TY - JOUR AU - Wanyama Ogutu PY - 2021/06/01 Y2 - 2024/03/29 TI - Halafu ya Sanaa za Ubunifu wa Kiafrika: Mtanziko Rejeleshi wa Tawala za Kiafrika JF - Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili JA - JAMMK VL - 3 IS - 1 SE - Makala DO - 10.37284/jammk.3.1.334 UR - https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/334 AB - Mwonekano wa aliyekuwa rais wa Zaire; Kukugbedu Zambanga Seseseko Mobuto kwenye Umoja wa Mataifa huko New York ulirejesha maisha ya baadaye ya ubunifu wa Kiafrika. Ufanisi wa marejeo ya ubunifu wa Kiafrika umeleta sheria, kuwapo kwa sheria za kitaifa na mikataba ya maafikiano na ujima katika baraza la mataifa la makavazi katika mataifa ya Afrika. Karatasi hii ni makala ya maoni kwa (Africa Union-AU) Jumuia ya Afrika mwaka 2021 Mwaka wa Sanaa ya Uchoraji, Turathi na Utamaduni. Dhamira ya mtafiti ni kutatua mtanziko wa urejeo wa ubunifu wa sanaa ya Kiafrika katika taifa la Afrika. Lengo limebainisha baadhi ya vikwazo vinavyofanya urejeshi wa ubunifu wa sanaa ya Kiafrika kuwa mgumu hasa katika nchi yake ya asili. Karatasi hii imechambua sauti ya kitaalam katika marejeleo ya fasihi, makala na vitabu vya kisasa kuhusu Sanaa ya uchoraji ya Afrika. Imeteua bila taratibu maalum, sampuli kadhaa za utawala wa zamani wa Uropa Afrika kama vile Uingereza, Ufaransa, na Italia miongoni mwa mengine katika mijadala yake kama mifano. Kuafiki ajenda ya Jumuia ya Afrika mwaka wa 2063, karatasi imeamua kuwa kuwapo kwa mijadala ya kina kuhusu kurejea katika makongamano ya kimataifa yaliyoandaliwa na Jumuia ya Afrika. Kurejeshwa huku kutawapa wataalamu  wa Kiafrika jukwaa la kuzidisha utafiti wa jambo la urejesho wa mali ya kitamaduni kwa taifa asilia, ili kuleta suluhu mwafaka na halisi. Mwisho, ina ombi kwa wakuu wa mataifa na nchi za Afrika walio mamlakani kuwa mstari wa mbele katika kunadi habari zaidi kuhusu turathi za kitamaduni duniani. Mataifa ya Afrika yalete kazi zake asilia, halisi na bora zaidi za sanaa ya uchoraji, minara na sanamu, vifaa vya dini, alama na ishara za kitaifa, mabaki ya mababu na kazi za sanaa bunifu zilizovurugika. ER -