TY - JOUR AU - Mohamed Karama PY - 2022/09/29 Y2 - 2024/03/28 TI - Ufungamanisho wa Fonolojiya Othografiya na Teknolojiya katika Kukiyand̪ika Upya Kiswahili Sanifu; Kujiokowa na Kuokowa Mustakabali wa Lahaja-Dadaze JF - Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili JA - JAMMK VL - 5 IS - 1 SE - Makala DO - 10.37284/jammk.5.1.803 UR - https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/803 AB - Lahaja za kiAmu, kiMvit̪a zafa, na lahaja nyenginezo za kiSwahili yasemekana zishakufa. Makala haya yanaonesha kuwa usuli wa matatizo haya ni mapungufu ya juhud̪i za kukisanifisha kiSwahili wakat̪i wa ukoloni. Vigezo va uwamilifu wa kut̪afaut̪isha maana, na kiwango cha matumizi wa saut̪i hiyo katika lugha, ni mambo yaliyopuuzwa na Kamati ya Lugha kwa sababu ya kut̪afut̪a unafuu wa kusanifisha. Tukifuwatʰa nadhariya-tʰetʰe ya Kina cha Othografiya, saut̪i hizi amilifu tumeziyonesha kuwa zachʰangiya katika kusoma maand̪ishi yaliyoand̪ikwa kwa sababu kiSwahili ni lugha yenye othografiya ya maonroni, yaani, kuna mnasaba wa moja kwa moja kati ya saut̪i na kiwakilishi chake kihati; kitamkwavo nrivo kiyand̪ikwavo. Kwengezeya, mfumuko wa TEKNOHAMA umeipa t̪ena, lugha ya kiSwahili, nafasi ya kufaid̪ika na saut̪i hizi kwa kutiya kila kʰitʰu katika nukt̪̪a ya kimahesabu hivo kurahisisha utambuzi wa saut̪i hizi na urahisi wa kuzitumiya katika masomi ya shuleni na kwenye t̪afsiri mashine ya makala ya kiSwahili. Ikawa nat̪ija ipatikanayo ni kukiokowa kiSanifu kut̪okana na kuziokowa lahaja dada zake. Lakini zaid̪i, ni kupatikana ut̪angamano wa lugha zot̪ʰe nchini Kenya na utambulisho muwafaka katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. ER -