisha masuala tata kwa njia ya kimzaha. Kutokana na hali hii, utafiti huu ulichunguza tashtiti katika vibonzo vya kisiasa vya Gado vilivyochapishwa katika mwaka wa 2017 kwenye tovuti yake. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kupambanua mikakati iliyotumika katika kuendeleza maudhui ya kitashtiti katika vibonzo vilivyoteuliwa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Semiotiki iliyoasisiwa na Ferdinand De Saussure, na baadaye kuhakikiwa na Chandler na pia Wamitila. Mihimili ya nadharia hii ilitumika kuchambua mikakati iliyotumiwa na Gado katika vibonzo vyake kwa minajili ya kuendeleza maudhui ya kitashtiti. Utafiti huu ni wa kimaelezo na ulifanyika mtandaoni, pale ambapo mtafiti alipekua tovuti ya Gado (www.gadocartoons.com) na kuteua kimaksudi vibonzo vinane kutokana na jumla ya vibonzo ishirini vilivyokuwa vimechapishwa katika mwaka wa 2017. Uteuzi huu ulijikita katika vibonzo vilivyofungamana na madhumuni ya utafiti huu. Kwa jumla, utafiti huu ulidhibitisha kuwa mwanakibonzo Gado alitumia mbinu za lugha kama vile; kinaya, kejeli, metonimia, sitiara, analojia na mwingiliano matini kama mikakati ya kuibua kitashtiti katika vibonzo vyake. Vilevile, utafiti huu ulionyesha kuwa Gado alitumia ishara kama vile; matumizi ya rangi mbalimbali, pamoja na alama kama vile; heshtegi, mviringo na nyota kama mikakati ya kuibua tashtiti katika vibonzo vyake. Mwishowe, utafiti huu ulidhibitisha kuwa vibonzo vilivyochapishwa kwenye mtandao, vilidhihirisha uhuru na ukali mwingi katika usawiri wa masuala mbalimbali, jambo ambalo lilisaidia katika kufanikisha lengo kuu la tashtiti; ambalo ni ushambulizi unaochochea mabadiliko. Mwishowe, matokeo ya utafiti huu yalitarajiwa kuwanufaisha wanamawasiliano, wanasemiotiki na wasomi wa masuala ya kisiasa kwa kuwapa mtazamo mpya kuhusiana na matumizi ya maneno na ishara katika kusimba jumbe tata zinazochapishwa kwenye mtandao ambapo kuna uhuru mwingi wa kuelezea masuala tata bila kudhibitiwa.</p> Kerryann Wanjiku Mburu Sheila Wandera-Simwa, PhD Nabea Wendo, PhD ##submission.copyrightStatement## http://creativecommons.org/licenses/by/4.0 2024-01-08 2024-01-08 7 1 11 27 10.37284/jammk.7.1.1685 Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/1699 <p>Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee ya uandishi ambayo watu wasioona hutumia katika mawasiliano na usomi wao. Vilevile, kutokuwepo kwa kipengele muhimu cha matamshi katika kamusi za breili na vitabu vya sarufi hasa vya sekondari. Jambo jingine ni kwamba, wanafunzi wanaotumia breili hupewa maswali mbadala wakati wanapotahiniwa katika maeneo ya fonolojia, mofolojia, na hata katika uchanganuzi wa sentensi. Aidha, kutokuwepo kwa ishara bainifu za isimu katika maandishi ya breili ya Kiswahili. Kichocheo cha mwisho, praima mbili za breili ya Kiswahili: ya 1978 na 1995 zinazotumiwa Afrika Mashariki hazina ishara za kiisimu. Utafiti huu ulikusudia kujibu maswali yafuatayo: changamoto zipi zinazozuia usimilishaji wa ishara za kiisimu katika breili ya Kiswahili? Rasimu za Kiingereza na Kiswahili huathiriana kwa njia zipi? Ukosefu wa ishara za isimu katika breili huathiri ufundishaji wa isimu kwa njia gani?&nbsp; Na mwisho, mikato ya Kiswahili na ya Kiingereza inayotumia nukta zinazofanana huathiri uchapishaji wa vitabu vya isimu kwa njia zipi? Utafiti huu ulilenga kutimiza malengo yafuatayo – kwanza, kubainisha na kutatua changamoto zinazozuia usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Pili, Kuchanganua rasimu ya Kiingereza na ya Kiswahili. Aidha, kuchunguza athari ya ukosefu wa ishara hizi katika ufundishaji wa isimu. Mwisho, kutathmini athari ya matumizi ya mikato inayotumia nukta zinazofanana katika uchapishaji wa vitabu vya isimu. Makala haya yameshughulikia vikwazo vya usimilishaji wa ishara za isimu katika breili. Mtafiti alitumia mbinu ya mahojiano katika kukusanya dataUtafiti huu ulichanganua usimilishaji wa ishara hizi kwa kuzingatia nadharia ya usomaji na uandishi wa breili iliyoasisiwa na Kizuka na Fuji (2005). Mtafiti aligundua kuwa uchache wa nukta nundu umesababisha uradidi mwingi wa matumizi ya nukta nundu hizi. Uradidi huu umechangia kuwepo kwa utata&nbsp; wa kimaana katika fonolojia na sintaksia ya Kiswahili, vikwazo vya ufundishaji wa isimu miongoni mwa wanafunzi wasioona, makosa katika vitabu vya sarufi hasa kidato cha kwanza na kidato cha pili na changamoto zinazotinga usimilishaji wa ishara za kiisimu katika Breili. Utafiti huu utawafaidi wanafunzi wanaotumia breili na walimu na wahadhiri wanaofunza isimu</p> Daniel Mburu Mwangi, PhD ##submission.copyrightStatement## http://creativecommons.org/licenses/by/4.0 2024-01-18 2024-01-18 7 1 28 38 10.37284/jammk.7.1.1699 Athari za Mtagusano wa Lugha ya Kiswahili na Kikuyu kwa Lugha ya Kishona https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/1703 <p>Utafiti huu unalenga kuchunguza athari zinazotokana na mtagusano wa lugha ya Kiswahili na Kikuyu kwa lugha ya Kishona. Shona ni kabila mojawapo la Wabantu ambao asili yao ni nchini Zimbabwe na walifika nchini Kenya zaidi ya miaka sitini iliyopita kama wamishenari. Kufikia sasa, Washona wametagusana na jamiilugha mbalimbali nchini Kenya katika Kaunti ya Kiambu inayojulikana kwa wingilugha hasa kwenye mitaa ya Kinoo, Kikuyu, Kiambaa, Gitaru, na Githurai. Mtagusano wa lugha unapotokea, lugha husika huathirika kwa viwango mbalimbali kama vile kwenye fonetiki, kifonolojia, kimofolojia, kisintaksia na hata kisemantiki. Utafiti&nbsp; huu uliongozwa na nadharia ya uthabiti wa kiisimujamii wa lugha iliyoasisiwa na Giles, Bourhis na Taylor (1977) na kuendelezwa na Landweer (2000) na nadharia ya uzalishaji kijamii ya Bourdieu (1977). Mawanda mawili yalihusishwa ambayo ni utafiti wa maktabani na wa nyanjani. Utafiti wa nyanjani ulifanyika katika makazi ya wanajamiilugha ya Kishona ili kupata data ya moja kwa moja iliyojibu swali la utafiti. Jumuiya ya utafiti ilikuwa kabila la Washona wanaoishi katika mitaa mitano ya kaunti ya Kiambu.Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kimaksudi na kwa njia elekezi. Mbinu zilizotumiwa katika ukusanyaji data ni pamoja na hojaji, mahojiano, uchunzaji, mijadala ya vikundi vidogovidogo na maswali mepesi yaliyoandaliwa kimbele. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kutumia mbinu changamano. Matokeo yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo, takwimu na asilimia huku yakiongozwa na nadharia mbili za utafiti. Kufuatia juhudi za UNESCO za kudumisha lugha asilia, utafiti huu ulikuwa wa manufaa kwa taifa la Kenya na mataifa mengine kwa kuwa uliongezea data muhimu katika kuhifadhi utamaduni wa Washona na mwelekeo wa udumishaji kwa lugha za kabila mbalimbali</p> Mercy Moraa Motanya Stephen Njihia Kamau, PhD Boniface Ngugi, PhD ##submission.copyrightStatement## http://creativecommons.org/licenses/by/4.0 2024-01-22 2024-01-22 7 1 39 55 10.37284/jammk.7.1.1703 Athari ya Rasimu za Breili katika Usimilishaji wa Ishara Za Isimu https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/1714 <p>Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee ya uandishi ambayo watu wasioona hutumia katika mawasiliano na usomi wao. Vilevile, kutokuwepo kwa kipengele muhimu cha matamshi katika kamusi za breili na vitabu vya sarufi hasa vya sekondari. Jambo jingine ni kwamba, wanafunzi wanaotumia breili hupewa maswali mbadala wakati wanapotahiniwa katika maeneo ya fonolojia, mofolojia na hata katika uchanganuzi wa sentensi. Aidha, kutokuwepo kwa ishara bainifu za isimu katika maandishi ya breili ya Kiswahili. Kichocheo cha mwisho, praima mbili za breili ya Kiswahili: ya 1978 na 1995 zinazotumiwa Afrika Mashariki hazina ishara za kiisimu. Utafiti huu ulikusudia kujibu maswali yafuatayo: changamoto zipi zinazozuia usimilishaji wa ishara za kiisimu katika breili ya Kiswahili? Rasimu za Kiingereza na Kiswahili huathiriana kwa njia zipi? Ukosefu wa ishara za isimu katika breili huathiri ufundishaji wa isimu kwa njia gani?&nbsp; Na mwisho, mikato ya Kiswahili na ya Kiingereza inayotumia nukta zinazofanana huathiri uchapishaji wa vitabu vya isimu kwa njia zipi? Utafiti huu ulilenga kutimiza malengo yafuatayo – kwanza, kubainisha na kutatua changamoto zinazozuia usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Pili, Kuchanganua rasimu ya Kiingereza na ya Kiswahili. Aidha, kuchunguza athari ya ukosefu wa ishara hizi katika ufundishaji wa isimu. Mwisho, kutathmini athari ya matumizi ya mikato inayotumia nukta zinazofanana katika uchapishaji wa vitabu vya isimu. Makala haya yatashughulikia lengo la kwanza. Mbinu za utafiti zifuatazo ndizo zilizotumiwa kukusanya data; uchunzaji, hojaji na mahojiano. Utafiti huu ulichanganua usimilishaji wa ishara hizi kwa kuzingatia nadharia ya usomaji na uandishi wa breili iliyoasisiwa na Kizuka na Fuji (2005). Mtafiti aligundua kuwa uchache wa nukta nundu umesababisha uradidi mwingi wa matumizi ya nukta nundu hizi. Uradidi huu umechangia kuwepo kwa utata wa kimaana katika fonolojia na sintaksia ya Kiswahili, vikwazo vya ufundishaji wa isimu miongoni mwa wanafunzi wasioona, makosa katika vitabu vya sarufi hasa kidato cha kwanza na kidato cha pili na changamoto zinazotinga usimilishaji wa ishara za kiisimu katika Breili. Utafiti huu utawafaidi wanafunzi wanaotumia breili na walimu na wahadhiri wanaofunza isimu</p> Daniel Mburu Mwangi, PhD ##submission.copyrightStatement## http://creativecommons.org/licenses/by/4.0 2024-01-22 2024-01-22 7 1 56 68 10.37284/jammk.7.1.1714 Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/1712 <p>Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee ya uandishi ambayo watu wasioona hutumia katika mawasiliano na usomi wao. Vilevile, kutokuwepo kwa kipengele muhimu cha matamshi katika kamusi za breili na vitabu vya sarufi hasa vya sekondari. Jambo jingine ni kwamba, wanafunzi wanaotumia breili hupewa maswali mbadala wakati wanapotahiniwa katika maeneo ya fonolojia, mofolojia, na hata katika uchanganuzi wa sentensi. Aidha, kutokuwepo kwa ishara bainifu za isimu katika maandishi ya breili ya Kiswahili. Kichocheo cha mwisho, praima mbili za breili ya Kiswahili: ya 1978 na 1995 zinazotumiwa Afrika Mashariki hazina ishara za kiisimu. Utafiti huu ulikusudia kujibu maswali yafuatayo: changamoto zipi zinazozuia usimilishaji wa ishara za kiisimu katika breili ya Kiswahili? Rasimu za Kiingereza na Kiswahili huathiriana kwa njia zipi? Ukosefu wa ishara za isimu katika breili huathiri ufundishaji wa isimu kwa njia gani? Na mwisho, mikato ya Kiswahili na ya Kiingereza inayotumia nukta zinazofanana huathiri uchapishaji wa vitabu vya isimu kwa njia zipi? Utafiti huu ulilenga kutimiza malengo yafuatayo – kwanza, kubainisha na kutatua changamoto zinazozuia usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Pili, Kuchanganua rasimu ya Kiingereza na ya Kiswahili. Aidha, kuchunguza athari ya ukosefu wa ishara hizi katika ufundishaji wa isimu. Mwisho, kutathmini athari ya matumizi ya mikato inayotumia nukta zinazofanana katika uchapishaji wa vitabu vya isimu. Makala haya yameshughulikia lengo la tatu na la nne. Mbinu za utafiti zifuatazo ndizo zilizotumiwa kukusanya data; uchunzaji, hojaji na mahojiano. Utafiti huu ulichanganua usimilishaji wa ishara hizi kwa kuzingatia nadharia ya usomaji na uandishi wa breili iliyoasisiwa na Kizuka na Fuji (2005). Mtafiti aligundua kuwa uchache wa nukta nundu umesababisha uradidi mwingi wa matumizi ya nukta nundu hizi. Uradidi huu umechangia kuwepo kwa utata&nbsp; wa kimaana katika fonolojia na sintaksia ya Kiswahili, vikwazo vya ufundishaji wa isimu miongoni mwa wanafunzi wasioona, makosa katika vitabu vya sarufi hasa kidato cha kwanza na kidato cha pili na changamoto zinazotinga usimilishaji wa ishara za kiisimu katika Breili. Utafiti huu utawafaidi wanafunzi wanaotumia breili na walimu na wahadhiri wanaofunza isimu</p> Daniel Mburu Mwangi, PhD ##submission.copyrightStatement## http://creativecommons.org/licenses/by/4.0 2024-01-22 2024-01-22 7 1 69 78 10.37284/jammk.7.1.1712 Mitazamo ya Kiskaz Kuhusu Covid-19 Inavyojitokeza katika Lugha ya Wananchi Nchini Kenya https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/1754 <p>Madhumni ya makala haya yalikuwa ni kubainisha na kuchanganua mitazamo ya WaKenya kuhusu Tangaavu la Korona (COVID-19) kama inavyodhihirika kupitia mazungumzo ya kikawaida, Skaz. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, tafiti za awali kuhusu mada hii hazikukitwa katika misingi ya Skaz. Kwa hivyo, taarifa nyingi kuhusu Tangaavu la Korona zilizowasilishwa na Shirika la Afya Ulimwenguni pamoja na Wizara ya Afya nchini Kenya zilikuwa za kitaalamu (kiakademia). Utafiti huu ulikuwa wa nyanjani na ulifanyika Kericho, Kenya. Mtafiti aliteua sampuli kimakusudi na kukusanya data kwa kutumia mbinu ya utazamaji nyanjani. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ya Usemezano ikijumuisha sifa za Skaz kama ilivyoelezwa na Bakhtin ikitiliwa nguvu na Mbinu ya Urazini wa Kiwatu kama ilivyoendelezwa na Sacks na wenzake. Uchanganuzi wa data ulionesha kuwa, mwanzomwanzo, kutokana na kukosa ufahamu wa kitaaluma kuhusu ugonjwa “mpya” Tangaavu la COVID-19 kwa jumla, bila kukusudia kupotosha WaKenya waliibuka na mitazamo mbalimbali kuhusu ugonjwa huu. Mitazamo hii pia ilitokana na jitihada za hekaheka kutafuta njia za kuzuia usambazaji na hata tiba miongoni mwa wanajamii. Utafiti huu umeweka wazi mitazamo “hasi” kuhusu ugonjwa wa COVID-19 jinsi ili(na)vyodhihirika katika mazungumzo ya kikawaida na hivyo kuwafaidi watafiti wa utabibu na wapangaji sera za kiserikali kutilia maanani mitazamo katika lugha ya kikawaida haswa kwenye majanga ya kiulimwengu</p> Alexander Rotich, PhD ##submission.copyrightStatement## http://creativecommons.org/licenses/by/4.0 2024-02-13 2024-02-13 7 1 79 86 10.37284/jammk.7.1.1754 Polisemi Ambazo Zimeundwa Kutokana Na Sitiari Na Metonimu Katika Kiswahili https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/1769 <p>Makala haya imechunguza polisemi ambazo zimeundwa kutokana na sitiari na metonimu katika Kiswahili.&nbsp; Kimsingi, polisemi ni leksimu moja yenye maana nyingi ambazo zinahusiana kwa njia moja au nyingine. Pia polisemi huundwa kwa njia zingine kwa mfano, ukopaji, mabadiliko katika matumizi ya neno, na ufasiri mpya wa homonimu. Nadharia ya semantiki tambuzi ilitumiwa katika uchambuzi wa data ya utafiti huu. Nadharia hii ni sehemu ya nadharia ya Isimu Tambuzi ambayo ina misingi yake katika saikolojia tambuzi .&nbsp; Data ya makala haya ilikusanywa maktabani. Maneno ambayo ni polisemi na yameundwa kwa sitiari na metonimu kwenye Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2018) yalikusanywa. Mbinu ya usampulishaji wa kimaksudi ilitumika katika uteuzi wa sampuli. Kutokana na data ya utafiti huu, imebainika kuwa kuna baadhi ya polisemi zilizojitokeza ndani ya homonimu.&nbsp; Kwa mfano, tata1 na chuo1. Pia, utafiti huu umebaini kuwa polisemi nyingi huundwa kisitiari ikilinganishwa na metonimu. Makala haya inapendekeza kwamba tafiti zingine zaidi zinaweza kufanywa kuhusu namna mbinu zingine za lugha kama vile chuku, methali, nahau na tashibihi zinaweza kuchangia katika Isimu</p> Mark Elphas Masika Leonard Chacha Mwita, PhD ##submission.copyrightStatement## http://creativecommons.org/licenses/by/4.0 2024-02-22 2024-02-22 7 1 87 97 10.37284/jammk.7.1.1769 Mwingilianomatini kama Upekee wa Mtindo wa Emmanuel Mbogo: Mifano Kutoka Ngoma ya Ng’wanamalundi na Fumo Liongo https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/1770 <p>Makala haya yanahusu mwingilianomatini kama upekee wa mtindo wa Emmanuel Mbogo kwa kurejelea tamthiliya zake mbili: <em>Ngoma ya Ng’wanamalundi </em>(1988) na <em>Fumo Liongo </em>(2009). Lengo la Makala haya ni kuibua upekee wa kimtindo wa Emmanuel Mbogo kupitia matumizi ya mwingilianomatini kwa kuangazia tamthiliya zake mbili alizoandika kwa kupishana muongo mmoja. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu mbili za ukusanyaji data ambazo ni usomaji makini na usaili. Aidha, nadharia ya mwingilianomatini imetumika katika kuchambua na kujadili data. Makala haya yanajadili kuwa matumizi ya mwingilianomatini katika utunzi wa Emmanuel Mbogo yanadhihirisha upekee wake wa kimtindo katika utunzi wake. Hili linajidhihirisha katika matumizi ya hadithi, ngoma, nyimbo, majigambo, wahusika wa fasihi simulizi, ushairi na nguvu za sihiri. Hivyo, makala haya yanahitimisha kuwa kila mtunzi ana upekee wake katika utunzi na uandishi wa kazi za fasihi, upekee huu hujidhihirisha katika uteuzi wa mtindo ambao unajirudiarudia katika kazi zake</p> Hadija Jilala ##submission.copyrightStatement## http://creativecommons.org/licenses/by/4.0 2024-02-22 2024-02-22 7 1 98 113 10.37284/jammk.7.1.1770 Mikabala Tofauti ya Waandishi wa Vitabu vya Kiada kuhusu Kipengele cha Mtindo wa Uandishi Insha za Kiswahili Nchini Kenya https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/1803 <p>Makala haya yanabainisha mikabala ya waandishi wa vitabu vya kiada katika ufundishaji na ujifundishaji wa mtindo wa insha za Kiswahili kwa shule za upili nchini Kenya. Mikabala tofauti ya waandishi aghalabu huwa chanzo cha utata miongoni mwa walimu na wanafunzi na hivyo kuathiri matokeo ya mtihani wa kitaifa. Uchunguzi huu umekitwa kwa mihimili ya Nadharia ya Mtindo iliyoasisiwa na Louis Tonko Milic. Nadharia hii inashikilia kuwa mtindo hutegemea mtu binafsi. Utafiti huu ulitumia muundo wa kimaelezo, mkabala wa kithamano. Idadi lengwa ya utafiti ni walimu wa somo la Kiswahili 73, wanafunzi 2,000 na vitabu vya kiada 7 vya shule za upili. Kwa hivyo, usampulishaji wa kimakusudi ulitumiwa kuteua walimu 22, wanafunzi 320 na vitabu vya kiada 6. Mbinu za ukusanyaji wa data zilizotumika ni uchanganuzi wa yaliyomo, mahojiano na hojaji. Data ilichanganuliwa kwa kutumia asilimia, majedwali na kuwasilishwa kiufafanuzi. Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kwamba, matumizi ya vitabu vya kiada tofauti tofauti yanazua mikabala tofauti katika ufundishaji na ujifundishaji wa mtindo wa insha. Hali hii inatokana na waandishi wa vitabu kiada kuwa na mikabala tofauti kuhusu mtindo wa insha za Kiswahili. Matokeo ya uchunguzi huu ni muhimu kwa walimu na wanafunzi wa Kiswahili katika shule za upili, viwango vingine vya elimu na wakuza mitaala pamoja na waandishi wa vitabu vya kiada. Wizara ya Elimu pamoja na vyuo vya walimu kupitia warsha na maarifa zaidi ya yale ya vitabu vya kiada, watafaidi mikakati ya kuimarisha ufundishaji na ujifundishaji wa somo la insha</p> Nester Ateya Eric Walela Wamalwa Stanley Adika Kevogo ##submission.copyrightStatement## http://creativecommons.org/licenses/by/4.0 2024-03-06 2024-03-06 7 1 114 123 10.37284/jammk.7.1.1803 Hali ya Kipindi cha Kupigania Uhuru na Mabadiliko ya Kimaudhui ya Ushairi wa Kiswahili Kati ya Miaka 1930 Hadi 1960 Nchini Tanzania https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/1804 <p>Makala hii inachunguza jinsi hali ya kipindi cha kupigania uhuru ilivyochochea mabadiliko ya kimaudhui ya ushairi wa Kiswahili kati ya miaka 1930 hadi 1960 nchini Tanzania. Kulingana na makala hii hali ni matukio mahsusi yanayoathiri ubunifu wa maudhui ya ushairi. Ili kukuza mjadala wetu, makala hii imezingatia kipindi cha kupigania uhuru nchini Tanganyika. Uchunguzi unazingatia mashairi teule kutoka diwani za watunzi wafuatao: Mathias Mnyampala, “Diwani ya Mnyampala (1965)”, Amri Abedi, “Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri (1954)”,&nbsp; Akilimali Snow-White, “Diwani ya Akilimali (1963)”, Shaaban Robert , “ Koja la Lugha (1969), Pambo la Lugha (1966), Kielezo cha Fasili (1968), na Masomo Yenye Adili (1967)”, na Saadani Kandoro, “Mashairi ya Saadani, (1966)”. Mashairi yaliyoteuliwa yanasomwa na kuhakikiwa ili kubainisha maudhui yaliyomo. Uchanganuzi wa data unaongozwa na mihimili ya Nadharia ya Utegemezi na Nadharia ya Ubidhaaishaji wa Lugha. Katika mashairi teule, inabainishwa kuwa washairi walishiriki katika siasa. Vyama vya kisiasa vilitumia Kiswahili kama chombo cha kuunganisha Watanganyika kisiasa. Mashairi yaliandikwa katika magazeti ili kuhamasisha na kuzindua watu wapiganie uhuru. Mashairi yalibeba maudhui ya dhuluma za kikoloni, utetezi wa haki, umoja wa Waafrika, uzalendo, chama cha TANU, uhuru, sifa za viongozi bora, madaraka na utamaduni wa Waafrika</p> Helina Wanjiku Njuguna Geoffrey Kitula King’ei, PhD Richard Makhanu Wafula, PhD ##submission.copyrightStatement## http://creativecommons.org/licenses/by/4.0 2024-03-06 2024-03-06 7 1 124 136 10.37284/jammk.7.1.1804 Mikakati ya Udumishaji wa Lugha ya Kishona Nchini Kenya https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/1824 <p>Makala haya yanalenga kuchunguza mikakati mbalimbali inayotumiwa na Washona katika kudumisha lugha ya Kishona nchini Kenya. Washona ni Wabantu ambao asili yao ni nchi ya Zimbabwe na walifika nchini Kenya kuanzia mwaka wa 1959 kwa lengo la kuhubiri injili kupitia kwa dhehebu la Gospel of God. Washona wametagusana na jamiilugha mbalimbali nchini Kenya hasa katika kaunti ya Kiambu iliyo na hali ya wingilugha hasa kwenye mitaa ya Kinoo, Kikuyu, Kiambaa, Gitaru, na Githurai ambayo ni makazi ya Washona wengi wanaoishi nchini Kenya. Mtagusano wa lugha mbalimbali waweza kuhatarisha uthabiti wa kiisimujamii wa lugha ambayo ina idadi ndogo ya wazungumzaji na ambayo haina usaidizi kutoka asasi mbalimbali za kiserikali. Hali hii ndiyo inayoikabili jamiilugha ya Washona nchini Kenya. Makala haya yaliongozwa na nadharia ya uzalishaji kijamii ya Bourdieu (1977) ambayo iliendelezwa na O’Riagain (1994). Kupitia kwa mhimili wake wa kwanza unaosema kwamba kila kizazi hubuni na kuweka mikakati ya kurithisha kizazi kinachofuata utamaduni wake, nadharia hii inasisitiza mikakati ambayo jamiilugha huweka ili kudumisha lugha ambayo ni kipengele muhimu cha utamaduni. Utafiti huu ulifanyikia maktabani na nyanjani. Utafiti wa nyanjani ulifanyikia kwenye maeneo ambayo wanajamiilugha wa Kishona huishi ili kupata data iliyobainisha mikakati ambayo Washona wanatumia ili kudumisha lugha yao ya Kishona nchini Kenya. Jumuiya ya utafiti ilikuwa jamiilugha ya Washona wanaoishi katika mitaa mitano ya kaunti ya Kiambu. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kimaksudi na kwa njia elekezi. Mbinu zilizotumiwa katika ukusanyaji wa data ni mahojiano, uchunzaji na mijadala ya vikundi vidogovidogo. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kutumia mbinu changamano. Matokeo yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo na kuongozwa na nadharia ya uzalishaji kijamii. Kufuatia juhudi za UNESCO za kudumisha lugha asilia, utafiti huu ni wa manufaa kwa Washona wenyewe, taifa la Kenya na mataifa mengine kwa kuwa uliongezea data muhimu katika kuhifadhi lugha ya Kishona nchini Kenya</p> Mercy Moraa Motanya Boniface Ngugi Stephen Njihia Kamau ##submission.copyrightStatement## http://creativecommons.org/licenses/by/4.0 2024-03-14 2024-03-14 7 1 137 154 10.37284/jammk.7.1.1824 TEHAMA na Athari zake katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa Kiswahili katika Shule Teule za Sekondari Nchini Rwanda https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/1795 <p>Katika enzi hizi, TEHAMA inatazamwa kama kifaa cha kurahisisha maisha. Inarahisisha maisha kwa kuathiri kila uwanja wa maisha ya mwanadamu (Mikre, 2011). Athari hizi zinajitokeza katika shughuli zote za mtu wa kisasa. Katika uga wa elimu, ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya pili nao uliathiriwa sana kutokana na TEHAMA. Hali hii ilisababisha kuibuka kwa makala haya kutokana na malengo mahsusi matatu. Lengo la kwanza lilikuwa kubainisha mchango wa TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kwa wanafunzi wa kidato cha nne katika shule teule za sekondari nchini Rwanda. Lengo la pili lilikuwa kuchambua hasara za matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wa kidato cha nne katika shule teule za sekondari nchini Rwanda. Lengo la tatu nalo lilikuwa kubainisha namna ya kutumia TEHAMA katika ufundishaji wa Kiswahili nchini Rwanda. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya ushuhudiaji, usaili, na upitiaji wa maandiko. Sampuli ilikuwa walimu na wanafunzi wa Kiswahili katika kidato cha nne katika shule teule za sekondari nchini Rwanda pamoja na wazazi wa wanafunzi hao. Sampuli ilipatikana kwa mbinu ya sampuli lengwa. Utafiti ulioibua makala haya uliongozwa na Nadharia ya Uunganisho. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba TEHAMA ni nyenzo mwafaka katika ufundishaji wa Kiswahili. Hii ni kwa sababu hutumiwa kufundisha msamiati, sarufi na stadi nne za lugha hasa kwa kutumia nyeno kadhaa za kiteknolojia. Aidha, utafiti huu umebaini kwamba TEHAMA inapotumiwa vibaya inaweza kusababisha madhara makubwa kwa wanafunzi. Baadhi ya madhara hayo ni pamoja na kuamini lugha ya mtandaoni zaidi, maandishi ya mkononi (kalamu) mabaya, kuathiriwa na tabia na damaduni za nje, na kutokubaliana kati ya mwalimu na wanafunzi juu ya masomo. Mwishoni, makala imejadili namna ya kuitumia TEHAMA katika ufundishaji wa lugha ya pili hususan nchini Rwanda</p> Stanislas Munyengabire ##submission.copyrightStatement## http://creativecommons.org/licenses/by/4.0 2024-03-15 2024-03-15 7 1 155 169 10.37284/jammk.7.1.1795 Maana za Majina ya Asili ya Watoto katika Jamii ya Waasu https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/1826 <p>Makala hii inachunguza maana za majina ya asili ya watoto katika jamii ya Waasu. Malengo mahususi yakiwa kwanza kubaini majina ya asili ya watoto, na pili kueleza maana zilizobebwa na majina hayo. Utafiti huu ni wa kitaamuli hivyo umetumia usanifu wa kifenomenolojia. Watoataarifa waliohusika katika kutoa data ni 18 ambao wamepatikana kwa mbinu ya usampulishaji tabakishi na usampulishaji tajwa. Data za makala hii zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya usaili na majadiliano ya vikundi lengwa; kisha zikachanganuliwa kwa mbinu ya kusimba maudhui. Nadharia ya Uumbaji iliyoasisiwa na Sapir (1958) ndiyo iliyotumika katika makala hii. Matokeo yamebainisha majina ya asili ya watoto 145. Maana za majina haya zimegawanyika katika makundi yafuatayo: majina yenye maana zitokanazo na imani kwa Mwenyezi Mungu, mahali mtoto alipozaliwa, wanyama, misimu ya miaka na siku, majanga, vyakula na matukio ya furaha. Utafiti huu una mchango mkubwa katika kuhifadhi historia, na utamaduni uliojificha katika lugha ya Kichasu. Hata hivyo, tafiti zaidi kuhusu majina zifanyike katika jamii nyingine kwani jamii zinatofautiana katika asili, historia, shughuli za kijamii na utamaduni</p> Janeth Jafet Perida Mgecha, PhD ##submission.copyrightStatement## http://creativecommons.org/licenses/by/4.0 2024-03-15 2024-03-15 7 1 170 181 10.37284/jammk.7.1.1826 Makosa ya Kiisimu Yanayofanywa na Wanafunzi Wanaozungumza Lahaja ya Kigichugu Wanapojifunza Kiswahili Kama Lugha ya Pili https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/1842 <p>Binadamu wanahitaji lugha ili kuwasiliana na mojawapo ya lugha maarufu ulimwenguni ni Kiswahili. Kiswahili kimetafitiwa na wataalamu wengi ili kutafuta suluhisho la baadhi ya changamoto zinazokumba lugha hii na kuiboresha. Mojawapo ya changamoto na suala ambalo halijatafitiwa na utafiti huu ulikusudia kubaini ni makosa ya kiisimu ya wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya pili : Uchunguzi kuhusiana na lahaja ya Kigichugu.Utafiti huu ulitumikiza kanuni na mihimili ya nadharia ya Sintaksia Finyizi ili kuweka wazi makosa ya kisintaksia na kisemantiki yanayofanywa na wanagenzi wa Kigichugu wanapojifunza Kiswahili kama L2. Uchunguzi huu uliendelezwa nyanjani na maktabani.Nyanjani ulitekelezwa katika shule za sekondari za kutwa katika kaunti ndogo ya Gichugu kwa sababu ndiko kuna wazungumzaji asilia wa Kigichugu. Katika utafiti huu tulipaswa kuteua shule,na wanafunzi wa kufanyia utafiti. Katika uchaguzi wa shule za kutwa za kufanyia utafiti tulitumia mbinu ya sampuli kimaksudi. Katika uteuzi wa wanafunzi tulitumia usampulishaji wa kinasibu pale ambapo tulipatia wanafunzi nambari kinasibu na kuteua waliopata nambari moja hadi sita. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kutumia hojaji , insha na masimulizi . Data ya utafiti iliwasilishwa kupitia majedwali na maelezo. Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha makosa mengi ya kisintaksia na kisemantiki yaliyotokana na lahaja ya Kigichugu. Makosa haya ni kama vile: makosa ya wanafunzi wagichugu katika matumizi ya nomino, vitenzi, vipatanishi, vivumishi, vibainishi, vielezi, vihusishi na vishamirishi. Makosa haya yalipelekea si tu kuibuka kwa muundo wa sentensi usiokubalika(sintaksia) bali hata kuwepo kwa maana, tofauti na iliyokusudiwa na wanafunzi hawa au isiyoeleweka, hivyo basi kuwepo kwa makosa ya kisemantiki (semantiki leksika na semantiki mantiki). Makosa haya yalichanganuliwa kwa kutumia nadharia ya Sintaksia Finyizi na kudhihirisha ukiukaji wa kanuni za nadharia hii</p> Nancy Wanja Njagi David Kihara ##submission.copyrightStatement## http://creativecommons.org/licenses/by/4.0 2024-03-27 2024-03-27 7 1 182 192 10.37284/jammk.7.1.1842 Dhana ya Kifo katika Mashairi Pepe ya Kumwomboleza Ken Walibora kwenye Kumbi za Kulikoni za Wataalam wa Kiswahili, Africa Mashariki https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/1855 <p>Makala hii inachunguza usawiri wa dhana ya kifo katika mashairi pepe yaliyotumiwa na malenga mbalimbali katika kuomboleza kifo cha hayati Ken Walibora. Kifo kinapotokea, wanajamii huomboleza kwa namna tofautitofauti kutegemea mila na desturi za jamii husika Barani Afrika. Kifo cha Ken Walibora kilivuta hisia za malenga wengi ambao walimwomboleza mtunzi mwenzao kwa kutunga mashairi mbalimbali. Katika huko kuomboleza, malenga hawa walieleza asili, maana na madhara ya kifo cha Ken Walibora kwa jamii nzima ya Waswahili. Katika makala hii, mashairi pepe sita (6) yalikusanywa kutoka kwenye kumbi za kulikoni za wataalam wa Kiswahili, Afrika Mashariki. Mashairi haya teule yamechambuliwa ili kujibu maswali kama vile; Je kifo cha Ken kilisababishwa na nani? Je, kifo chake kilikuwa kizuri au kibaya? Je, Ken ataendelea kuishi miongoni mwa Waswahili hata baada ya kifo chake? Kifo chake kimesababisha madhara gani katika jamii ya Waswahili? Masuala haya na mengine yamedadavuliwa kwa kuchanganua mashairi teule yaliyotungwa kwa ajili ya kuomboleza kifo cha marehemu Ken Walibora. Uchambuzi huu ulifanywa kwa kuongozwa na Nadharia ya Jazanda. Kwa ujumla, Nadharia ya Jazanda ilitumika katika kupasua istiari zilizotumiwa na malenga katika kueleza asili, maana na madhara ya kifo cha Ken Walibora katika mashairi teule</p> Fred Wanjala Simiyu, PhD ##submission.copyrightStatement## http://creativecommons.org/licenses/by/4.0 2024-04-07 2024-04-07 7 1 193 211 10.37284/jammk.7.1.1855